TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, September 19, 2013

SEKONDARI YA ILIBORU YAFUNGWA

Na :Pamela Mollel, Arusha

SHULE ya Sekondari Iliboru, iliyopo Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, imefungwa na Serikali kwa muda usiojulikana baada ya kuwepo kwa hofu ya kuchomwa moto.Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa, tangazo la kufungwa shule hiyo lilitolewa jana asubuhi na Mkuu wa shule hiyo, Bw.Julius Shila baada ya kushauriana na Bodi ya Shule hiyo.


Akizungumza kwa njia ya simu jana, Bw. Shila alikiri shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana ambapo uamuzi wa kuifungua utatolewa na Ofisi ya Mkoa wa Arusha."Ni kweli shule imefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu ambapo wanafunzi wote wamerejea nyumbani, kuna taratibu ambazo wanapaswa kuzifuata," alisema Bw. Shila.

Baada ya tangazo la kufungwa kwa shule hiyo, inadaiwa zaidi ya wanafunzi 800 kuanzia kidato cha kwanza hadi sita, wameathirika wakiwemo wanaofanya mitihani ya mwisho.

No comments:

Post a Comment