TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 20, 2014

MAMA BILALI: WANAWAKE TUJIWEKEE AKIBA

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha.DSC01538Bila kusahau burudani kutoka THT, ambao waliigiza mahudhui ya Tamasha.DSC01581Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali akisoma hotuba yake wakati akifungua Tamasha hilo la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana.DSC01593Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akitoa ushuhuda wake juu ya kutumia fursa katika ujasiriamali. Mama Tunu alishiriki katika Tamasha hilo akiwa mjasiriamali aliyekuwa akiuza mazao yatokanayo na nyuki.DSC01606Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.DSC01614Kulikuwa na utaoji wa tuzo kwa washiriki katika Tamasha hilo. Bila kusahau burudani kutoka THT, ambao waliigiza mahudhui ya Tamasha.DSC01640Wake wa Viongozi (New Millenium Women Group) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.DSC01691Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimuonesha bidhaa zilizomo bandani kwake alipotembelewa na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Wanawake nchini wameaswa kujenga tabia ya kutunza akiba ili kufikia malengo wanayojiwekea na kwa maendeleo ya familia zao.
Wito huo umetolewa na Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali wakati akifungua Tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalofanyika kwa muda wa siku tatu jijini, Dar es Salaam.
Mama Asha alisema kuletwa kwa Tamasha hilo ni fursa mojawapo na adimu sana kwa wanawake kujipatia utaalamu na kupanua wigo wao kibiashara. 
Alisema kuwa maendeleo ya Tanzania yanaanza kwa kina mama kwa wao wenyewe kujijengea tabia ya kujiwekea akiba japo kidogo ni kwani ni furaha na mkombozi wa siku za baadae. 
“Akiba ni msingi wa maendeleo ya kila mwananchi. Kwa kila biashara, na kila ajira tuliyonayo, bila kuwa na elimu na utaratibu wa kujiwekea akiba tutazidi kuwa na kipato kidogo hivyo kushindwa kuendelea kiuchumi na kijamii,” aliasa Mama Asha.
“Nachukua nafasi hii pia kuwaomba wanawake wote watakaohudhuria kutilia maanani mafunzo yote watakaopewa katika siku mbili zijazo ili kuweza kujenga uwezo wao katika uwekaji wa akiba,” aliongeza. 
Mama Asha aliipongeza kampuni ya Angels Moment pamoja na timu yake kwa kuwaza kuandaa tamasha hilo la elimu kwa akina mama hususani walio katika sekta isiyo rasmi kwani linatoa fursa ya kuwatoa wanawake katika utegemezi na umaskini kwa kuongeza kipato chao.
Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima alisema lengo kuu la Tamasha hilo ni Kuboresha kasumba ya kujiwekea akiba, hususan ikwa akina mama, na mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato miongoni mwao.
“Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Naima. 
Aliongeza kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha. 
“Tamasha linatoa fursa za maonyesho na semina ambazo zitawaelimisha wanawake namna tofauti za kuweka akiba, na mbinu mbalimbali za kujikimu,” alisema Bi Naima.
Aliongeza kuwa Tamasha hili pia linakusudia kuwaelimisha wanawake umuhimu wa kuweka akiba, mbinu tofauti za kuweka akiba na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kujiwekea akiba.
Tamasha hilo linalofanyika katika Ukumbi wa  Dar Live – Mbagala, jijini Dar es Salaam limehudhuriwa na mamia ya kina mama na vijana ikiwemo wake wa viongozi waliongozwa na Mama Tunu Pinda ambaye ameshiriki kama mjasiriamali wa kuuza mazao ya nyuki.

No comments:

Post a Comment