TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, September 21, 2013

MISS TANZANIA KUPATA MWAKILISHI WA DUNIA LEO

Mashindano ya 20 ya kumsaka mrembo bora wa Tanzania maarufu kwa jina la Miss Tanzania inafanyika leo jijini Dar es Salaam ikishirikisha warembo 30. Miss Tanzania, mashindano yaliyoanza mwaka 1994 ndiyo mashindano makubwa zaidi nchini ya urembo yanayoanzia ngazi za chini hadi yanafikia ngazi ya taifa ambayo yanafanyika leo.
Pamoja na miaka mingi ya kufanyika kwa mashindano hayo bado Tanzania imekuwa haifanyi vizuri katika mashindano ya kumtafuta mrembo bora wa dunia, Miss World. Ni mwaka 2005 tu ndiyo bendera ya Tanzania ilipeperushwa vyema katika mashindano ya Miss World kwa Nancy Sumari kufanya vyema na kuwa mrembo bora wa Bara la Afrika.
Kwa hiyo, wakati mashindano hayo yakifikia kilele leo tunaamini kwamba ni wajibu wa majaji wa mashindano hayo kufanya kazi yao kwa weledi ili kuipatia Tanzania mrembp bora. Ni vyema mrembo atakeyachaguliwa kuvaa taji la Miss Tanzania awe ana sifa za kutosha na vigezo vikubwa zaidi kuliko washiriki wengine kiasi kwamba akichaguliwa hakuna mtu
atakayethubutu kulalamika. Tungependa apatikane mshindi ambaye atakuwa na uwezo wa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia na kuing’arisha nchi katika mashindano hayo. Kufanya vizuri kwa mrembo wetu katika mashindano hayo ya dunia kutasaidia kuitangaza nchi yetu duniani jambo ambalo linaweza kusaidia katika kukuza utalii na kuimarisha uchumi wetu. 
Kwa utaratibu wa sasa mrembo atakayetwaa taji la Miss Tanzania leo atakuwa na kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss World. Kipindi hicho ni kikubwa ikiwa waandaji wa mashindano ya Miss Tanzania kama watataka kukitumia vyema kwa kumwuandaa mrembo huyo kabla ya kwenda kwenye mashindano ya Miss World.
Ikiwa waandaaji na wadhamini wa mashindano hayo watakuwa makini wana muda wa kutosha wa kumwuongezea ujuzi na uwezo Miss Tanzania kabla ya kupanda jukwaani katika mashindano ya dunia. Tunashauri ili kumjengea uzoefu Miss Tanzania apelekwe kwenye mashindano ya mwaka huu ya Miss World ambayo Tanzania itawakilishwa na Brigitte Alfred aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka jana.
Mbali na kupenda kuona Miss Tanzania akifanya vizuri katika anga ya kimataifa tunashauri washiriki wote wa mashindano hayo wawe mfano mzuri katika jamii kwa kuishi maisha yenye weledi. Wasichana waliopata nafasi ya kushiriki Miss Tanzania walkionyesha nidhamu ya hali ya juu katika maisha ya kila siku kutatoa fursa kwa wazazi kutokuwa na wasiwasi kwa watoto wapo kushiriki katika mashindano hayo.
Ni wajibu kwa waandaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Lino International Agency kuhakikisha kwamba inawajenga wasichana wanaoshiriki katika mashindano yao kwa kuwapa mbinu za kupambana na maisha ya kila siku. Kwa kufanya hivyo mashindano hayo yatakuwa na faida ya ziada na itakuwa inatoa mfano kwa waliopata nafasi ya kushiriki kwa kuwa raia wema.

No comments:

Post a Comment