TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, September 16, 2013

‘Sugu’: Ndugai aliamuru askari wanipige bungeni



NI kauli iliyotolewa na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Chunya. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema tukio la kupigwa ngumi na askari ndani ya Ukumbi wa Bunge lilisababishwa na  amri ya Naibu Spika, Job Ndugai na wala siyo askari.
Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai  askari.
‘Sugu’ alitoa kauli hiyo  wakati akiwahutubia wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo ziarani  mkoani Mbeya  wakifanya  mikutano na wananchi kwa lengo la kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na  wabunge wengine bungeni hivi karibuni.
‘ Sugu’ alidai kuwa Ndugai ni adui wa wapinzani bungeni na kwamba kwa vyovyote vile ilikuwa vigumu kuvumilia kwa mtu yeyote baada ya askari kuanza kupiga wabunge kutokana na amri ya  Ndugai. Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema kitendo alichofanyiwa Sugu hakikuwa kibaya kwake peke yake, bali hata wananchi waliomchagua.
Hata hivyo, Dk Slaa  alisema kwa upande mwingine ili heshima ya Bunge lolote lile duniani  iwepo, ni lazima wabunge watandikane makonde ndani ya Bunge  na si vinginevyo hivyo hashangai kwa kilichotokea kwa Sugu bungeni.
Je, yanapotokea hayo Heshima ya Nembo hii inakuwa wapi
Dk Slaa, alimjia juu Ndugai akisema alikiuka Kanuni za Bunge kwa kitendo hicho na  kubainisha kwamba kanuni za Bunge zipo wazi kabisa  kwamba iwapo itatokea vurugu ndani ya Bunge anachotakiwa kukifanya ni kuahirisha Bunge kwa wakati huo.
Pia alisema askari ambao ni  wapambe wa Bunge ‘Sargent at arms’ ndio wenye mamlaka ya kuingia ukumbini na endapo itatokea nguvu ya ziada hao ndio wanaotakiwa kisheria na siyo kuwaita askari wa nje ya Bunge kuingia ndani.
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, inapenda kuwapa Pole sana wale wote wanaoendelea kuishi na kuwa na wasiwasi juu ya Muonekano wa Kadri ya Siku zinavyosogea kuelekea Uchaguzi, Kikubwa ni kuhakikisha Unatumia Haki yako ya Msingi katika kupiga kura(kuchagua Kiongozi Bora na Siyo Bora Kiongozi).Baadhi ya Wananchi wameanza kuweka midomoni mwao Kitu kinaitwa Mapigano(Vita), lakini Kampuni hii ya Miss Demokrasia Tanzania inakuhakikishia kwamba Usiwe na wasiwasi kwa maana hakuna jambo lolote baya litakalojitokeza kwa kuwa watanzania tayari Wamefunguka na wanaendelea kupanuka kifikra na kimawazo, ni wapumbavu wachache sana yaani kikundi cha watu wachache sana ni sawa na asilimia 5 katika 100 wanaowaza na kufikilia Mapambano, Mapigano,na Vita.Zingatia kutoshirikiana na kukubaliana na mawazo ya mtu mpumbavu, mshawishi, mlaghai,Mwivi,Wauaji,usikubali kutoa ama kupokea Rushwa, wakati sasa umefika wa kutambua umuhimu wa haki, uhuru, na kutambua kwamba je ni kwa nini viongozi wanawajibika kwetu kama watumishi? kutambua wajibu wa Viongozi kwa jamii na wajibu wa jamii kwa viongozi,na baada ya kutafakari hayo kumbe je ni kweli kwamba Jamii ndiyo Mwajiri wa Kiongozi wake, je Bosi ni nani kati ya Jamii yaani wewe na Serikali?. je nani anapaswa kumtumia mwenzake? je ukiwa na watoto wagomvi, wezi, wasema uongo, wasiyotii maagizo yako ndani ya nyumba yako  ama ofisini mwako,  nini matarajio yake ya baadae?.www.missdemokrasia.blogspot.com  
Dk Slaa alisema kitendo kilichofanywa na Sugu pamoja na wabunge wengine ni cha kijasiri na aliwataka kutokurudi nyuma na misimamo yao  bali waendelee kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment