TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 17, 2013

TPSF YAWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA KUJIENDELEZA KIUCHUMI

Posted: 16 Sep 2013 05:09 AM PDT

 TAASISI yaSekta Binafsi (TPSF) imewataka vijana nchini wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia fursa za kibiashara zilizopo ili kukuza kipato chao na taifa kwa ujumla, U shauri huo umetolewa na Mwenyekiti waTaasisi ya Sekta Binafsi(TPSF), Reginald Mengi,m wishoni mwa wiki jijini Dares Salaam wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo ya heshima Mwenyekiti na  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Helvetic Solar Contractors LTD , Patrick Ngowi, kama njia ya kutambua mafanikio aliyoyapata katika biashara.


"Vijana wana wajibu wa kutumia vipaji vyao na elimu kujiendeleza kibiashara ili waweze kukua kibiashara na kusaidia taifa kuboresha ustawi wa jamii ," alisema. Alisema kijana liyetunukiwa tuzo hiyo ameweza kufanikiwa kibiashara akiwa na umri wa miaka 28, hivyo vijana wengine wanatakiwa kuiga mfano huo.Alisema taifa linategemea vijana hivyo wanatakiwa kujituma ili waweze kuwa wafanyabiashara wakubwa na matajiri wasaidie jamii inayowazunguka.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, a l i s ema k i j a n a  h u y o amefanikiwa kupitia biashara ya ukandarasi wa kutumia teknolojia ya nishati ya jua (Solar Power contractor) kusambaza umeme."Kijana huyu kwa sasa anamiliki makampuni mbalimbali ya kusambaza na kutumia nishati ya jua katika nchi tatu za Afrika Mashariki," alisema.Alisema makampuni hayo yamejumuishwa kundi la kampuni za Helvetic Group of Companies lenye jumla ya mapato ya mamilioni ya dola.

No comments:

Post a Comment