TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 7, 2012

WABUNGE WAKUTANA NA WATAALAM WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012.

Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo akitoa maelezo ya awali kuhusu maendeleo ya kazi za maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyopangwa kufanyika nchini wakati wa semina kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi iliyofanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma,Hata hivyo waziri Mkulo amefafanua kuwa serikali itahakikisha kuwa sensa hiyo inafanyika kama ilivyopangwa kwa ubora na ufanisi ikilinganisha na sensa zilizopita.
Manaibu waziri wa Fedha Gregory Theu (kushoto) na Pereira Silima(kulia) wakifuatilia masuala mbalimbali kuhusu Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu wakati semina iliyowahusisha wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi wakifuatilia taarifa mbalimbali kuhusu maandalizi ya sense ya watu na makazi itakayofanyika mwaka walipokutana na wataalam kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu jana mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Sensa Dkt. Albina Chuwa akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi kuhusu zoezi la sensa ya watu litakalofanyika nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu jana mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment