TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 19, 2014

KISARAWE KUKUTANISHA MIAMBA WA NGUMI APRIL 26 MWAKA HUU

Bondia Mbaruku Heri kushoto akimvisha gloves Mwenyekiti wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng’imba wengine kulia ni Masudi Bakari na Said Chaku .
……………………………………………………………………….Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI  wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng’imba amepokea maombi ya kuhamasishwa mchezo wa masumbwi katika halmashahuri hiyo baada ya mchezo huo kurudi tena  kwa kipindi hiki


Maombi hayo yaliyopelekwa na kamati ya kufufua mchezo wa masumbwi Kisarawe ikiongozwa na Bondia Mbaruku heri, Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila ‘SuperD‘ pamoja na wadau wengine wa masumbwi nchini Saidi Chaku na Masudi Bakari ambao wamepeleka barua hiyo kwa ajili ya kuanzisha  hamasa ya mchezo huo tena huko Karawe
akizungumza mara baada ya kusoma maombi yaliyopo katika barua hiyo alijibu kwa kusema nimepokea kwa moyo mmoja maombi haya na ngumi zitapigwa kama zamani nakumbuka mabondia wengi akiwemo Habibu Kinyogoli ‘Masta’ ametokea hukuhuku Kisarawe na mkumbuke kuwa bondia wa ngumi za ridhaa anaetamba kwa sasa na aliyetuwakilisha katika mashindano ya Olimpic yaliyomalizika hivi karibuni Selemani Kidunda naye anatoka hapa hapa katika wilaya ya Kisarawe hivyo tunaweza  kuhakikisha ngumi zinarudia enzi zake
Ninawaahidi ngumi hizi zitapigwa katika viwanja vya wazi ili kila mtu ashuhudie mchezo wa ngumi unavyorudi upya katika wilaya hii naomba wapenzi mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakae mkao wa kula siku ya April 26 ngumi zitapigwa katika uwanja wa Bomani ili kila mtu ajionee mwenyewe
aliongeza kwa kusema ataendelea kutafuta wafadhili ili walete hamasa ya mchezo wa ngumi katika wilaya hiyo ambayo imejinyakulia umaarufu mkubwa mpaka sasa kupitia mchezo wa ngumi, Nita akikisha tunanunua vifaa vya mchezo ili vijana wapate kuendelea kushiriki mazoezi na hatimae waje kurudia enzi za Kinyogoli
Nae mkuu wa msafara wa kuhamasisha mchezo wa ngumi katika wilaya  hiyo, Mbaruku Heri amesema atakikisha siku hiyo analeta vijana wengi wakali wanaotamba katika ulimwengu wa masumbwi kwa sasa kama vile Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’,Hamza Mchanjo,Thobias Adaut, Husein Pendeza,Said Uwezo,Adamu Ngange,Ambokile Chusa,George Dimoso,Twalibu Mchanjo na wengine wengi wanaofanya vizuri katika ulimwengu wa masumbwi kwa sasa

No comments:

Post a Comment