TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

Watanzania watakiwa kulinda Utamaduni

Benjamin Sawe
Kitengo cha Habari
Zanzibar
Watanzania wametakiwa kulinda na kuheshimu tamaduni ili waweze kusonga mbele na kujiletea maendeleo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Lily Beleko katika mafunzo kwa maafisa wa Idara mbalimbali za serikali.
Akiongea kwenye mafunzo hayo Bi Beleko alisema lengo la mafunzo hayo ni kuelimisha umma wa watanzania kulinda,kuheshinu,ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika nyanja za kiutamaduni.
Akifungua mafunzo hayo Kamishna wa Utamaduni na Michezo Zanzibar Bwana Hamadi Bakari Mshindo alisema kuna umuhimu wa kulinda utamaduni na kuheshimu tamaduni za mataifa mengine.
“Kuna umuhimu wa kulinda na kuheshimu tamaduni zetu na tamaduni za mataifa mengine lakini tuheshimu tamaduni zile zilizo nzuri pekee na kuacha tamaduni zisisoendana na mila mna tamaduni za mwafrika”.Alisema Bwana Mshindo.
Bwana Mshindo alisema ni wajibu kwa kila mtanzania kulinda na kuheshimmu tamaduni za mwafrika na za mataifa mengine kwa ujumla.
Alisema mara nyingi kuna miradi mingi ya maendeleo inafanyika katika maeneo mbalimbali lakini tamaduni za sehemu husika zinakuwa hazifuatwi.
Aidha alisema kwa upande wa Zanzibar wameshaanza kutoa elimu jinsi ya kulinda na kuheshimu tamaduni za jamii mbalimbali

No comments:

Post a Comment