TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 6, 2012

Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amnadi Mohamedraza Hassanal Dharamsi mgombea wa CCM Uzini Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinajiendesha kwa kuheshimu maoni, maamuzi na ushauri unaotolewa na wananchama wake katika ngazi mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati akimnadi mgombea wa CCM Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassanal Dharamsi katika shehia ya Mchangani Mkoa Kusini Unguja.
Profesa Mbarawa amesema Kamati Kuu ya Taifa ya CCM hufanya uchambuzi, kupima mambo kwa vigezo husika hatimaye huzingatia maamuzi na ushauri wa wananchama wake.
Amesema CCM si chama kinachochakachua, kubadili au kupuuzia maoni na maamuzi ya wanachama wake kwa kufanya upendeleo.
Ameeleza kuwa CCM ni taasisi ya kisiasa yenye uzoefu mkubwa Barani Afrika, viongozi wake ni mahiri, wajuzi na wenye uwezo wa kupima mwenendo ulivyo.
Aidha Mjumbe huyo Kamati Kuu ya CCM amesisitiza kuwa CCM huongozwa na mwelekeo wa Katiba na Kanuni zake bila ya kufanya ubaguzi, upendeleo na maonevu.
Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea wa Uzini, Profesa Mbarawa amesema Kamati Kuu ya CCM imefanya tafakuri pana, uchambuzi wa kutosha na kukusanya vielelezo vilivyomthibitisha kuwa Raza anatosha kuwa mgombea.
Amewataka wananchi wa Uzini kujipanga na kuhakikisha Mgombea huyo wa CCM anashinda katika uchaguzi wa Februari 12 mwaka huu, ili ashirikiane na wananchi wenzake kuleta maendeleo.

SERIKALI YAOMBWA KUENDELEA KUBORESHA MAKAZI YA POLISI

Na Ashura Mohamed - Arusha
Serikali kupitia Wizara ya ulinzi na usalama imeombwa kuendelea kuwaboreshea makazi askari polisi ili waweze kuishi katika mazingira mazuri na kuongeza ufanisi katika kazi.
Akizungumza katika sherehe za kukaribisha mwaka mpya 2012 zilizoandaliwa na jeshi la polisi mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni hakimu mkazi mkoani arusha Charles Magesa amesema kuwa ili kuongeza ufanisi katika kazi pia ni vyema polisi nao wakaboreshewa makazi yao.
Magesa ameongeza kuwa taasisi yeyote inayofanya kazi ya kuihudumia jamii ni lazima changamoto zake zishughulikiwe hivyo amewataka polisi kufanya kazi kwa uwazi na umakini zaidi ili jamii inayoizunguka iweze kuwa na imani nao.
Aidha amesema kuwa jamii ni lazima iweze kulisaidia jeshi la polisi katika kuhakikisha kuwa linatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwapa ushirikiano zaidi ili kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andeng’enye amesema kuwa vitendo vya uhalifu katika mkoa wa Arusha vimepungua ukilinganisha na mwaka 2010.
Andeng’enye amesema kuwa jumla ya matukio 25,833 yaliripotiwa mwaka 2011 ikilinganishwa na matukio 26,698 yaliyoripotiwa kwa mwaka 2010 ambapo ni pungufu ya matukio 865.
Amefafanua kuwa matukio hayo yamegawanyika katika makundi manne ni makosa dhidi ya binadamu,makosa dhidi ya mali,makosa dhidi ya maadili ya Jamii na makosa ya usalama barabarani ambapo ni pamoja na mauji,kubaka,kulawiti.wizi wa watoto,kutupa watoto,unyang’anyi wa kutumia silaha,unyang’anyi wa kutumia nguvu,wizi wa magari,wizi wa mifugo,ajali za moto na makosa ya usalama barabarani.
Hata hivyo kamanda Andengenye ametaja changamoto wanazokabiliana nazo kwa mwaka 2012 ni pamoja na Tatizo la ajira kwa vijana ni changamoto nyingine inayosababisha kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu kutokana na vijana hao kutokuwa na namna ya kutafuta kipato hivyo inakuwa rahisi kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

WAKOREA KUSINI KUSAIDIA KISIMA KATA YA NABERERO SIMANJIRO, KISIMA KUGHARIMU DOLA 6500

Picha ikionyesha moja ya mitambo ya kuchimbia visima.
Na Ashura Mohamed – Simanjiro
Jumuiya ya wananchi wa Korea Kusini wamechimba kisima cha maji katika kata ya Naberero wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambacho kimegharimu dola za kimarekani 6500.
Akizungumza wakati wa kuzindua kisima hicho mchungaji wa kanisa la Juan Jung Ang lililopo Korea Kusini Park Eung Soon, amesema kuwa maji ni muhimu hivyo wameona ni vyema kuwasaidia wakazi wa maeneo hayo kwa kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Park Soon amesema ikiwa kama wananchi wa Tanzania watakuwa na moyo wa kujitolea kama ilivyo kwa wananchi wa Korea Kusini basi ni wazi wataweza kubadili nchi kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwa miaka 50 iliyopita hali ya kiuchumi katika nchi hiyo ilikuwa ni mbaya sana kuliko Tanzania lakini wananchi waliweza kujengewa imani kuwa wananafasi kubwa ya kuibadili nchi yao na wakafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
“Wananchi waliojitolea msaada huo sio kama ni matajiri bali ni ile hali ya kujitoa na uaminifu juu ya wengine ndio kinachowasaidia” alisema Park Soon.
Naye Askofu Erick Mkwenda wa Kanisa la kikristo la Marannatha ambaye ni mwenyeji wa ugeni huo amesema ni jambo la neema kwa kuwa kisima hicho kitaweza kuwasaidi wakazi wa kata hiyo kutokana na wilaya hiyo kuwa na tatizo la maji.

MWANAMILAMBO BENDI YAFUNIKA COCO BEACH- WAKATI WA KUPIGA PICHA ZA UJUMBE WA ALBAMU YAO ILIYODHAMINIWA NA UBALOZI WA MAREKANI.

Kiongozi wa Kundi la Mwanamilambo Bendi,  Mango  Star(kati), akionyesha Umaili wake katika kucheza na Nyoka wakati wa zoezi la Kupiga Picha za Mabango yanayobeba Ujumbe wa Albamu yao iliyodhamini wa na Ubalozi wa Marekani jana.
Wasanii wa Mwana-Milambo Bendi, wakionyesha Mabango yanayobeba Ujumbe wa Albamu yao Mpya iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Marekani, wakati wa upigaji picha katika Ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana.
Msanii wa Kundi la Mwanamilambo Bendi, Mango Star, akiwa na Mtoto wakati wa kupiga picha za Mabango yanayobeba Ujumbe wa Albamu yao iliyodhamini wa na Ubalozi wa Marekani jana.
Wasanii wa Mwana-Milambo Bendi, wakionyesha staili ya Sarakazi, wakati wa kupiga picha za Mabango yanayobeba Ujumbe wa Albamu yao Mpya iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Marekani, wakati wa upigaji picha katika Ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana.

KITUO CHA UTAMADUNI CHA IRAN CHAFANYA MAADHIMISHO YA MAPINDUZI YA KIISLAMU NCHINI IRAN

Mkurugenzi mtendaji kituo cha utamaduni wa jamhuri ya kiislam Bw. Mortazar Sabour akiongea na waandishi wa habari kwenye maadhimisho miaka 33 ya mapinduzi ya kiislam ya yaliyotokea mwaka 1979 chini ya utawala wa Imamu Ayatolla Khomein yaliofanyika juzi katika kituo cha utamaduni cha Iran jijini Dar es salaam.
w Mortazar Sabour akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya waumini wa kiisilam wakiangalia picha za kumbukumbu za mapinduzi ya Iran katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya waumini wa kiisilam wakiangalia picha za kumbukumbu za mapinduzi ya Iran katika maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa shule ya Darul Huda Islamic wakiimba wimbo wa Taifa kwenye maadhimisho hayo.

SBL KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA KIFEDHA

Afisa Masoko Mwandamizi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika mikoa ya Arusha na Manyara Joan Semuguruka akitoa salamu za kampuni hiyo kwa wafanyakazi wa benki mbalimbali (hawapo pichani) zilizoshiriki hafla ya 'Bankers Gala Night' iliyofanyika mkoani Arusha mwishoni mwa wiki.SBL kupitia bia yake ya Tusker Malt ilidhamini hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki tofauti nchini wakipatiwa utaratibu kabla ya kuingia katika hafla iliyowakutanisha pamoja wafanyakazi wa benki katika tukio lililojulikana kama 'Bankers Gala Night'.Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Tusker Malt.
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Tusker Malt imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano ndani ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kibenki katika lengo la kukuza maendeleo ya uchumi nchini.
Hii ilikuwa wakati wa hafla maalum ya wadau katika sekta ya kibenki iliyodhaminiwa na bia ya Tusker Malt na kuzileta pamoja taasisi za kifedha zikiwemo benki zinazoongoza kibiashara nchini.
Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha mwishoni mwa wiki ilitoa fursa maalum kwa wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kibenki kuzungumza pamoja changamoto mbalimbali zinazoikabiri sekta ya fedha nchini.
Akizungumza wakati wa halfa, Afisa wa kampuni ya Serengeti wa Nyanda za Juu Kaskazini, Bw. Mapendo, alisema kuwa kampuni yake itaendelea kufanya kazi karibu na wadau wote ili kuleta maendeleo ya uchumi nchini.
Alisema hafla hiyo imetoa nafasi kubwa kwa wadau wa taasisi za kifedha haswa za kibenki kuungana pamoja na kubadilishana mawazo jinsi gani wanaweza kusonga mbele na kupanua sekta hiyo muhimu katika uchumi wa taifa.
Mapendo alisema SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt imedhamini hafla hiyo na kwamba itaendelea kushirikiana na sekta hiyo katika mambo mbalimbali kulingana na uwezo wake kifedha.
“Sekta ya kibenki inakuwa kwa kasi sana na hivyo kutoa fursa nyingi mbalimbali kwa nyanja zote mbili za kibiashara pamoja na ajira kwa watanzania walio wengi. Na fursa hizo huonekana zaidi wakati wa matukio muhimu kama haya.
"Tunaamini kwamba kupitia hafla hii, jamii ya wafanyabiashara itachukua na kuzifanyia kazi fursa zilizopatikana. Tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa tukio hili.
“Bia ya Tusker Malt imekuwa ikidhamini matukio mbalimbali nchini lakini mwaka huu tumedhamiria kuweka mkakati madhubuti ambao unaangalia zaidi biashara katika makampuni na makundi mengine ndani ya jamii,” aliongeza.
Kwa upande wake mwakilishi wa waandaaji wa tukio hilo Peter Morgan aliishukuru Tusker Malt kwa udhamini wake na kusema kuwa ni vyema SBL ikaendeleza wazo hilo zuri la kuwa na matukio kama hayo katika kanda mbalimbali nchini.
“Hili ni tukio la kukumbukwa ndani ya jamii ya wadau wa taasisi za kibenki. Tumeweza kuzikutanisha taasisi mbalimbali za kifedha pamoja si kukutana tu bali pia kuweza kubadilishana mawazo jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabiri sekta ya kibenki. Tunaishukuru bia ya Tusker Malt kwa udhamini wake,” alisema.

Rais Jakaya Kikwete akutana na meya wa jiji la Wurzburg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumapili, Februari 5, 2012, alikutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Mji wa Wurzburg wa Ujerumani, Mh.George Rosenthal.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye Ikulu Ndogo mjini Mwanza, Meya Rosenthal ameambatana na madiwani wanne, mkewe, Hanna Rosenthal na binti yake, Lisa Rosenthal.
Ujumbe huo wa mji wa Wurzburg unatembelea Jiji la Mwanza kwa muda wa wiki moja ikiwa ni ziara ya kirafiki kati ya miji hiyo miwili uhusiano wa kindugu.
Mji wa Wurzburg ulianzishwa miaka 1,300 iliyopita, una vyuo vikuu vitatu na wanafunzi kiasi cha 30,000 wanaosoma katika vyuo hivyo.
Mji wa Wurzburg unalisaidia Jiji la Mwanza katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na utunzaji mazingira, afya, nishati. Pia miji hiyo miwili ina program ya kubadilishana wanafunzi kwa maana ya wanafunzi wa miji hiyo miwili kutembeleana na pia Jiji la Wurzburg linaisaidia taasisi za kijamii za Jiji la Mwanza.
Rais Kikwete amemwambia Meya Rosenthal kuwa Tanzania na Ujerumani zina uhusiano mzuri na wa karibu na Serikali yake imedhamiria kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano huo.
Rais pia amesifu uhusiano huo wa kindugu kati ya miji ya Mwanza na Wurzburg na ametaka miji hiyo kuimarisha uhusiano huo kwa sababu ni muhimu na unanufaisha pande zote mbili. Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu mkoani Mwanza.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA KITABU CHA PIUS MSEKWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Februari 5, 2012, amezindua Kitabu kiitwacho Uongozi na Utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika halfa fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Ndogo Mjini Mwanza.
Kitabu hicho kilichoandikwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius Msekwa kinaelezea uzoefu wa miaka 25 ya Mzee Msekwa katika utumishi wa umma chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu K. Nyerere.
Sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho chenye kusara 156 zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwamo mawaziri, viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Katibu Mkuu Mheshimiwa Wilson Mukama na viongozi wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza kabla ya Mheshimiwa Rais Kikwete hajazindua kitabu hicho, Mzee Msekwa amesema kuwa moja ya mambo yaliyomchochea aandike kitabu hicho ni pamoja na changamoto aliyopata kuitoa Rais Kikwete kwa viongozi wastaafu wa umma kuchangia maendelea na historia ya Tanzania kwa kuandika vitabu kuelezea uzoefu wao katika utumishi wa umma.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho, Mheshimiwa Rais Kikwete amempogeza Mzee Msekwa kwa kuandika kitabu hicho na kuwataka wastaafu wengine wa utumishi wa umma kufuata mfano wa Mzee huyo kwa kuandika uzoefu wake katika kuwatumikia Watanzania.
Kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Msekwa ameshika nafasi nyingi za madaraka katika Serikali na siasa ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu wa Bunge, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa chama cha TANU, Mtendaji Mkuu wa CCM, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu mjini Mwanza ambako leo alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Sherehe za Miaka 35 ya CCM zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.

Balozi mpya wa Tanzania nchini Ubelgiji,Dk.Diodorus Kamala na Dk. Sezibera katibu mkuu wa (EAC) wakati wa kuagana

Balozi mpya wa Tanzania nchini Ubelgiji,Dk.Diodorus Kamala(kushoto)akiongea na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera alipoenda kumuaga,Dk Kamala alikuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera(kulia) akiagana na Balozi mpya wa Tanzania nchini Ubelgiji,Dk Diodorus Kamala(kushoto)aliyemtembelea ili kumuaga,Dk Kamala amewahi kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera(kushoto) akimsindikiza Balozi mpya wa Tanzania nchini Ubelgiji,Dk Diodorus Kamala(kulia)aliyemtembelea na kumuaga,Dk Kamala amewahi kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania.Picha Zote na Fibert Rweyemamu

Msama Promotions waomba kibali BASATA

NA MWANDISHI WETU KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, imeomba rasmi kibali cha kufanya tamasha la Pasaka mwaka 2012, litakalofanyika Aprili 8, mwaka huu katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza na Dira ya Mtanzania jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, alisema tayari wamepeleka maombi BASATA ili waweze kupata kibali cha kuendesha tamasha la mwaka huu.
“Tumepeleka maombi yetu ya kuandaa tamasha la Pasaka mwaka huu, tunategemea BASATA watatusikiliza na kutupatia kibali,” alisema.
Msama alisema tamasha la mwaka huu litapambwa na waimbaji wengi wa kimataifa, wakiwemo nyota wa muziki wa injili nchini.
Alisema katika tamasha hilo, kamati yake itakutana kupanga sehemu litakalopofanyika tamasha hilo kwa mwaka huu.
“Miaka yote tumezoea tamasha kufanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, lakini mwaka huu kazi ya kutafuta sehemu kubwa ya kuweza kushuhudiwa na waumini wengi wa dini ya kikristo, tumeiachia kamati, ikikamilisha tutatangaza,” alisema.
Pamoja na kusema kuwa, tamasha hilo litafanyika mikoa mbalimbali nchini, Msama alishindwa kuitaja na kusema kuwa, itatangazwa baada ya kamati yake kuichagua.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya maandalizi ya Pasaka, alisema kuwa, mgeni rasmi katika tamasha hilo atatangazwa hapo baadaye.
“Suala la mgeni rasmi naomba kwa sasa mliache, linafanyiwa kazi, mambo yakikamilika, tutamweka hadharani,” alisema.
Msama alisema kuwa, mwaka jana mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA CCM MWANZA YAFANA

Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wana CCM na wakaazi wa Mwanza leo katika kuadhimisha miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba (PICHA NA IKULU)
Wageni waalikwa mbalimbali kutoka nje ya nchi wamehudhuria katika maadhimisho hayo ya miaka 35 ta CCM mkoani Mwanza. (PICHA NA IKULU)
Mama Salma Kikwete na Spika Anne Makinda na wakinamama wakisherehekea miaka 35 ya CCM baada ya kukunwa na wimbo wa Vicky kamata. (PICHA NA IKULU)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akipokea salamu za heshima kutoka kwa gwaride la vijana wa CCM wakati wa sherehe hizo. Wengine kushoto ni Makamau Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia wananchi alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, jana
Maelfu ya watu waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza leo wakishangilia kwa furaha 
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Suma Lee akionyesha umahiri wake alipopanda jukwaani kutumbuiza wakati wa sherehe hizo. (Picha Zote na na Bashir Nkoromo)

WATAKAOPATA AJALI KULIPWA MILIONI MBILI

NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
Madereva mbalimbali hasa wa masafa marefu wanatarajia kunufaika na bima ya maisha kwa kupewa Kiasi cha Milioni Mbili kutoka katika Bima ya jubilee hali ambayo itawafanya madereva walio wengi kuweza kujikwamua katika suala zima la umaskini, ulemavu, vifo ambavyo vinasababishwa na ajali hizo.
hayo yamebainishwa na Meneja wa kanda ya kaskazini kutoka katika bima ya Jubilee(JUBILEE INSUARANCE} Bw Charles Magori wakati akiongea na vyombo vya habari jijini hapa mapema wiki hii.
Bw Magori alisema kuwa Bima ya maisha ambayo itaweza kuwafikia madereva wengi zaidi itakuwa na manufaa makubwa sana kwa kuwa baadhi ya madereva hasa wale wa masafa marefu wamekuwa katika maisha ya taabu mara ya kupata ajali.
Alibainisha kuwa mara baada ya kupata ajali asilimia kubwa ya madereva hao hushindwa kufikia malengo yao kwa kuwa tayari wanakuwa wameshapata vilema vya maisha,vifo ambapo hupelekea kukosa garama za mazishi hali ambayo ni hatari kwa maisha ya sasa.
“tulichoweza kugundua ni kwamba hawa madereva mara nyingi wanakuwa katika hatari mbaya sana ya ajali na hivyo hata kwa wale ambao wanakufa familia zao zinakuwa katika wakati mgumu sana huku nyingine nazo zikiwa hata kwenye hatari ya kukosa fedha kwa ajili ya mazishi lakini tunachoweza kukifanya hapa ni kuhakikisha kuwa tunasaidia jamii kwa kuwapa milioni mbili kwa ajili ya maandalizi mbalimbali'alisema Bw magori
Awali alisema kuwa mbali na kutoa bima hiyo hasa kwa madereva pia kwa sasa zoezi hilo la kutoa bima litaenda sanjari na elimu mbalimbali ambazo zinahusu uimu wa bima kwa maisha ya mtanzania kutokana na kuwepo kwa matukio mbalimbali ambayo yana historia ya kutokea sana kwa ndani ya jamii.
Bw. Magori alisema kuwa endapo kama madereva hao wataweza kupata elimu hiyo ya bima basi watanufaika kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo kwa sasa bado baadhi ya jamii hazina mwitikio wa masuala ya bima.
Pia aliwataka wananchi wote kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kutafuta elimu mbalimbali za bima kwa kuwa bima ni msingi wa maisha ya kila mtanzania hususani kwa sasa ambapo jamii nyingi kukosa elimu hali ambayo inachangia kuwepo fikra hasi juu ya uimu wa bima kwa maisha ya mtanzania wa sasa.

KANISA LA BABTIST TIMBOLO LAWAJENGEA WATOTO SHULE


NA GLADNESS MUSHI- ARUMERU
Kanisa la Baptist Timbolo lilopo sambasha wilayani arumeru limetoa msaada wa kujenga shule kwa ajili ya watoto yatima, wasiojiweza, pamoja na walemavu a mbapo shule hiyo itagarimu zaidi ya million 150 sanjari na kuanza kuwapa elimui ya sekondari bure mayatim a 30 mwaka huu.
Akiongea na Mwandish wetu mkurugenzi ambaye pia ni mchungaji wa kanisa hilo Bw Saitoti Mollel alisema kuwa lengo ni kuhakkisha kuwa motto wa kike anapata elimu ambayo ni bora zaidi
Alisema kuw a shule hiyo ya timbolo ambayo ni ya sekondari imelenga kuhakikisha kuwa inatoa kipaumble zaidi kwa motto wa kike ambaye amesaulika na jamii hasa za wakazi wa eneo hilo ambapo ni jami za kimasai, na waarusha
Alisema kuwa shule hiyo ambayo inanza rasmi kutoa elimu ya sekondari kwa mwaka huu itaanza na wanafunzi 90 kutoka katika jamii mbalimbali huku kati yao 30 wakiwa ni watoto mayatima ambaoi wataweza kusoma bure ikiwa ni mchango wao kwa kanisa dhidi ya watoto ambao ni mayatima
“Haya ni maono ya kanisa hili la Baptist Timbolo kwa kuwa hapa jirani hakuna shule ambayo inalenga katika kuhakikisha kuwa hawa watoto ambao wanaishi mazingira magumu, na mayatima wanapata elimu lakini sasa kupitia shule hii wataweza kupata haki zao za msingi ambapo ni elimu “alisema Mchungaji Saitoti
Pia aliongeza kuwa mbali na kuweza kuwajengea shule ambayo imegarimu zaidi ya million 150 pia wamefanikiw a kutoa elmu mbalimbali za uasiamli kwa wananchi wa maeneo yao pamoja na khakkisha kuwa wanawajenga kimwili wakristo wao
Alisema kuw a mpaka sasa tayari wameshahamasisha wakristo ndani ya kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanajiwekea uataribu maalumu wa [kufuga ambapo kanisa limetoa mbuzi wa kienyeji kama 40 kwa ajili ya vikundi hivyo
“Hawa mbuzi pia ni msada kw a wakristo0 wertu kwa kuwa tunaamini kuwa kupitia mbuzi hawa ambao tumewapa bure tutaweza kuwatoa katika suala zima la umaskini na hivyo wataweza kujikita katika suala zima a ufugaji na kuachana na tabia ya kukaa bure”alisema Mchungaji Saitoti
Hataivyo alisema kuwa ni vema kama makanisa ya leo yatahakikisha kuw a yanatoa msaada hata kwa wakazi wa maeneo ya jirani ambnayo yanazungukwa na makanisa ili waweze kuwasaidia katika kuondokana na umaskini ndani ya maisha yao
Mchungaji huyo aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika shuguli za maendeleo na kuachana na tabia ya kukata tama kwa kisingizio kuwa maisha yao ni magumu

Vodacom and CCBRT launch a major public campaign against obstetric fistula


Vodacom and CCBRT launch a major public campaign against obstetric fistula with the aim of collecting one billion (TZS) to enable women suffering from fistula to get free treatment. Vodacom Tanzania, in collaboration with CCBRT, has today launched a MOYO (heart) campaign that aims to raise more than a billion Tanzanian shillings from the public to support maternal healthcare for women suffering an obstetric fistula in the country. Every year in Tanzania, an estimated 3,000 women develop obstetric fistula, a condition caused by prolonged or obstructed labour. Due to a lack of adequate maternal health facilities, the baby often dies during the labour and many of the mothers are left suffering from incontinence. "This is yet another initiative by Vodacom to support solving problems that exist in the communities as part of a company's commitment to see people living better life", said Vodacom Chief Officer of Marketing and Corporate Affairs, Ms. Mwamvita Makamba, during the press launch held today in Dar es Salaam. The MOYO campaign will raise funds from Vodacom customers and the general public. Contributions will be channeled through Vodacom M-PESA and will be used to cover free treatment to affected women at CCBRT's Disability Hospital in Dar es Salaam and its partner, Selian Lutheran Medical Centre, in Arusha. "It is not unusual for women suffering from fistula to be unable to have children, which in combination with incontinence can lead to ostracism from the family and society. These women are some of the poorest individuals in the community in which Vodacom operates; hence they need our support and humanity", said Ms. Makamba. Ms. Makamba added that the condition costs the lives of our beloved mothers, sisters and friends, and strips them of their happiness, confidence and dignity. It bring loneliness to them and sometimes their husbands run away from them amidst severe physical and psychological challenges. Vodacom and CCBRT want to do more. The goal is to make a difference to the women suffering from fistula in Tanzania by 2016 and eventually make them and everyone smile as the campaign aims to change lives. The MOYO campaign is the biggest health campaign to be initiated by any communication company in the country to address a specific challenge. It therefore reflects a true Vodacom commitment towards changing people's lives through mobile telecommunications technologies. "I and my company are very optimistic that everyone will take interest in, and hence contribute not only because women are important people in the family and community at large but also because we must ensure their dignity and decent living conditions regardless of their income status," added Ms. Makamba. Since 2010, Vodacom Tanzania has been in a partnership with CCBRT using mobile technology to remove the barrier of travel costs, enabling women to get the treatment needed using the M-PESA money transfer system.. CCBRT has appointed a series of ambassadors around the country who, when they diagnose women with this condition, can recommend them to the hospital for surgery. Within the hour, a date for the surgery is sent to the ambassador via SMS and money to cover the costs of travel is also sent to the ambassador via M-PESA. CCBRT Chief Executive Officer Erwin Telemans expressed his profound gratitude to Vodacom Tanzania, the Government of the United Republic of Tanzania and other stakeholders for their commitment in the fight against obstetric fistula. "The project we are launching today, in which CCBRT is partnering with Selian Lutheran Medical Centre in Arusha and other health facilities in the country, aims to facilitate the treatment of over 8,000 fistula patients during the next five years', Chief Executive Officer, Mr. Erwin Telemans explained. He added that, in the developed world, fistulas are caused by surgery, malignancy, radiography or a combination of all three; but, in the developing world, the most common causes are obstructed labor, poor delivery conditions , unskilled Caesarian sections and female genital mutilation. Mr. Telemans urged the Tanzanian community, the Government and other stakeholders to tackle these issues in order to end the suffering caused by fistula. The M- PESA initiative has so far enabled the treatment of over 600 women with fistula, and the target is to treat per year 1,000 such women at CCBRT and a further 250 at Selian Hosipital in Arusha by 2013 with all treatment free of charge. CCBRT and Vodacom call upon all stakeholders to restore the dignity of all Tanzanian women who are suffering from this treatable condition.

PINDA AONGOZA SHEREHE ZA CCM IRINGA

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiongoza matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha mika 35 ya CCM yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Ifwagi wilayani Mufindi, Iringa Februari 5, 2012. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Deo Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wa Mufindi wakitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara katika maadhimisho ya miaka 35 ya CCM yaliyofanyika kimkoa kwenye kijiji cha Ifwagi wilayani Mufindi, Iringa, Februari 5, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Wasanii wa Mufindi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Ifwagi wilayani Mufindi ambako Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikuwa Mgeni rasmi katika maadimisho ya miaka 35 ya CCM yaliyofanyika kimkoa Februari 5, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PIKIPIKI NA BAISKELI ZAGONGANA IRINGA

Ajali hii ilihusisha pikipiki na baiskeli katika eneo la Nduli mkoani Iringa. Barabara ni pana sana, lakini sijui ilikuwaje wakagongana. Mwendesha baiskeli aliyeketi alikuwa amepakia ulanzi.Inawezekana ni matokeo ya kilaji!
Manyerere Jackton

BONGO MOVIEYAIKANDAMIZA KADANSE FC YA WANAMUZIKI 4-3 UWANJA WA TAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Bongo Movie Vicent Kogosi (Ray), katika mchezo wa wanamuziki na waigizaji uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa leo, ili kuchangia wahanga wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es salaam na kusababisha vifo na uharibifu wa mali, mgeni wa heshima katika pambano hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik, wengine katika picha kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova Bongo Movie yaani waigizaji wameshinda magoli 4 wakati timu ya Kadanse FC ambayo imepata magoli 3 hivyo kufanya mpambano huo kumalizika kwa Bongo Movie kuchukua kombe la mashindano hayo ya kuchangia wahanga wa mafuriko ya Jangwani ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndiye aliyekabidhi kombe hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Bongo Movie mara baada ya kuishinda Kadanse FC goli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa jana.
Wachezaji wa Bongo Movie wakishangilia mara baada ya ushindi huo.
Mmoja wa waigizaji na shabiki wa Bongo Movie akimwaga mauono mbele ya mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo uwanja wa Taifa.
Refarii wa mchezo huo Bw. Othman Kazi akikabidhi kombe kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Said Meck Sadik ili naye akabidhi kwa washindi wa mchezo huo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiingia kwenye uwanja wa Taifa tayari kwa kutoa kombe kwa washindi mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kulia ni Kamanda wa Kamda maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova na kulia ni Kamishna Jamal Lwambo.
Rich Mtambalike "Rich Rich" kulia pamoja na Steven Nyerere wakimwaga mauno katika moja ya staili yao ya kushangilia ushindi wa timu yao ya Bongo Movie.
Vimwana wa Bongo Movie wakielekea uwanjani kushuhudia upokeaji wa kombe lao.
Vimwana wa Bongo Movie wakielekea uwanjani ilikuwa burudani kweli.
Wachezaji wa Bongo Movie wakiongozwa na Claudi wakishangilia kuzunguka uwanja mara baada ya mpira kumalizika huku timu yao ikiibuka mshindi kwa kushinda magoli 4-3 dhidi ya Kadanse FC ya wanamuziki.
Mwanamuziki Christian Bella wa bendi ya Akudo Impact katikati akiongozana na wenzake wakatika wachezaji hao waliposawzisha goli lao,
Mwanamuziki wa FM Academia Totoo Kalala akiukokota mpira kiuelekea goli la timu ya waigizaji wakati chezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa.
Hili ndiyo benchi la ufundi la timu ya Bongo Movie likogozwa na Mzee Chilo kushoto, JB Steven, Saimon Mwakifwamba na Cheki Budi.
Benchi la ufundi la Wanamuziki likiongozwa na Asha Baraka wa tatu kutoka kulia waliosimama na kulia ni MCD wa Twanga Pepeta, Yelo Masai wa FM Academia na kushoto ni Jose Mara wa Mapacha Watatu wakiwa pamoja na wachezaji na baadhi ya wanenguaji wa bendi tofauti.