TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 19, 2014

ENDABASHI WAFURAHIA UANZISHWAJI WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO

GEDSC DIGITAL CAMERA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akitoa elimu ya Ulinzi Shirikishi kwa viongozi na wananchi wa Tarafa ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)GEDSC DIGITAL CAMERADiwani wa kata ya Buger Bw. Emmanuel Tlaqho akitoa shukrani zake kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Liberatus Sabas mara baada ya kueleza uanzishaji wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto katika eneo hilo. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)GEDSC DIGITAL CAMERAKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Endabashi mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa wakazi hao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wananchi wa Tarafa ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu wamefurahishwa na utaratibu mpya wa jeshi la Polisi wa kupeleka askari 15 kila Tarafa kwa lengo la kuimarisha ulinzi katika maeneo yao. Akimshukuru Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, kwa niaba ya wananchi hao Diwani wa kata ya Buger Bw. Emmanuel Tlaqho, alisema kwamba mbali na mpango huo pia wamepokea kwa mikono miwili uanzishaji wa Dawati la Jinsia na Watoto.
Bw. Tlaqho alisema kwamba Dawati hilo litasadia katika mambo mengi ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro ya ndoa na utelekezwaji wa familia. Alisema pamoja na kuwepo kwa Dawati hilo pia viongozi wa mtaa wa maeneo hayo wanatakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwaasa  wanandoa ili waishi kwa amani ndani ya familia zao pia kutotumikisha watoto pamoja na kutowanyanyasa.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akizungumza na viongozi na wananchi wa maeneo ya Tarafa hiyo ambayo ina jumla ya vijiji 16 na wakazi wapatao 68,339, alisema kwamba mpango huo wa kupeleka askari 15 kila Tarafa una nia ya kuliweka Jeshi la Polisi karibu na wananchi ili waweze kushirikiana katika utatuzi wa matatizo ya kiulinzi na kiusalama kabla hayajafika kwa Mkuu wa Polisi wa wilaya.
Kamanda Sabas aliongeza kwa kusema kwamba, mbali na askari hao kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo pia watakuwa wanatoa elimu ya Polisi Jamii kwa askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi ili wajue namna ya utendaji wa kazi za ulinzi ikiwa ni pamoja na ukamataji salama na pia kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ili waweze kujua haki zao na wajibu wao katika suala zima la ulinzi.
Kamanda Sabas aliwasisitizia wakazi wa Tarafa hiyo wawe wanatumia mbinu za Ulinzi Jirani katika nyumba zao. Alisema suala la ulinzi ni la kila mmoja na haliihitaji kusubiri kudra ya M/mungu kwani uwezo wa kuzuia uhalifu upo ndani yao.
Akimalizia kutoa elimu hiyo kwa wakazi hao, Kamanda Sabas aliwaambia katika suala la ulinzi itikadi za kisiasa na udini hazina nafasi kwani mhalifu anapovamia eneo lolote hamuulizi mtu kwamba ni wa Chama gani au Dini gani bali yeye anatekeleza kile alichokikusudia.
Kwa upande wake mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la John Bula alisema kwamba, inaonyesha dhahiri kwa sasa jeshi la Polisi limeamua kushirikiana na wananchi kwani katika maisha yake hayawahi kuongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ana kwa ana mbali ya kumuona kwenye runinga au akiwa katika msafara wa Viongozi wa kitaifa lakini kupitia kikao hicho ameweza kuongea naye.
Bw. Bula alisema kutokana na hamasa iliyotolewa na Kamanda Sabas yeye kwa kushirikiana na wananchi wenzake watakuwa bega kwa bega na askari hao waliopo tarafani hapo ambao wanaongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robert Majenga.
Mpaka hivi sasa katika Mkoa wa Arusha tayari Kamanda Sabas amekwisha toa elimu juu ya ulinzi shirikishi kwa wananchi  wa Tarafa mbalimbali za wilaya nne huku bado akisubiri kumalizia wilaya mbili ambazo ni Ngorongoro na Longido.

No comments:

Post a Comment