TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 20, 2014

KITUO CHA DALADALA SIMU 2000 KITAANZA KAZI HIVI KARIBUNI

indexMEYA wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda, amesema Kituo cha Daladala Simu 2000 kinatarajia kuanza kazi hivi karibuni baada ya kukamilika hatua za mwisho za ujenzi.
 
Akizungumza  jijini Dar es Salaam , Mwenda, alisema Kituo hicho kinajengwa kwa ajili ya kuhamishwa kituo kidogo cha daladala Ubungo ambacho kimeathiriwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka (BRT).
 
Alisema kuanza kazi kwa kituo hicho kunatokana na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la choo na Kituo cha Polisi na sehemu nyingine muhimu.
 
“Kwa wastani kazi ya ujenzi ya kituo hicho inaendelea vizuri na ni vema nanyi wandishi mkatembelea pale ili mkajionee wenyewe baadala ya kungoja kusimuliwa,”alisema Mwenda.
 
Alisema hivi sasa mkandarasi anakamilisha ujenzi wa barabara pamoja na upangwaji wa maeneo maalumu ya wafanyabiashara katika kituo hicho.
 
Mwenda, alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha simu 2000 kutasaidi kumaliza manung’uniko ya baadhi watumiaji wa barabara ya Morogoro kuwa uwepo wa kituo hicho hvi sasa umekuwa ukiachangia msongamano wa magari katika eneo hilo.
 
“Kila kitu kimekamilika hivyo wakati wowote kwenye mwezi Machi mwaka huu kituo kile kitaanza kazi ujenzi unaendelea kwa kasi,”alisema Mwenda.
 
Awali watumiaji wa barabara hiyo walisema pamoja na foleni zinazosababishwa na ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka bado kuchelewa kuhamishwa kituo hicho kimekuwa kikichangia msongamano hususan pale daladala zinapoingia na kutoka kwenye kituo hicho.
 
Novemba mwaka jana Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini alifanya ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo hicho ambako alihakikishiwa na uongozi wa wilaya hiyo kuwa kingeanza kazi mwezi Desemba.

No comments:

Post a Comment