TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 17, 2013

Mapigano yazuka Baina ya Wakulima na Wafugaji katika kijiji cha Kambala Mvomero-Morogoro.

Wafugaji wa kijiji cha Mvomero-Morogoro wamewavamia wenzao Wakulima na kuwapiga, na kisha kusababisha Mejeruhi ya watu wanne(4) kutokana na mzozo unaoendelea kati ya wafugaji(wamaasai) na wakulima kutika kijiji hicho cha Kambala Mvomero,  Pia wananchi wa kijiji hicho wameilaumu serikali kwa kushindwa kutoa suluhisho la mzozo huo baina ya Wafugaji na Wakulima ambalo kwa sasa linazidi kukua na limekua swala la mda mrefu sasa. Taarifa zinasema kuwa Wafugaji hao waliamua tu kuvamia wenzao wakulima na kuwapiga pasipo sababu ya msingi na huku Polisi wa eneo hilo kushindwa kuchukua hatua inayotakiwa mapema.  Mkuu wa wilayani hapo (Mvomero) Anthony Mtata amewaomba wananchi hao waathirika wa tukio hilo kutojichukulia hatua mkononi na kuwahakikishia wakulima hao kwamba, waliohusika na tukio hilo lazima watiwe nguvuni.

Utangulizi
 
Wilaya ya Mvomero ni moja kati ya Wilaya 5 (tano) za Mkoa wa Morogoro. Wilaya hii imeanzishwa mwaka 2002 na ina jumla ya kilomita za mraba 7,325 sawa na 9.98% ya eneo la Mkoa. Wilaya ina jimbo moja la Uchaguzi wa Ubunge la Mvomero linaloanzia Mgeta kwenye Milima ya Uluguru hadi Turiani kwenye Milima ya Nguu. Wilaya inapakana na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kwa upande wa Kaskazini na Wilaya ya Kilosa kwa upande wa Magharibi. Kwa upande wa Kusini inapakana na wilaya Morogoro na kwa upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na wilaya za Bagamoyo na Handeni.
 
 
UMBILE LA ARDHI
 
Umbile la Wilaya ni kama mwezi mchanga unaoambaa ambaa Manispaa ya Morogoro kuelekea Kaskazini. Kijiografia Wilaya imegawanyika katika nyanda tatu kama ifuatavyo:-
•  Nyanda za juu ( Highland and Mountainous Zone):
Nyanda hizi hasa ni zile za milima ya Uluguru na Ungulu. Eneo hili limechukua 25% ya eneo la Wilaya. Nyanda hizi zipo kwenye mwinuko wa mita 1200 – 2000 kutoka usawa wa bahari. Nyanda hizi zinafaa kwa mazao ya biashara kama vile; kahawa, Hiliki na mazao ya chakula kama mahindi, maharage, mboga, ndizi, viungo na matunda.
•  Nyanda za chini (Low and Semi Mountainous Zone):
Nyanda hizi zipio kwenye mwinuko wa mita 800 hadi 1200 kutoka usawa wa bahari. Nyanda hizi hustawisha mazao kama mahindi, mihogo, mtama kwa chakula na mazao ya biashara ni Miwa na Alizeti.
•  Nyanda za Tambarare (Savannah Zone):
Nyanda hizi zipo kwenye mwinuko (altitude) wa mita 600 – 800 kutoka usawa wa bahari. Mazao yanayostawi kwenye nyanda hizi ni mpunga, Mahindi, na Mihogo kama mazao ya chakula, na mazao ya biashara ni Miwa, Pamba na Katani.
 
 

IDADI YA WATU 
 
Kutokana na sensa ya mwaka 2002, Wilaya ina wakazi wapatao 260,525 kati yao wanaume ni 131,256 na wanawake 129,269. Jumla ya Kaya katika Wilaya ni 58,314 zenye wastani wa watu 4.5 kwa kila Kaya. Ongezeko la watu kwa mwaka ni 2.6%.Wilaya inaonyesha kuwa na nguvu kazi ya watu 142,755 sawa na 54.8% ya wakazi wote 260,525.
 
Hali ya Hewa 
Kwa kawaida Wilaya inapata mvua mara mbili kwa mwaka. Mvua za vuli, ambazo huanza mwezi Oktoba hadi Januari. Mvua za masika, ambazo huanza mwezi Februari hadi Mei/Juni. Wilaya hupata wastani wa 1900mm za mvua kwa mwaka. Hali ya joto ni nyuzi 29 0 C
Utawala
Halmashauri ina jimbo moja la uchaguzi ambalo ni Mvomero na Bw Paul C. Kiyumbi ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri na Bibi S. Linuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
 
Sekta ya Kilimo
 
Hali ya Kilimo

Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Wilaya ya Mvomero. Asilimia 84.1% ya wakazi wa Wilaya wanajishughulisha na Kilimo na ufugaji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 549,375 na eneo linalolimwa ni Hekta 247,219 sawa na 45% ya eneo lote linalofaa kwa kilimo. Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni Hekta 20,579 lakini eneo linalomwagiliwa ni Hekta 5,281 Idadi ya wakulima ni 142,755 ambao kati yao wanaume ni 71,922 na wanawake ni 70,833.
 
Maeneo ya uzalishaji
Katika kutekeleza mpango huu, Halmashauri iLiainisha maeneo maalumu ya kuanzia katika mpango huu kwa mwaka 2007/2008.
Maeneo yamegawanywa katika Kanda tano, zenye Kata kumi na moja (11) na vijiji 44 kati ya vijiji 132 vya Wilaya ya Morogoro, Mazao yaliyohusishwa ni Mpunga, Mahindi na jamii ya mikunde.
Upatikanaji wa pembejeo.
Pembejeo zilipatikana vizuri katika maduka ya mawakala wa pembejeo walioko mjini. Pembejeo zenye ruzuku pia upatikanaji wake ulikuwa mzuri, wakulima walipata mahitaji yao kupitia mawakala.
Pembejeo za ruzuku zilizopatikana ni mbolea aina ya urea tani 76, DAP tani 20 na mbegu za mahindi 2.2. Ambazo zilinunuliwa na mawakala na kuuzwa kwa wakulima. Wakulima walipata pembejeo kupitia mawakala waliopo vijijini na mjini.Vile vile wakulima katika vijiji 15 vya wilaya waliweza kuzalisha mbegu bora za mahindi tani 10 na kuwauzia wakulima wenzao kwa bei nafuu .Hii iliwezekana baada kupata mafunzo ya kuzalisha mbegu bora chini ya mradi wa ASDP.
 
Ushirika na Masoko
 
Hali ya Ushirika:
Shughuli za Ushirika katika Wilaya ni za muhimu kwa kuzingatia kuwa idadi kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Mvomero ni Wakulima wanaotegemea Kilimo na shughuli za biashara ndogondogo. Hata hivyo, ustawi wa vyama vya kilimo/Mazao bado sio wa kuridhisha japokuwa uanzishaji wa vikundi vya uzalishaji umekuwa ukijitokeza katika baadhi ya maeneo.
Pamoja na mikakati ya kuhakikisha Ushirika unawanufaisha Wananchi, huduma hii kwa sasa inatolewa na vyama 22. Vyama 17 vikiwa ni vya Ushirika wa Akiba na Mikopo, chama kimoja (1) kikiwa kinajishughulisha na Kilimo cha Mbogamboga na kuuza Pembejeo Mgeta. Chama kimoja (1) kinajishughulisha na Kilimo cha umwagiliaji Dakawa. Vyama viwili ambavyo ni Laramatak cha Kambala ni chama cha Ushirika wa wafugaji na Turiani AMCOS ambacho ni chama Ushirika cha Kilimo. Hivi ni vyama ambavyo tayari vimesajiliwa.
Vilevile kuna vyama 2 vya Ushirika wa Akiba na Mikopo kutoka Maskati na Melela viko kwenye mchakato wa kusajiliwa na kimoja cha ufugaji wa Mbuzi wa Maziwa kutoka Mgeta nacho kiko katika mchakato wa kusajiliwa.
Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo
Wilaya ina jumla ya vyama vya Akiba na Mikopo 17 ambavyo vina jumla ya wanachama 6726, Me 4597, Ke 2129 vikiwa na Hisa 435,091,000/=, Akiba 473,790,000/= na Amana 411,622,000/=. Pia vimeweza kutoa Mikopo yenye thamani ya Tshs. 5,177,457,000/= ."Hali Halisi angalia Jedwali A"
Mbali na kuwa na SACCOS 17, Wilaya ina Vyama 5 (vitano) vya Ushirika ambavyo vinajishughulisha na kilimo cha mbogamboga, maduka, umwagiliaji, kilimo cha nafaka na ufugaji. Vyama hivi vina jumla ya wanachama 961, Me 760 na Ke 201. Pia vina Hisa zenye thamani ya Tshs. 9,542,000/=

Barabara

Hali ya barabara kwa kilometa

Wilaya ya Mvomero ina mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa km. 831.47 ambazo zinagawanyika katika makundi makuu manne:-
Barabara za Mkoa km. 232.89 
Barabara za Wilaya km. 79.60 
Barabara za Vijiji km. 406.90
Barabara kuu na za Mkoa zinazopitika ndani ya Wilaya ya Mvomero zinahudumiwa na Wakala wa barabara wa Mkoa wa Morogoro (TANROADS) na barabara za Wilaya na za Vijiji zinahudumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
Barabara kuu na za Mkoa zinazopitika ndani ya Wilaya ya Mvomero zinahudumiwa na Wakala wa barabara wa Mkoa wa Morogoro (TANROADS) na barabara za Wilaya na za Vijiji zinahudumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
Mpango kazi wa Matengenezo ya Barabara Mwaka Wa Fedha 2008/2009.
Halmashauri inahudumia barabara zake kwa kuzifanyia matengenezo yafuatayo:-
Matengenezo ya kawaida km. 206.4 Tshs. 144,700,000.00
Matengenezo ya sehemu korofi km. 32 Tshs. 40,000,000.00
Matengenezo ya muda maalum km 19 Tshs. 192,000,000.00
Matengenezo ya Madaraja na Makalvati Tshs. 20,000,000.00
Usimamizi wa matengenezo Tshs. 24,600,000.00
JUMLA Tshs. 421,300,000.00


Barabara Kuu km. 112.08 
Matengenezo/ukarabati wa barabara
Wilaya ya Mvomero inahudumia barabara zake kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwemo Mfuko wa Barabara (Roads Fund), Mradi wa Usafiri na Uchukuzi Vijijini (VTTP) na Mpango wa Maendeleo ya barabara vijijini (LGTP).
Aina za matengenezo
Matengenezo ya kawaida ( Routine Maintenance)
Matengenezo ya sehemu korofi (Spot Improvement)
Matengenezo ya muda maalum (Periodic Maintenance)
Matengenezo ya Madaraja na Makalvati (Bridges and culverts)
Katika mwaka wa fedha 2008/2009 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imejipangia kufanya matengenezo ya barabara zake kwa kutumia fedha kutoka vyanzo mbalimbali kwa jumla ya Tshs. 668,300,000/= kama ifuatavyo:-
Mfuko wa Barabara (Roads Fund) 


Hifadhi ya Mazingira
Hali ya utunzaji mazingira na uzingatiaji wa sheria ya mazingira ya 2003
Halmashauri imekuwa inatekeleza majukumu yake kufuatana na sera ya misitu ya 1998 na sheria ya misitu ya 2002, na ya wanyamapori ya 1998 “Ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhi na kuzingatia matumizi endelevu”.
Halmashauri pia imekuwa ikitekeleza sera na sheria ya Mazingira ya 1997 na 2004 ” kuhusu Uzingatiaji wa athari za kimazingira popote tulipo”.
Halmashauri inatoa elimu kwa wananchi juu ya miti ya Misederela na kutunga sheria ndogo za udhibiti upandaji wa miti hiyo jirani na misitu ya hifadhi. Vijiji 44 vya kata za Melela, Doma, Tchenzema, Mvomero, Turian na Hembeti vimepatiwa mafunzo ya hifadhi ya mazingira, kati ya vijiji 101 vya wilaya ya Mvomero.
Elimu ya Mazingira na athari za uchomaji moto misitu ilitolewa. kwa kipindi cha Julai hadi Juni 2007/2008, Halmashauri ilitumia gari la wizara Mobile video van kutoa elimu na kuonesha picha za video katika vijiji 8 vilivyo chini ya mpango wa usimamizi shirkishi wa misitu (USM) na katika vijiji vya Melela, Mlandizi na Nyandira. Katika utoaji wa mafunzo hayo mwitikio umekuwa mkubwa na mabadiliko yamekuwa makubwa kwani athari za mazingira zimepungua.

Mikakati
Halmashauri imefanya doria za mara kwa mara katika barabara kuu za Iringa na Dodoma kwa ajili ya udhibiti wa mkaa. Hata hivyo jamii kwenye vijiji wamefundishwa sheria ya Misitu ya 2002 na kisha kuunda kamati za udhibiti wa uharibifu wa mazingira za vijiji.
Sheria ndogo za kuhifadhi misitu, na kudhibiti uchomaji wa moto zimeundwa katika vijiji vya Tchenzema, Nyandira, Kibuko, Mwarazi, Kanga, Dihinda, Mziha na Difinga. Mchakato wa kutunga sheria ndogo za kudhibiti uchomaji moto misitu katika vijiji nane vya mpango wa usimamizi shirikishi unaendelea.
Katika kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji vya Manza, Wami Dakawa, Makuyu, na Tangeni wananchi wameainisha njia za kudhibiti uchomaji moto ikiwa ni pamoja na kuandaa sheria ndogo. Katika maeneo yaliyotajwa sheria zimekamilika na zinatumika.
Kamati za Mazingira za vijiji (Village environmental Management committees) zimeundwa ama kuimarishwa na kwa kushirikiana na Serikali za vijiji , zimesaidia katika kuwakataza watu kuvamia misitu na kwenda kuishi au kuanzisha mashamba bila idhini ya serikali ya kijiji husika. Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti matukio ya moto yanayotokana na uaandaji wa mashamba au malisho ya mifugo.
Katika kipindi cha 2007/2008 kamati za mazingira katika vijiji vya Tchenzema, Nyandira, Kibuko, Mwarazi Manza, Wami Dakawa, Makuyu, Nyandira, Tangeni, Mangae, Msongozi na Maharaka ziliundwa na kupatiwa Mafunzo.

Ardhi
Wilaya ya Mvomero ni moja wapo kati ya Wilaya zilizogubikwa na migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Morogoro.Mingi ya migogoro ni ya zamani na imeshughulikiwa tangu enzi za Wilaya mama ya Morogoro Vijijii ikiwa ni pamoja na kuundiwa Tume za Kitaifa. Migogoro mikubwa kati ya migogoro mingi ya ardhi Wilayani ni pamoja na:
Mgogoro kati ya Kijiji cha Melela na Ushirika wa Twende Pamoja
Mgogoro katika kijiji cha Melela kati ya wakulima wa Ushirika wa Twendepamoja kutoka Manispaa ya Morogoro na wafugaji ni wa muda mrefu. Wakulima kutoka mjini Morogoro walivamia ardhi katika kitongoji cha Mela mwaka 1999 kilichotengwa na wanavijiji kwa ajili ya wafugaji. Huu mgogoro ulipelekwa mahakamani na Twende pamoja walishindwa kwenye kesi sasa wameungana na wanakijiji waliokuwa wanaishi Mela na wameishitaki Halmashauri, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Melela na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mela walipwe fidia ya Sh. bilioni 10 kwa ajili ya mashamba waliyonyang'anywa. Bado kesi ipo Mahakamani na hivi karibuni Waziri Mkuu ameunda tume ya kuchunguza mgogoro huo na bado hatujajua majibu ya Tume.
Mgogoro kati ya shamba la Kipunguni Enterprises Ltd na vijiji jirani:
Mgogoro mwingine ni kati ya Kipunguni Enterprises LTD mmiliki wa shamba lenye ukubwa wa karibia ekari 98,000 linaloenea katika vijiji vitano vya Mangae, Msongozi, Mkata, Melela na Magali. Mashamba na makazi ya wanavijiji yamo ndani ya hilo shamba ambalo hapo awali lilikuwa likimilikiwa na MODECO na baadae mwaka 1975 likauzwa kwa zabunikwa Kipunguni Enterprises Ltd. Uongozi wa wilaya una mpango wa kuwasiliana na mmiliki ili aachie kwa hiari maeneo yaliyokaliwa na wanavijiji ili iwe ardhi ya vijiji.




Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi 

Mipango ya matumizi bora ya ardhi imeandaliwa katika vijiji 20 kati ya vijiji 101 vya Wilaya. Malengo ya mwaka 2008/2009 ni kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 11.


Utoaji hati na vyeti vya ardhi 
Vijiji vyote 101 vimepimwa mipaka kwa ufadhili wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ramani zimekamilika hivi karibuni. Hatua inayofuata ni kutayarisha vyeti vya ardhi ya Vijiji kwa kuanza na vijiji 20 ambavyo tayari vimeandaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi. Baada ya hapo vijiji vitapewa cheti cha ardhi ili Ofisi za vijiji zianze kutoa hati za hakimiliki za kimila kwa eneo la kila mwanakijiji. Wanakijiji watazitumia hati hizo kama dhamana ya upatikanaji wa mikopo .

Upimaji mashamba
Upimaji wa ranchi 50 za wafugaji eneo la Dakawa umeshaanza lakini bado haujakamilika kutoka na ugumu wa upatikanaji wa vifaa vya upimaji.
Utoaji hatimiliki za mashamba
Utoaji wa hatimiliki za mashamba utafanyika baada ya kazi ya upimaji ranchi 50 kukamilika.
Utwaaji wa mashamba yasiyoendelezwa
Mashamba 34 yamewasilishwa kwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kubatilisha hatimiliki ambayo ni kati ya mashamba 68 yenye ukubwa wa hekta 54,193 yaliyotambuliwa kuwa hayaendelezwi.
Ufugaji nyuki
Katika kipindi cha 2007/2008 Halmashauri, watu binafsi na mashirika yasiyo ya Kiserikali imevuka lengo la kutundika mizinga 500 ambapo mizinga 629 imetundikwa sehemu mbalimbali na mingi ya hiyo ina asali. Bado utaratibu unaendelea wa kusimamia zoezi hilo ili liwe la manufaa kwa jamii kama njia ya kuinua kipato. Sekta inafanya utaratibu wa kupata soko la uhakika hapa mkoani Morogoro na Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment