TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

SBL KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA KIFEDHA

Afisa Masoko Mwandamizi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika mikoa ya Arusha na Manyara Joan Semuguruka akitoa salamu za kampuni hiyo kwa wafanyakazi wa benki mbalimbali (hawapo pichani) zilizoshiriki hafla ya 'Bankers Gala Night' iliyofanyika mkoani Arusha mwishoni mwa wiki.SBL kupitia bia yake ya Tusker Malt ilidhamini hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki tofauti nchini wakipatiwa utaratibu kabla ya kuingia katika hafla iliyowakutanisha pamoja wafanyakazi wa benki katika tukio lililojulikana kama 'Bankers Gala Night'.Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Tusker Malt.
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Tusker Malt imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano ndani ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kibenki katika lengo la kukuza maendeleo ya uchumi nchini.
Hii ilikuwa wakati wa hafla maalum ya wadau katika sekta ya kibenki iliyodhaminiwa na bia ya Tusker Malt na kuzileta pamoja taasisi za kifedha zikiwemo benki zinazoongoza kibiashara nchini.
Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha mwishoni mwa wiki ilitoa fursa maalum kwa wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kibenki kuzungumza pamoja changamoto mbalimbali zinazoikabiri sekta ya fedha nchini.
Akizungumza wakati wa halfa, Afisa wa kampuni ya Serengeti wa Nyanda za Juu Kaskazini, Bw. Mapendo, alisema kuwa kampuni yake itaendelea kufanya kazi karibu na wadau wote ili kuleta maendeleo ya uchumi nchini.
Alisema hafla hiyo imetoa nafasi kubwa kwa wadau wa taasisi za kifedha haswa za kibenki kuungana pamoja na kubadilishana mawazo jinsi gani wanaweza kusonga mbele na kupanua sekta hiyo muhimu katika uchumi wa taifa.
Mapendo alisema SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt imedhamini hafla hiyo na kwamba itaendelea kushirikiana na sekta hiyo katika mambo mbalimbali kulingana na uwezo wake kifedha.
“Sekta ya kibenki inakuwa kwa kasi sana na hivyo kutoa fursa nyingi mbalimbali kwa nyanja zote mbili za kibiashara pamoja na ajira kwa watanzania walio wengi. Na fursa hizo huonekana zaidi wakati wa matukio muhimu kama haya.
"Tunaamini kwamba kupitia hafla hii, jamii ya wafanyabiashara itachukua na kuzifanyia kazi fursa zilizopatikana. Tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa tukio hili.
“Bia ya Tusker Malt imekuwa ikidhamini matukio mbalimbali nchini lakini mwaka huu tumedhamiria kuweka mkakati madhubuti ambao unaangalia zaidi biashara katika makampuni na makundi mengine ndani ya jamii,” aliongeza.
Kwa upande wake mwakilishi wa waandaaji wa tukio hilo Peter Morgan aliishukuru Tusker Malt kwa udhamini wake na kusema kuwa ni vyema SBL ikaendeleza wazo hilo zuri la kuwa na matukio kama hayo katika kanda mbalimbali nchini.
“Hili ni tukio la kukumbukwa ndani ya jamii ya wadau wa taasisi za kibenki. Tumeweza kuzikutanisha taasisi mbalimbali za kifedha pamoja si kukutana tu bali pia kuweza kubadilishana mawazo jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabiri sekta ya kibenki. Tunaishukuru bia ya Tusker Malt kwa udhamini wake,” alisema.

No comments:

Post a Comment