TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 20, 2014

WAZAZI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUWAFICHA WATOTO WENYE ULEMAVU

indexBAADHI ya wazazi nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kinyume cha haki za binadamu. Akizungumza kwa njia ya simu na Fullshangwe, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Kibaha, Pwani, Regina Mbaji alisema wandishi wanapaswa kufanya kazi ya ziada katika kuwaibua watoto wa aina hiyo popote walikofichwa. Alisema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto hao kutokana na mtazamo hasi, wakizani kuwa na mtoto kama huyo katika familia kuwa ni aibu na kioja wakati sio kweli.
Mbaji alisema jamii inapaswa kutambua kuwa watoto wenye ulemavu ni binadamu kama wengine na wanahaki sawa na wengine. “Kuna baadhi ya familia ambazo zimekuwa zikiwanyanyapaa watoto au watu wenye ulemavu kwa kuwalaza wakati mwingine kwenye vyumba vya mifugo kwa kweli huu ni unyama uliyopitiliza naviomba vyombo vya habari kwenda mbali katika majukumu yao kwa kuibua unyama huu hususan maeneo ya vijijini,”alisema Mbaji.
Mbaji alisema maeneo ya vijijini bado wazazi wanaendelea kuwakosesha mahitaji ya msingi watoto hao, ikiwemo elimu, wakidhani kuwa hawana uwezo wa kuelewa masuala mbalimbali watakayofundishwa. Alitoa wito kwa jamii kuwafichua watoto hao popote walipofichwa ili serikali iweze kuwapatia mahitaji yao kama wanayoyapata watu wengine wenye viungo kamili.

No comments:

Post a Comment