TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

WATAKAOPATA AJALI KULIPWA MILIONI MBILI

NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
Madereva mbalimbali hasa wa masafa marefu wanatarajia kunufaika na bima ya maisha kwa kupewa Kiasi cha Milioni Mbili kutoka katika Bima ya jubilee hali ambayo itawafanya madereva walio wengi kuweza kujikwamua katika suala zima la umaskini, ulemavu, vifo ambavyo vinasababishwa na ajali hizo.
hayo yamebainishwa na Meneja wa kanda ya kaskazini kutoka katika bima ya Jubilee(JUBILEE INSUARANCE} Bw Charles Magori wakati akiongea na vyombo vya habari jijini hapa mapema wiki hii.
Bw Magori alisema kuwa Bima ya maisha ambayo itaweza kuwafikia madereva wengi zaidi itakuwa na manufaa makubwa sana kwa kuwa baadhi ya madereva hasa wale wa masafa marefu wamekuwa katika maisha ya taabu mara ya kupata ajali.
Alibainisha kuwa mara baada ya kupata ajali asilimia kubwa ya madereva hao hushindwa kufikia malengo yao kwa kuwa tayari wanakuwa wameshapata vilema vya maisha,vifo ambapo hupelekea kukosa garama za mazishi hali ambayo ni hatari kwa maisha ya sasa.
“tulichoweza kugundua ni kwamba hawa madereva mara nyingi wanakuwa katika hatari mbaya sana ya ajali na hivyo hata kwa wale ambao wanakufa familia zao zinakuwa katika wakati mgumu sana huku nyingine nazo zikiwa hata kwenye hatari ya kukosa fedha kwa ajili ya mazishi lakini tunachoweza kukifanya hapa ni kuhakikisha kuwa tunasaidia jamii kwa kuwapa milioni mbili kwa ajili ya maandalizi mbalimbali'alisema Bw magori
Awali alisema kuwa mbali na kutoa bima hiyo hasa kwa madereva pia kwa sasa zoezi hilo la kutoa bima litaenda sanjari na elimu mbalimbali ambazo zinahusu uimu wa bima kwa maisha ya mtanzania kutokana na kuwepo kwa matukio mbalimbali ambayo yana historia ya kutokea sana kwa ndani ya jamii.
Bw. Magori alisema kuwa endapo kama madereva hao wataweza kupata elimu hiyo ya bima basi watanufaika kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo kwa sasa bado baadhi ya jamii hazina mwitikio wa masuala ya bima.
Pia aliwataka wananchi wote kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kutafuta elimu mbalimbali za bima kwa kuwa bima ni msingi wa maisha ya kila mtanzania hususani kwa sasa ambapo jamii nyingi kukosa elimu hali ambayo inachangia kuwepo fikra hasi juu ya uimu wa bima kwa maisha ya mtanzania wa sasa.

No comments:

Post a Comment