TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

WAISLAMU ARUSHA WALAANI KIKUNDI CHA BOKO HARAMU

NA GLADNESS MUSHI  - ARUSHA
VIONGOZI wa dini ya kiislamu mkoani Arusha, wameongoza kongamano maalumu la kulaani mauaji yanayofanywa na kikundi kidogo cha kiislamu chenye msimamo mkali cha Boko haramu nchini Nigeria dhidi ya madhebebu ya dini ya kikristo. . Wakizungumza kwenye kongamano la amani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti Al hamadiyya jijini hapa,walidai kuwa hakuna maagizo ya mwenyezi mungu yanayotoa mamlaka kwa kikundi hicho ama mtu yoyote kutekeleza mauaji hayo dhidi yawaumini wa dini nyingine. Amiri na mbashirimkuu wa jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhly aliwaomba waislamu kote duniani kuungana na kulaani vitendo vya kinyama kama hivyo vinavyofanyika kwa kutumia mgongo wa uislamu .Aliwaomba watanzania kuwalilia wananchi wote waliouawa kutokana na kikundi hicho cha Boko haramu nchini Nigeria,na aliiomba serikali nchini humo, kukakikisha inadhibiti mauaji hayo na kukishughulikia kikundi hicho kinachotumia mgongo wa uislamu. ‘’Sisi waislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya uvunjifu waamani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini wenzetu ,hakuna maandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini nyingine ‘’alisema Choudhly. Aidha aliongeza kwa kuwataka viongozi wamadhehebu ya dini nchini kusimama imara katika kutetea amani na kujiepusha na uchochezi,kwani taifa linawategemea sana katika kuepusha machafuko yanayoweza kuibuka . Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuheshimu viongozi waliopo madarakani na kuacha kupinga kila kitu kinachotamkwa na kiongozi aliyeko madarakani, badala yake watoe mchango wakusukuma maendeleo ya taifa hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine. Naye Sheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini, Mzafara Ahamad,alisema kuwa lengo lakongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba amani na kulaami mauaji ya kikatili yanayoongozwa na kikundi haramu cha kiislamu nchini Nigeria. Alisema kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa Ahmadiyya Muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa ajili ya ukarabati ulioanza mwishoni mwa mwaka jana . Kwa upandewa sheikh mkuu wa Ahamadiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dini nchini kutawala kiuadilifu huku wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa sehemu yakuleta mitafaruku ya kidini . Ameyasihi madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba amani,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri uvunjifu wa amani kwa maslahi yao binafsi. Naye meya wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi hao kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo. Aliwasihi viongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa nchini na duniani kote.

NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
WANASAYANSI nchini kwa kushirikina wenzao duniani, wametakiwa kufuatilia hewa ya ukaa katika misitu iliyopo nchini, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, ambayo huathiri upatikanaji wa mvua kwa msimu .
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi kwa niaba ya Waziri wa mali asili na utalii, Ezekiel Maige, ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa 3 wa wadau wa mazingira, kuhusu uhifadhi endelevu na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, unaofanyika Jijini Arusha na kushirikisha wanasayansi 53 kutoka duniani kote.
Alisema kuwa Tanzania tayari wanampango wa Nafoma unaojihusisha na upandaji miti ya uhifadhi mazingira, ambayo ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za mazingira hususani hewa ya ukaa inayozalishwa nchini.
“Watu lazima wapande miti kwa wingi na siyo bora miti tu, bali wapate ushauri aina ya miti watakayopanda, tukifanya hivi tutapata mvua kwa wakati unotakiwa kwa sababu mpango huu umefanikiwa Mkoani Iringa, ambapo zamani walikuwa hawapati mvua kwa wakati na hewa ilikuwa mbaya ila baada ya kupanda miti mingi sasa mvua huja kwa mpango na hewa safi” alisema Maimuna.
Aidha alisema kuwa huwenda wananchi wengi wakashindwa kupanda miti na kuisubiri kukomaa na kuvuna, badala yake wanapopata shida huivuna kabla ya kukomaa, ili kuondoka na na tatizo hilo aliwashauri wananchi kubuni mradi wa ufugaji nyuki kwa kuweka mizinga katika miti watakayootesha shambani mwao.
Naye Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu alisema kuwa, asilimia 80 ya watanzania hutumia nishati ya kuni na mkaa na asilimia 10 tu wanatumia umeme, hali mbayo ni hatari kwa taifa, katika uharibifu wa mazingira.
Alisema kuwa serikali ili kuondokana na tatizo hili, ipo mbioni kufanya juhudi za makusudi kutoa ruzuku katika nishati ya gesi, ili wananchi wengi wamudu gharama ya gesi na kuitumia, na kuondokana na matumzi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa yakisababaisha uharibifu mkubwa wa mazingira nchini.

No comments:

Post a Comment