TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI LIU XINSHENG ALIYEMALIZA MUDA WAKE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu cha China kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mabalozi wateule wanaokwenda kufanya kazi nchi za nje walizopangiwa, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya Mabalozi wateule baada ya kumaliza mazungumzo nao wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kuondoa kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa

Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mohamed Shaban, akimbeba juu juu mwanachama mpya, Omar Said Hunda, aliyekuwa mgombea Udiwani Kata ya Dutumi kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi wa mwaka 2010, aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na CCM. Hapa mwanachama huyu alikuwa akipelekwa mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kukabidhi kadi yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, zilizofanyika Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, jana Februari 5, 2012.
Baadhi ya Wanachama wapya waliojiunga na Chama cha Mapinduzi CCM, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya chama hicho zilizofanyika jana Februari 5, 2012 Wilaya ya Kibaha Vijijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mafia, Abdallah Mdimu, baada ya Wilaya hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kwa ulipaji wa Ada za Wanachama, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya chama hicho zilizofanyika Wilaya ya Kibaha Vijijini jana Februari 5, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kadi ya mwanachama mpya kutoka CUF, Omar Said Hunda, aliyeamua kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, zilizofanyika Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, jana Februari 5, 2012.

No comments:

Post a Comment