TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 20, 2014

MSAMA YAWEKA BAYANA TARATIBU ZA UPIGAJI KURA WA TAMASHA LA PASAKA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO YA BUNGE LA KATIBA DODOMA

PG4A0417Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba , Saidi Mohamed Mtunda (katikati) na Subira Mgalu kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma  Februari 19,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A0435Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wajumbe wa  Bunge Maalum la Katika kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 19, 2014. Kutoka kushoto ni Dominick Lyamchay, Rashid Mtuta, Consitantine Akitanda na  Fahmi Fovutwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na Edina Kahurananga (DSJ)
KAMPUNI ya msama promotions hivi karibuni ilitangaza zoezi la upigaji kura kuchagua  taratibu za ufanyikaji wa Tamasha la Pasaka la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era zoezi la upigaji kura litahusika kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo.
Mang’era alisema mwaka huu wametoa nafasi hiyo ili kuwapa nafasi mashabiki wa muziki wa Injili kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji watakaoshiriki katika tamasha hilo.  
Aidha Mang’era alifafanua kuwa ili kumchagua mgeni rasmi unaanza na neno Mgeni rasmi Pasaka  unaacha nafasi kisha jina la mgeni rasmi kwenda 15327.
Mang’era alisema kumchagua mwimbaji katika tamasha hilo ni kuandika neno Mwimbaji Pasaka  unaacha nafasi jina la mwimbaji kwenda namba 15327 sambamba na kuchagua mkoa, unaandika neno Mkoa Pasaka  unaacha nafasi kwenda namba 15327.
Makamu huyo Mwenyekiti  alitoa wito kwa Watanzania kupiga kura kuchagua nafasi hizo tatu ili kufanikisha tamasha hilo.
Mwisho
Msama promotions kutumia vyombo vipya tamasha la Pasaka
Na Samia  Mussa
WAKATI maandalizi ya Tamasha la Pasaka yakipamba moto, Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo iko mbioni kununua vyombo vya muziki vitakavyotumika katika tamasha hilo.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Abihudi Mang’era, hatua hiyo imekuja mara baada ya kampuni hiyo kupata ushauri kutoka katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuishauri Msama kumiliki vyombo vyake vya muziki vitakavyotumika katika matamasha yake kwa nia ya kuboresha zaidi.
Mang’era alisema kuwa licha ya Basata kutoa ushauri huo kampuni hiyo ilianza harakati hizo mapema, ambapo inatarajia kununua vyombo hivyo katika nchi za Marekani na Canada.
Aidha Mang’era alisema kuwa, lengo ni kuboresha tamasha katika safu ya uimbaji amabyo ndio muhimu hivyo wanatakakuepukana usumbufu unaojitokeza katika vyombo.
“Lengo ni kuondoa dosari za vyombo, lakini pia nia yetu ni kuwashawishi waimbaji kuimba kwa kutumia vyombo sio CD tena kama ilivyozoeleka tunaamini kupitia matamasha tutafanikiwa kwa hilo waimbaji watazoea kuimba kwa vyombo tutakuwa tumepiga hatua kubwa,” alisema Mang’era.
Mang’era alisema kuwa hayo ni baadhi ya maboresho ya tamasha hilo ambalo mwaka huu linatarajia kufanyika katika mikoa nane hapa nchini.
Aidha Mang’era alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia watanzania na wadau wa tamasha hilo kuwa tamasha la mwaka huu ni la kimataifa kwa kuwa kamati imefanya marekebisho ya dosari zilizojitokeza katika tamasha lililopita.
Mwisho
makala
Uhondo wa Tamasha la Pasaka na faida 10
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions ambao  hivi sasa ipo katika harakati za maandalizi ya Tamasha la Pasaka ‘Tamasha,  lenye historia inayoanzia mwaka 2000, likibeba malengo 10, kubwa ni kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kupitia nyimbo za Injili kupitia waimbaji mbalimbali wa Kimataifa kwa watu wote.
Tamasha hili  ni la aina yake huisindikiza Pasaka ambayo ni kielelezo na alama ya ushindi wa Wakristo dhidi ya zambi kupitia kifo cha Yesu Kristo pale Msalabani, huwaleta pamoja watu bila kujali dini, itikadi na jinsia kufurahia ufufuko wa kristo kwa kusikiliza na kucheza nyimbo za injili. 
Katika mahojiano  maalum na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya jijini Dar es Salaam inayoratibu tamasha hilo na lile la Krismasi lililoanza mwaka jana, Alex Msama anasema manufaa ya matukio hayo mawili ya kimataifa, yamezidi kuongezeka kulingana na haja ya wakati na mazingira halisi kulingana na changamoto zinazojitokeza.
Msama anasema Tamasha la Pasaka la mwaka huu ni la kisasa zaidi ya miaka iliyopita kwa sababu la mwaka huu ni la mashabiki zaidi, watapiga kura kuchagua mikoa, waimbaji na mgeni rasmi.  
Anasema sambamba na hayo, Msama anasema utaratibu huo wa kuwashirikisha mashabiki utaliboresha zaidi tamasha hilo ambalo kadri miaka inavyokwenda linazidi kupiga hatua zaidi. 
Achilia mbali hilo, Tamasha la Pasaka lina malengo 10 ambayo ni maeneo ambayo yanaisaidia jamii kulifikia neno la Mungu kupitia waimbaji:-

No comments:

Post a Comment