TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 28, 2014

Mchawi Akutwa Kaanguka Nje Ya Kanisa Asubuni Alipokuwa Akiwanga Usiku.

Bibi kizee mmoja huko mkoani Mbeya ambae jina lake halikuweza kufaamika mara moja, amekutwa ameanguka nje ya kanisa akiwa uchi wa mnyama kwa kile kilichodaiwa alikuwa anawanga.
Kikongwe huyo alionekana ni mwenye kuishiwa nguvu pia kuhema sana, alipozinduka alijikuta amezingirwa na watu asubuhi huku akiwa ni mwenye woga wa wingi wa watu hao. Katika kumuhoji haraka haraka alieleza kuwa alikuwa anasafiri safari zake za usiku kutokea mkoani Morogoro kuelekea Ruvuma na alipopita maeneo hayo ya kanisa alijikuta anavutwa na kitu asichokijua ndipo kukapelekea kuanguka kwake.
Watu wa maeneo ya bibi huyo alipoanguka hawakuweza kumtambua na kuonekana hakuwa anaishi hapo ndipo walipomuuliza anakotoka na akajibu kuwa anatokea mkoani Morogoro na alikuwa anaenda Ruvuma kikazi yaani kazi zake za kishirikina.
Tukio la wachawi kuanguka karibu na maeneo ya makanisa mkoa wa Mbeya hutokea mara kwa mara na hivi inajiidhirisha kuwa nguvu za giza zinazotawala maeneo mbalimbali mbele ya mungu hufifishwa kama yaliyomkuta kikongwe huyu.

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS KUPELEKA MATAMASHA MENGINE MJINI SONGEA, NI KUTOKANA NA MWITIKIO WA WANASONGEA

Wngine ni Ambwene Mwasongwe, Bonny Mwaiteje, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa Kutoka nchini DRC Congo , Tumaini Njole, Titha Mutinda kutoka nchini Kenya Joshua Mlelwa na wengine wengi.Tamasha la leo lilikuwa ni la kwanza kufanyika mjini Songea na Mwandaaji wa tamasha hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama,  amesema kampuni hiyo inatarajia kufanya matamasha mengine ya injili katika mkoa huo wakati ujao kutokana na mwitikio wa watu wa Songea. 2Mwimbaji Upendo Kirahilo akipagawisha mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 3Mwimbaji Upendo Kirahilo akipagawisha mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 6Mwimbaji Upendo Kirahilo akserebeka na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama  alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 8Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na MC wa Tamasha hilo Bw. Mwakipesile wakielekea kumtunza mwimbaji wa muziki wa injili Joshua Mlelwa wakati alipokuwa akionyesha uwezo wake jukwaani kwenye tamasha la Krismas lililofanyika mjini Songea leo. 11Mgeni rasmi wa tamasha hilo Meya wa mji wa Songea Mh. Charles Mhagama akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili kwenye uwanja wa majimaji kutoka kushoto ni Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo John Melele. MC Mwakipesile na Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion. 9Mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje nakipagawisha mashabiki wake kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo. 10Mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje nakipagawisha mashabiki wake kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo. 12Somlomon Mkukubwa akiimba wimbo unaoelezea kisa cha mkono wake kukatwa ambao unamuelezea mama wa kambo aliyesababisha tukio hilo na kuwaasa mashabiki wake kusamehe kama yeye alivyomsamehe mama yake wa kambo 13Mashabiki wakiimba pamoja na mwimbajo Solomon Mukubwa 01
Mwimbaji  Ambwene Mwasongwe akiimba kwa hisia huku akishirikiana na mwimbaji Solomon Mukubwa wakati wa tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo kutoka kushoto ni Edson Mwasabwite na Faraja Ntaboba kutoka nchini DRC Congo.

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

 
Nkoromo Blog, Singida.
 
Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang’anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
“Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto”, alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM”, alisema.
Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo theNkoromo Blog)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS YAPONGEZA WATEJA WAKE ,SASA YAJA NA MWONEKANO MPYA

Furaha ya bidhaa mpya ya asas Dairies Ltd katika mwonekano mpya
Hivi ndivyo maziwa hayo yanavyoonekana kwa sasa
Na Matukiodaimablog
Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imewapongeza wateja wake kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutumia bidhaa zake .
Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu alisema hayo leo wakati akitoa salam za mwaka mpya 2015 na kutambulisha mwonekano mpya wa kisasa zaidi wa chupa za maziwa ya kampuni hiyo kwa sasa.
Alisema mbali ya mafanikio makubwa ambayo kampuni hiyo imefanikiwa kuyafikia kwa kuendelea kupata tuzo ya ubora wa maziwa kwa miaka takribani miwili sasa bado kampuni hiyo imejipanga kuporomoka katika ubora na katika kuhakikisha wanaendelea kushikilia nafasi ya kwanza na ubora wa maziwa nchini Tanzania hivi sasa tayari kampuni hiyo imekuja na mwonekano mpya wa maziwa yake kwa kuwa katika chupa tofauti na zile za mwanzo .
Hata hivyo alisema kuwa kuanzisha mwonekano mpya wa chupa za maziwa hayo kumekwenda sambamba na kuongeza ubora zaidi wa bidhaa hizo hivyo kuwakata watumiaji wa bidhaa zao kuanza kufurahia kuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 kwa kutumia maziwa yenye mwonekano tofauti na ule wa mwanzo
Pia alisema kampuni yake imekuwa mbele katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Iringa kama sehemu ya kutambua ushirikiano mkubwa wa kampuni kwa maendeleo ya Taifa .

Kiwelu alitaja moja kati ya shughuli ambazo kampuni imepata kusaidia kuwa ni pamoja na kuhamasisha jamii ya Iringa na watanzania kupenda kunywa maziwa kwa afya badala ya kutumia muda wao kuingiza sumu mwilini kwa kunywa pombe pia kampuni imepata kutoa msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.7 kwa shule za msingi tatu ambazo zilishinda katika mashindano ya uchoraji wa picha zinazoelezea umuhimu wa unywaji maziwa mashuleni

Mbali ya zawadi hizo kwa shule hizo tatu pia kampuni hiyo ilipata kuwanywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa.

Shule hizo zilizopatiwa msaada wa madawati ni pamoja na Hoho iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata madawati yenye thamani ya Tsh milioni 1 ,Mlangali iliyoshika nafasi ya pili na kupata madawati ya Tsh.750,000 pamoja na St Dominic iliyopata madawati yenye thamani ya Tsh 500,000.

MAMA PINDA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA UWT WILAYA YA MLELE

unnamed4Mkewa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayaya Mlele Mkoani Katavi kwenye shule ya Sekondari ya Mamba Desemba 28, 2014. (Pichana Ofisiya Waziri Mkuu)
unnamed5
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mlele mkoani Katavi vwakimsikiliza Mgeni rasmi Mama Tunu Pinda wakati alipofungua mkutano wao katika Shule ya Sekondari ya Mamba Desemba 28, 2014. (PichanaOfisiyaWaziriMkuu)
unnamedMkewa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Umoja waWanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakati alipowasili kwenye shule ya Sekondari ya Mamba  kufungua Mkutano wa Baraza hilo Desemba 28, 2014. (PichanaOfisiyaWaziriMkuu)
unnamed1Mkewa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akijumuika na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wanawake la Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakati alipowasili kwenye shule ya sekondari ya Mamba kufungua Mkutano wa Baraza hilo, Desemba 28, 2014. (PichanaOfisiyaWaziriMkuu)

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

index
LIGI KUU YA VODACOM YAINGIA RAUNDI YA 9.

Wakati raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo (Desemba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano.
Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
Nayo mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wakati huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Hamisi Kasanga.  
MBAO FC YAKAMATA USUKANI SDL
Timu ya Mbao FC ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.
Kwa matokeo hayo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC imeitoa kileleni JKT Rwamkoma baada ya kufikisha pointi tisa kwa kushinda mechi zote tatu dhidi ya Arusha FC, Pamba na JKT Rwamkoma.
Mbao FC inafuatiwa na JKT Rwamkoma yenye pointi sita, Arusha FC pointi sita wakati Bulyanhulu na Pamba zikiwa za mwisho kwa pointi moja kila moja. Kundi hilo litakamilisha mzunguko wa kwanza Januari 3 mwakani kwa mechi kati ya JKT Rwamkoma na Arusha FC, na Bulyanhulu na Mbao FC.
Katika kundi A, Mji Mkuu (CDA) na Singida United ndizo zinazochuana kileleni kwa kufikisha pointi saba kila moja. Timu hizo zinafuatiwa na Milambo yenye pointi nne, Mvuvumwa FC yenye pointi moja wakati Ujenzi Rukwa ni ya mwisho ikiwa haina pointi.
Hata hivyo, Mvuvumwa FC na Milambo ziko nyuma kwa mechi moja. Mechi hiyo ya kukamilisha raundi ya tatu kati ya timu hizo itachezwa kesho (Desemba 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kiluvya United imeendelea kuchachafya kundi C baada ya kushinda mechi zote ne ilizocheza, hivyo kufikisha pointi 12. Inafuatiwa na Mshikamano yenye pointi saba huku Abajalo ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 6.
Nafasi ya nne inashikwa na Transit Camp yenye pointi nne, Cosmopolitan yenye pointi mbili ni ya tano wakati Kariakoo ambayo haina pointi ni ya mwisho. Hata hivyo, Cosmopolitan na Kariakoo zina mchezo mmoja mkononi.
Mechi zinazofuata za kundi hilo ni Januari 3 mwakani kati ya Kariakoo na Mshikamano na Mshikamano (Ilulu), Transit Camp na Abajalo (Mabatini), na Cosmopolitan na Kiluvya (Karume).
Kundi D, vinara bado ni Njombe Mji yenye pointi 12 ikifuatiwa na Wenda yenye pointi sita wakati Volcano FC iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano. Mkamba Rangers ina pointi nne, Town Small Boys ina pointi moja wakati Magereza FC haina pointi.
Katika kundi hilo leo (Desemba 28 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Magereza itakayochezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.  Januari 3 mwakani kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Njombe Mji, Volcano FC na Magereza, na Wenda na Mkamba Rangers.

TAARIFA YA MSIBA

unnamedBI FORTUNATA RAYMOND (MENEJA NHIF LINDI) ANATANGAZA KIFO CHA BABA YAO MPENDWA MZEE RAYMOND KULLAYA KILICHOTOKEA TAREHE 21/12/2014 HOSPITALI YA DR. MVUNGI KINONDONI DAR ES SALAAM,MAZISHI YATAFANYIKA TAREHE 30/12/2014 KIJIJI CHA CHEKERENI-MOSHI.
IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU NA SHUGHULI ZA KUAGA KABLA YA SAFARI YA KUELEKEA MOSHI KWA MAZISHI ITAFANYIKA KATIKA KANISA KATOLIKI HANANASIFU KINONDONI SAA 6:00 TAREHE 29/12/2014.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO
        ***BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE***

DC Momba awataka wafanyabiashara Tunduma wasiogope mikopo

Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.
Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma.
Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo.

BENKI ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma imetoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Tunduma, wilayani Momba. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 100, ililenga kuwaelimisha wafanyabiashara hao kuhusu matumiza mazuri ya huduma za kibenki, hususan mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya, aliipongeza Benki ya Posta kwa kutoa mafunzo ambayo alisema yanawasaidia wafanyabiashara wa Tunduma kukuza uelewa wa matumizi sahihi ya huduma zinazotolewa na taasisi za fedha.
Aliwashauri wafanyabiashara wachukue mikopo ili kukuza mitaji yao na kuongeza uzalishaji, lakini bila kuwa na elimu sahihi juu ya matumizi ya mikopo hiyo faida yake inaweza isipatikane. “Nawashauri wafanyabiashara mnaohudhuria semina hii kutimia fursa hii kujadiliana na benki ya Posta ili mfikie muafaka katika huduma mnazozitaka,” alisema Mkuu wa Wilaya hiyo.
Aidha aliwaasa wafanyabiashara kujiepusha na biashara haramu zitokanazo na bidhaa haramu zilizozagaa mpakani mwa wilaya yao, kwani kufanya hivyo bishara zao zinaweza kutaifishwa na hivyo kupoteza mitaji yao bila kujua.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta, Henry Bwogi iliwasisitiza wafanyabiashara hao kutembelea tawi la benki hiyo lililopo Tunduma ili kujipatia huduma zote za kibenki hususan mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji yao. Pamoja na hayo aliongeza kuwa benki ya TPB inatoa mikopo ya aina nyingi, kuanzia ile ya vikundi hadi ya wafanyabiashara wakubwa, huku riba zinazotozwa na benki hiyo ni nafuu sana.

WAKAZI WA MKOA WA LINDI WATAKIWA KUSHIKAMANA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUJILETEA MAENDELEO – MAMA SALMA KIKWETE

IMG_7814Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Rasibura katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la Stendi huko Lindi Mjini tarehe 27.12.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI     
IMG_7579Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la Mbanja. Mama Salma alitembelea tawi hilo tarehe 27.12.2014 kwa ajili ya kukagua kazi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi. IMG_7630 Baadhi ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya Mbanja wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo tarehe 27.12.2014. IMG_7656Katibu wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 27.12.2014. IMG_7681Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika Kata ya Rasibura tarehe 27.12.2014.
………………………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
 Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kushikamana kwa  pamoja, kufanya kazi kwa bidii  na kuzitumia rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa jana Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mitwero Stendi Kata ya Rasibura wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mkoa wa Lindi  umejaliwa kuwa na rasilimali nyingi  ikiwa ni pamoja na zao la korosho, ardhi yenye rutuba, bahari  na  gesi lakini bado kuna changamoto zinazowakabili wananchi na hivyo kukwamisha maendeleo yao.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na elimu kwani baadhi ya wanafunzi wafikapo darasa la tano wanaacha  shule kwa ajili ya utoro, mimba za utotoni na vijana kutokufanya kazi kwa bidii.
“Kuna baadhi ya watoto wakifika darasa la tano wanaanza tabia ya utoro hakikisheni wanakwenda shule kusoma kwani elimu itawasaidia katika maisha yao,  msikubali waache shule.  Kutokana na umri wao mdogo wanaona  raha kuacha shule na kwenda kucheza lakini wakifika umri wa utu uzima ndiyo watakapoona umuhimu wa elimu”.
Maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana ikiwa kila mtu atapata elimu itakayomsaidia  katika maisha yake, wakati shule za Sekondari za Kata zinajengwa kuna baadhi ya watu walitubeza na kuziita majina ya ajabu ikiwa ni pamoja na shule za Yeboyebo lakini shule hizi zimewasaidia watoto wengi kutoka familia maskini ambao wameweza kupata elimu”, alisema Mama Kikwete.
Kuhusu  tazizo la mimba za utotoni alisema ni hatari kwa maisha ya Mama na mtoto lakini kama kijana atasoma mimba zitaepukika,  jukumu la wananchi ni kuhakikisha watoto wao wanasoma  kwa bidii na kutokubali  kupewa  mimba ambazo zitawakatisha masomo.
Kwa upande wa vijana MNEC huyo aliwahimiza kuangalia  mstakabali wa maisha yao na kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwani hizi sasa kuna baadhi ya vijana wakati wa  asubuhi wanaacha kwenda shamba kulima na kucheza Pool kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata maendeleo.
“Vijana wengine wanatumia  madawa ya kulevya na kuvuta sigara wanajua kwa kufanya hivyo ndiyo ujanja kitendo ambacho siyo ukweli,  bali unaharibu afya yako na kujirudisha nyuma kimaendeleo. Kama wewe kijana unahitaji kuwa na maisha bora ni lazima uachane na vitendo hivyo na kufanya kazi”, alisisitiza.  
Licha ya kufanya mkutano huo wa hadhara  Mama Kikwete pia alifanya vikao na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM matawi ya Mbanja, Mabano na Mitwero Stendi na kuwataka wajumbe hao kuwapa vijana  nafasi za uongozi pale watakapojitokeza kugombea nafasi hizo.        
Pia aliwahimiza wajumbe hao wakiwemo vijana, wanawake na wanaume kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani ili kuwe na ushindani wa kutosha ndani ya chama.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kichama na katika mkutano wa hadhara aligawa kadi kwa  wanachama wapya 23 walijiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Kiongozi wa Al-Shabaab akamatwa

Kundi la wapiganaji wa Al shabaab
Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali.
Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo ameiambia BBC Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupashwa habari.
Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi.
Kundi la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Alshabaab upande wa Amniyat.
Mapema mwaka huu alikosana na kiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane ambaye aliuawa katika mashambulizi ya Marekani mnamo mwezi Septemba.

Indonesia yasitisha utafutaji wa Airasia

Airasia iliotoweka
Indonesia imesitisha utafutaji wa ndege ya AirAsia hadi kesho iliopotea na takriban abiria 160 waliokuwa wakielekea Singapore kutoka mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
Takriban abiria 162 walikuwa wakiabiri ndege hiyo aina ya Airbus 320 wengi wao wakiwa raia wa Indonesia.
Ndugu na familia za waathiriwa wa AirAsia wakisubiri habari za kutweka kwa ndege hiyo
Rubani wa chombo hicho anadaiwa kutaka kubadilisha njia ili kuepuka kimbunga lakini hakuomba usaidizi wowote.
Baadhi ya meli katika eneo hilo zinaendelea kuitafuta ndege hiyo,licha ya hali mbaya ya hali ya anga
Familia na marafiki wa waathiriwa wamekongamana nchini Singapore na uwanje wa ndege wa surabaya wakingojea habari kuhusu ndege hiyo.

Aliyetaka kumuua Papa John Paul amuenzi


Mehmet Ali Agca aliyetaka kumuua papa John wa Pili mwaka 1981.
Mwanamme mmoja raia wa Uturuki aliyempiga risasi na nusura amuue aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki papa John Paul wa pili mwaka 1981 ameweka maua kwenye kaburi lake katika makao makuu ya kanisa katoliki ya Vatican.
Ziara ya Mehmet Ali Agca kwenye makao ya Vatican inafanyika miaka 30 tangu John Paul amtembelee gerezani na kumsamehe kwa kujaribu kumuua.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa
Aliachiliwa kutoka gerezani nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye akatumikia kifungo chengine cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa tofauti.
Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.

Wanaume waliooana wapunguziwa hukumu

Wanaume waliooana Misri wapunguziwa hukumu jela
Mahakama moja ya Misri imepunguza hukumu ya watu wanane waliodaiwa kushiriki katika ndoa ya watu wa jinsia moja kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja.
Mwezi Uliopita ,wanane hao walipatikana na hatia ya kuchochea uasherati.
Walishtakiwa baada ya kanda moja ya video kusambaa katika mitandao ikiwaonyesha wakisherehekea katika boti moja lililokuwa mto Nile huku wanaume wawili wakionekana wakivalishana pete na kukumbatiana.
Watu hao baadaye walikataa kwamba ilikuwa harusi ya watu wa jinsia moja.
Ushoga ni kinyume na utamaduni wa Misri ,ijapokuwa si kinyume na sheria.
Wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu wanasema kuwa kampeni dhidi ya mashoga imeimarishwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni nchini Misri.

Feri ya abiria 460 yashika moto Ugiriki


Feri yashika moto ikiwa na abiria 460
Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kwneye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe .
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.

Malaysia:Waziri mkuu akatiza ziara

Mafuriko nchini Malaysia
Waziri mkuu nchini Malaysia amesitisha ziara yake nchini Marekani na kurejea nyumbani kuweza kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na janga la mafuriko mabaya tangu miaka kumi iliyopita.
Uamuzi huo wa Najib Razak unafanyika baada ya shutuma dhidi ya serikali kwa kukosa kutangaza hali ya hatari kwenye majimbo matano yaliyo kaskazini mashariki mwa nchi.
Kupanda kwa haraka kwa viwango vya maji kumewalazimu zaidi ya watu 100,000 kuhama makwao.
Watu watano waliuwa.
Waziri mkuu aliyekuwa akicheza gofu na rais obama akatiza ziara yake nchini humo ili kushungulikia mafuriko nchini mwake
Mvua zaidi inatarajiwa kunyesha katika maeneo ya kusini mwa nchi saa zinazokuja.
Bwana Razak alishutumiwa baada ya picha zake alizokuwa akicheza gofu na rais wa Marekani Barack Obama kusambaa mitandaoni.

Ndege ya AirAsia yapotea na abiria 160

Ndege ya AirAsia
Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.
Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

WANACHAMA WAKE 42 WATIMULIWA CHADEMA

index
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatimua wanachama wake 42 wakiwemo wagombea walioshindwa kupita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, kutimuliwa kwa wanachama wake hao ni hatua ya chama hicho kujisafisha kutokana na kile kinachodaiwa kwamba baadhi ya wagombea hao wanatuhumiwa kufanya hujuma wakati wa mchakato wa uchaguzi serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.

Akitangaza uamuzi huo mjini humo, Katibu wa Chadema Jimbo la Korogwe Mjini, Ezekiel Mbwilo alisema wahusika waliotimuliwa uanachama wanatuhumiwa kwa kukubali vitisho na wengine kurubuniwa kwa fedha za wapinzani wao, hatua iliyowalazimu kwenda kuondoa majina yao katika hatua za mwisho kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.

“Tuligundua kuwa baadhi ya wahusiska walijihusisha na hujuma mbalimbali dhidi ya chama chetu, ikiwamo kukubali kupewa fedha na wapinzani wao ili wajiondoe. Tangu awali, tulishakubalina kwamba ikibainika watu waliofanya hujuma tutawatimua kundini na hapa ndipo tunahitimisha lile tulilokubaliana,” alisema.

Mbwilo alitaja maeneo wanayotoka wanachama hao waliotimuliwa na idadi yao kwenye mabano ni Kwamsisiwatu (6), Mahenge (10), Kitifu (25) pamoja na mmoja kutoka Manundukati ambaye alidai kwamba mhusika huyo aliamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi ukiwa katika hatua za mwisho baada ya kurubuniwa na wapinzani wa chama hicho.

Akizungumzia vitisho alivyodai vilitolewa baadhi ya wanachama wa vyama vingine dhidi ya wagombea wa Chadema, Mbwilo alisema tayari amewasilisha taarifa hizo kwenye vyombo vya usalama na katika jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Tibaijuka:Nitatetea kiti changu

Aliyekuwa waziri wa Ardhi na makao nchini Tanzania Anne Tibaijuka anasema kuwa atatetea kiti chake cha ubunge licha ya kashfa ya Escrow
Siku kadhaa tu baada ya rais Kikwete kumfuta kazi Anne Tibaijuka kama waziri wa ardhi,nyumba na makao ,kiongozi huyo amewaambia wakaazi wa bunge lake kwamba hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao wa bunge, kulingana na gazeti la The citizen nchini Tanzania.
Tibaijuka alipigwa kalamu kutokana na maadili yake kufuatia kashfa ya akaunti ya tageta escrow ambapo alipokea sh.billioni 1.6.'' Mungu anayetoa ndiye aliyechukua jina la mungu libarikiwe alisema tibaijuka akimaanisha kuwa yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri ndiye aliyekichukua.
Katika kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti chake katika uchaguzi wa 2015,Tibaijuka aliwaonya wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo chagua bora la wapiga kura.
Kulingana na The Citizen kiongozi huyo aliwashukuru wapiga kura wa eneo bunge lake kwa kumchagua kuwa mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa uwaziri.
''Lazima muelewe kwamba ninyi mulinipigia kura mimi ili niwahudumie bungeni na sio kama waziri,kwa hivyo yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa tayari kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa Muleba.
Hatahivyo bi Tibaijuka amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa upinzani waliochaguliwa katika uchaguzi wa madiwani wa hivi karibuni

AVAMIWA NYUMBANI PARK NA KUJERUHIWA VIBAYA MMILIKI NA KUPORWA FEDHA

Farida mess Matlou
Sehemu alizoathilika
Mkurugenzi mtendaji wa Nyumbani Park & Samaki Sport Farida mess Matlou alivamiwa na majambazi na kumjeruhi.Tukio hilo lilitokea usiku wa Trh 19 kuamki 20 maeneo ya nyumbani kwake Kihonda.

Kwa taarifa zilizofikia mtandao huu ni kwamba tayari watu wawili wamekatwa kuhusishwa na tukio hiloMkurugenzi huyu alivamiwa usiku wa saa saba.