TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

SERIKALI YAOMBWA KUENDELEA KUBORESHA MAKAZI YA POLISI

Na Ashura Mohamed - Arusha
Serikali kupitia Wizara ya ulinzi na usalama imeombwa kuendelea kuwaboreshea makazi askari polisi ili waweze kuishi katika mazingira mazuri na kuongeza ufanisi katika kazi.
Akizungumza katika sherehe za kukaribisha mwaka mpya 2012 zilizoandaliwa na jeshi la polisi mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni hakimu mkazi mkoani arusha Charles Magesa amesema kuwa ili kuongeza ufanisi katika kazi pia ni vyema polisi nao wakaboreshewa makazi yao.
Magesa ameongeza kuwa taasisi yeyote inayofanya kazi ya kuihudumia jamii ni lazima changamoto zake zishughulikiwe hivyo amewataka polisi kufanya kazi kwa uwazi na umakini zaidi ili jamii inayoizunguka iweze kuwa na imani nao.
Aidha amesema kuwa jamii ni lazima iweze kulisaidia jeshi la polisi katika kuhakikisha kuwa linatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwapa ushirikiano zaidi ili kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andeng’enye amesema kuwa vitendo vya uhalifu katika mkoa wa Arusha vimepungua ukilinganisha na mwaka 2010.
Andeng’enye amesema kuwa jumla ya matukio 25,833 yaliripotiwa mwaka 2011 ikilinganishwa na matukio 26,698 yaliyoripotiwa kwa mwaka 2010 ambapo ni pungufu ya matukio 865.
Amefafanua kuwa matukio hayo yamegawanyika katika makundi manne ni makosa dhidi ya binadamu,makosa dhidi ya mali,makosa dhidi ya maadili ya Jamii na makosa ya usalama barabarani ambapo ni pamoja na mauji,kubaka,kulawiti.wizi wa watoto,kutupa watoto,unyang’anyi wa kutumia silaha,unyang’anyi wa kutumia nguvu,wizi wa magari,wizi wa mifugo,ajali za moto na makosa ya usalama barabarani.
Hata hivyo kamanda Andengenye ametaja changamoto wanazokabiliana nazo kwa mwaka 2012 ni pamoja na Tatizo la ajira kwa vijana ni changamoto nyingine inayosababisha kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu kutokana na vijana hao kutokuwa na namna ya kutafuta kipato hivyo inakuwa rahisi kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment