TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 11, 2012

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM CHAFANYIKA DODOMA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete,akiendesha Kikao cha kamati Kuu ya Chama hicho katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM Dodoma leo,(wa pili kushoto) Rais Msataafu wa Zanzibar,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu,Dk Ali Mohamed
Shein,kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa Wilson Mkama.

Mshabuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akishangilia mara baada ya kufunga goli, katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, unaoendelea kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii dhidi ya Azam FC ya Chamazi. Mpira umekwisha na timu ya Simba imeshinda magoli 2-0 dhidi ya Azam FC yaliyofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi, mchezo wa leo ulikuwa ni wa kuvutia sana kwa kila timu lakini Simba imeonekana kutawala sana mchezo katika kipindi cha chote cha mchezo
Wachezaji wa timu ya Simba wakishagilia kwa pamoja na mashabiki mara baada ya kujipatia goli la kwanza katika mchezo wao dhidi ya Azam FC ya Chamazi.

Hiki ni kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya Mango Garden kilichoshiriki katika bonaza la Serengeti Intebar Soccer Bonanza kwa ajili ya kutambulisha Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager lililofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam na kushirikisha bar mbalimbali hapa jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa timu ya Mango Garden na Breakpoint wakichuana vikali wakati timu hizo zilipocheza katika bonanza la mpira wa miguu kwa timu za baa mbalimbali jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders.
Timu ya Lakers ya Namanga na na timu ya Temboni wakichuana kuwania mpira wakati wa mchezo wao kwenye michezo ya Serengeti Interbar soccer Bonanza kwa ajili ya kutambulisha Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager.
Kikosi cha timu ya Lakers kutoka Namanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano wao na timu ya Breakpoint.
Kikosi cha timu ya Temboni kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpamabno wao na Breakpoint.
Kikosi cha Blakepoint kikiwa katika picha ya pamoja.
Timu ya Mango Garden ikipasha kabla ya kucheza mchezo wao.
Wakati wenzake wakipata maji ya Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager Mdau Victor Makinda yeye aliamua kupoza koo kwa Dafu kama anavyoonekana hapa katika picha.
Wadau wakikamata glasi zao za Muonekano Mpya wa Dhahabu na Serengeti Lager kama wanavyoonekana hapa katika picha.
Kikundi cha muziki kikitumbuiza wakati wa mapumziko ya timu zilizokuwa zikishiriki katika bonanza hilo.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuzungumza na wabunge wa CCM katika kikao chake na wabunge hao kilichofanyika jana jioni Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.Wengine kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.
Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Muhagama akitoa maelezo ya awali kabla ya Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kuzungumza na wabunge hao. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara ) Pius Msekwa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wabunge wa CCM, katika kikao chake na wabunge hao jana katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.
Mbunge wa Simanjoro Ole Sendeka akitoa hoja zake katika kikao hicho.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na Mmiliki wa Redio Pangani Dkt Vera Pieroth alipotembelea Redio hiyo wakati wa Ziara ya Kutembelea Ukuta wa Ukingo wa Bahari Pangani.[Picha na Ali Meja]

Mwandaaji wa onyesho la mavazi la 'Lady in Red' Reloaded 2012 Asia Idarous akiwa katika picha ya pamoja na mume wake Bw. Wa Hamsini katika onyesho hilo lilinalofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serenea Dar es salaam jijini Dar es salaam, onyesho hilo pia litatumika kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga kituo cha kuhudumia watu walioathirika na madawa ya Kulevya hapa nchini. kitakachojengwa huko Kikale, Rufiji mkoani Pwani
Mmoja wa wanamitindo akipita na moja ya mavazi yaliyobuniwa kwa ajili ya siku ya wapendanao katika onyesho la mavazi la Lady In Red jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wabunifu akipita jukwaani na mwanamitindo aliyeonyesha vazi alilobuni.
Mkurugenzi wa Benchmark Production Ritah Paulsen akiwa katika pozi na kivazi chake.
Mshereheshaji wa onyesho hilo akitoa ratiba ya onyesho hilo siku huu katika hoteli ya Serena Dar es salaam.
Mtangazaji wa Clouds TV akifanya mahojiano na warembo wa zamani Jaquiline Patrick na mrembo Lisa Jensen katika onyesho hilo.
Wadau kutoka Africa Media Group wakifurahia jambo katika onyesho hilo.
Msanii Chid Benz kulia na rafiki yake Koba wakiwa katika onyesho hilo.
Wapenzi mbalimbali wa masuala ya mitindo wakiwa katika onyesho hilo.
Kutoka kulia ni Mange Kimambi, Kisa na Loveness mdau mkubwa wa masuala ya urembo ambaye kwa sasa yuko Liberia kikazi.
Jaquiline Patrick na mrembo Lisa Jensen wakipozi kwa picha katika onyesho hilo.

Bandi ya muziki wa Dansi ya Kalunde na uongozi wa hoteli ya Trinity ya Oysterbay jijini Dar es salaam, imeandaa onyesho kali katika siku ya wapendanao (Valentine Day) itakayofanyika Februari 14 duniani kote.
Akizungumza na FULLSHANGWE Mkurugenzi wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi, amesema bendi yake imejiandaa vyema kuhakikisha inatoa burudani kabambe siku ya wapendanao, ikiwa na wanamuziki wake kama Bob Ludala, Gringo Junior, Deo Mwanambilimbi mwenyewe na Debora Nyangi pamoja na wanamuziki wengine. Siku hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo Wine pamoja na zawadi zingine kemkem, huku mwanamuziki mwalikwa Shilole akishiriki katika onyesho hilo na kutoa burudani kwa kuimba nyimbo zake zote, katika usiku huo wa wapendanao. Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa bei rahisi kabisa yaani shilingi elfu 15.000 kwa kila mtu, watu wote mnakaribishwa kuja kuona burudani kutoka kwa Kalunde Band.

Rais Jakaya Mrisho KLikwete katika mazishi ya Mzee Omar Selemani ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dodoma. Mzee Suleiman alifariki dunia hospitalini ya mkoa wa Dodoma jana tarehe 9 Februari, 2012 alikokuwa amelazwa kwa matibabu. (PICHA NA IKULU)

WASANII wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mwana FA, AY, Kundi la TMK Wanaume Family na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kwa pamoja wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo siku ya Jumapili hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam huko Mbagala.
Akizungumza na wanahabari mchana huu, mratibu wa burudani katika ukumbi huo, Juma Mbizo, alisema maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yamekamilika.kama anavyoonekana mwanamuziki Mwana FA akielezea jinsi atakavyofanya makamuzi ya nguvu. Ambwene Yessayah ‘AY’ akiumwagia sifa ukumbi wa Dar Live ambao baada ya kuuona aligundua kuwa una hadhi ya kimataifa.
Chegge akielezea jinsi atakavyofunika katika shoo hiyo 'bab kubwa' kushoto ni Said Fella Meneja wa kundi la TMK.

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF, wakati alipoelezea maadalizi ya timu yake, kabla ya kushuka dimbani kwenye uwanja wa Taifa Kesho jumamosi,kumenyana na vijana wa Bakhressa yaani Azam FC ya huko Chamazi.
Kocha Milovan ameisifu timu ya Azam FC na kusema ni timu nzuri na yenye ushindani mkubwa, lakini pamoja na kwamba kuna baadhi ya wachezaji wake hawako fiti sana, wamejiandaa vyema kupambana na timu hiyo na lengo ni kupata Pointi tatu muhimu, ili kujweka vizuri katika msimamo wa Ligi kuu ya Vodacom
Naye Msemaji wa timu hiyo Ezekiel Kamwanga amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mchezo huo utakaokuwa wa kuvutia kutokana na viwango vya timu zote mbili, ameongeza kwamba kama inavyofahamika michezo mingi katika ya Simba na Azam FC inakuwa siyo ya kukamiana, hivyo ana imani kuwa mchezo wa kesho utakuwa na burudani tosha kwa mashabiki wa mpira, katika picha kushoto ni msemaji wa Simba Ezekiel Kamwanga.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi. Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dodoma leo January 10, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo
(PICHA NA IKULU)

.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma.
Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Wajumbe na Viongozi wa chama cha wamiliki wa shule Vyuo na shule binafsi (TAMONGSCO) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Viongozi hao wapo bungeni Dodoma kukutana na kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii kwa lengo la kuhimiza ushirikiano kati yao na wabunge pamoja na serikali ili kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazoikabili sekta binafsi ya elimu nchini Tanzania.
Mbunge wa Bumbuli January Makamba akiwasilisha Hoja binafsi kuhusu sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi aliyoitoa chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge toleo la 2007 ya kuliomba bunge kuazimia kwa kauli moja ,kuitaka serikali katika mkutano ujao wa saba kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini kutokana na adha wanazopata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi kwenye nyumba hizo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwasalimia viongozi na wachezaji wa timu ya Villa Squard ya Kinondoni jijini Dar es salaam waliofika bungeni hapo kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na bunge.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Hijra ya mjini Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma.

No comments:

Post a Comment