TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 19, 2014

NMB KWA KUSHIRIKIANA NA TIGO PESA YASOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI KARIBU ZAIDI NA WATEJA WAKE

       Yote hii ni kupitia simu ya mkononi na hela kuchukuliwa kupitia Wakala yeyote wa Tigo Pesa
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi Tigo wamezindua huduma ya kuweka na kutuma pesa kupitia simu za mkononi. Lengo kubwa la huduma hii  ni kuwezesha huduma za kibenki kuwafikia wateja kwa ukaribu na urahisi zaidi.
Huduma hii mpya inawawezesha wateja  wote wa NMB na Tigo kuweka  na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Tigo Pesa  kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Vilevile, mteja anaweza kuweka na kuhamisha  pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Tigo Pesa.  Huduma hii inafanyika kwenye  simu za mkononi na utoaji wa fedha unafanyika kwa Wakala yeyote wa Tigo Pesa.  
1Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa kitengo cha Athari  wa NMB,  Tom Borghols (kati) na Mkuu wa kitengo cha huduma ya Tigo Pesa, Ruan Swanepoel wa kwanza (kulia) wakiweka sahihi mkataba wa kutoa huduma za NMB kwa kupitia Tigo Pesa . Huduma ambayo inamwezesha mteja wa NMB mobile kutuma fedha kwenda Tigo Pesa na mteja wa Tigo Pesa kuweka fedha  kwenye akaunti ya NMB. Kushoto akishuhudia ni Mkuu wa kitengo cha Huduma Binafsi wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela.DSC_3690Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa kitengo cha Athari  wa NMB,  Tom Borghols (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha huduma ya Tigo pesa,  Ruan Swanepoel wakibadilishana mkataba wa ushirikiano utakao muwezesha mteja wa NMB mobile kuweka na kuchukua pesa zake mahali popote kupitia mawakala wa Tigo Pesa nchini na mteja wa Tigo Pesa kuweka  fedha  kwenye akaunti ya NMB.

No comments:

Post a Comment