TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 10, 2015

SERIKALI HAITORIDHIA KUWAACHA WAPANGAJI NA WAFANYABIASHARA KATIKA JENGO LA TRENI KUEPUSHA MAAFA

Na Abdulla Ali   Maelezo-Zanzibar.    
                                         
Serikali haitoridhia kuwabakisha Wapangaji na Wafanyabiashara katika jengo la Treni ili kuepusha maafa na kuokoa maisha ya Wananchi na mali zao.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban wakati wa mkutano wa mzungumzo ya pamoja kati ya Wapangaji na  Wafanyabiashara wanaolitumia jengo hilo na Serikali uliofanyika katika ofisi ya Mamlaka ya Mji Mkongwe iliopo Forodhani Mjini Zanzibar.  

Waziri huyo amesema kuhamishwa kwa Wakaazi na Wafanyabiashara katika jingo hilo sio jambo la mjadala kama wanavyotaka wao bali ni wajibu wao kufuata maagizo ya serikali ili kuepukana na vifo visivyo vya lazima na hasara za mali zao pindi jengo hilo litakapo poromoka na kupelekea kuitupia lawama serikali pale majanga yatakapotokezea. “Hili si jambo la majadiliano kama mnavyotaka nyinyi”, alieleza Waziri Ramadhan.  

Ametanabahisha kuwa serikali imeshachukua hatua mbalimbali za kulijenga tena jengo hilo ikiwemo kutafuta mafundi, wahandisi pamoja na vifaa vya ujenzi na inategemewa hivi karibuni kuanza rasmi kwa ujenzi huo.

Aidha waziri ramadhan amewataka Wapangaji na Wafanyabiashara hao kutokaidi agizo la Serikali kwa usalama wa mali na maisha yao kwani jengo hilo linaonekana halitoweza kuhimili mvua za Masika zinazotarajiwa kuanza mwezi machi mwaka huu na badala yake linaweza kuporomoka kutokana na mvua hizo.

Jengo la Treni liliopo Darajani Mjini Zanzibar lina wakaazi 57 wakiwemo Wapangajia na Wafanyabiashara ambapo kwa sasa hali yake hairizishi baada ya kupasukapasuka na kutishia usalama wa maisha ya watu wanaoishi humo pamoja na wapita njia.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI GEORGE SIMBACHAWENE AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI NISHATI ENDELEVU NCHINI KWA WOTE

 Waziri wa Nishati na Madini  George Simbachawene akifungua mkutano  kwa ajili ya  kujadili nishati endelevu  nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable  Energy for  All)  ulioshirikisha  sekta binfasi,  wataamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini.  Mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya   Protea jijini  Dar es Salaam  lengo lake lilikuwa ni kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuboresha  sekta ya umeme  nchini. 
 Meneja   Hifadhi kutoka Shirika la WWF Nchini Dk. Amani Ngusaru  akitoa hotuba ya kumkaribisha  Waziri wa Nishati na Madini George  Simbachawene (hayupo pichani)

NAPE ATEMBELEA OFISI ZA MAJIRA LEO

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akisisitiza CCM kuendelea kuimarisha ushirikiano na uwazi na vyombo vya habari, mwishoni mwa mazungumzo yake na wahariri wa magazeti ya kampuni ya BTL,  Wachapishaji wa Magazeti ya Majira, Bussines Times na Sports Starehe,  Wapili kushoto ni Mtahiriri wa Majira Eckland Mwaffisi na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imma Mbuguni. Picha zote na Bashir Nkoromo).
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Bussines Times, Wachapichaji wa Magazeti ya Majira, Bussines Times na Sports Starehe, akiwa katika mwendelezo wa ziara ya vyombo vya habari aliyoaianza wiki iliyopita mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtahiriri wa Majira Eckland Mwaffisi na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imma Mbuguni.

MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR YAFANYIKA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati  wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary

VIONGOZI WA KANISA LA ANGLICAN WATEMBELEA SHAMBA LA WAZIRI MKUU ZUZU DODOMA KUJIFUNZA KILIMO BORA CHA ZABIBU NA EMB 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea malisho ya ng’ombe  kwenye shamba lake  lililopo  Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo.  ANGLI4 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (wapili kushoto) na  kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mwakyembe azungumzia Kenya kuzuia magari ya Tanzania Viwanja vya Ndege






Tarehe 22 Desemba, 2014, Serikali ya Jamhuri ya Kenya ilitoa amri ya kuzuia magari ya kitalii yenye usajili wa Tanzania kwenda kuchukua na kushusha watalii wanaotumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakiwa njiani kuja kutembelea vivutio vya utalii katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. 

Baada ya uamuzi huu wa Serikali ya Kenya, Waziri wa Maliasii na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu alifanya majadiliano na Waziri wa masuala ya utalii wa Serikali ya Kenya siku ya tarehe 16, Januari, 2015 ili kutafuta ufumbuzi wa kadhia hii. Matokeo ya mkutano wa Mawaziri hawa yalikuwa ni kusitishwa kwa muda katazo lililotolewa na Serikali ya Kenya kwa makubaliano kuwa yafanyike mazungumzo baina ya pande hizi mbili ndani ya kipindi cha wiki tatu kuanzia tarehe 16 Januari, 2015 ili kurekebisha Mkataba wa Ushirikiano katika sekta ya utalii wa mwaka 1985 kati ya nchi zetu mbili.

Airtel yazindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi kwa Wakazi wa Mwaza

Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari ( pichani hawapo) wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. kushoto Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma na Kulia ni Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael.
 Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael 

JENGO MOJA MTAA WA LIBYA/MOSKI-KARIAKOO JIJINI DAR UMEZUKA MOTO MKUBWA NA KULETA MACHAFUKO

 Moto uliozuka mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.
Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Libya na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kilkuwepo eneo la tukio na kukuletea kila kilichojiri ,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walieleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo huku kikosi cha zimamoto na magari nayo yaliendelea  kuwasili kupambana na moto huo..

Monday, February 9, 2015

REDDS MISS TANZANIA 2013- HAPPYNESS WATIMANYWA AFUNGUA CLUB YA KUJISOMEA WATOTO YA NKEMA

 Redds Miss Tanzania 2013, Happness Watimanywa (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Club ya kujisomea watoto ya ijulikanayo kwa jina la Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Mtaa wa Kasana jirani na Kituo kinachojengwa kwa ajli ya Mabasi ya Mwendokasi nyuma ya Sheli ya Mwanamboka katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo, Getrude Kilyabusebu.
 Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa (kushoto), akiwafundisha kusoma watoto wakati wa hafla ya kufungua Club ya  kujisomea watoto ya Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa mgeni rasmi.

SKYLIGHT BAND YAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE NDANI YA NYAMA CHOMA FESTIVAL

DSC_0020
Kikosi cha Skylight Band kikiongozwa na mkongwe wa muziki wa Live Band, Joniko Flower (kushoto) kutoa burudani kwa mashabiki wake ndani ya viwanja vya Leaders Club kwenye tamasha la Nyama Choma lilifanyika mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Sam Mapenzi, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Sony Masamba.
DSC_0025Swagga za Skylight Band hii inafahamika kama “Mashauzi” mkongwe Joniko Flower akiwasebenesha mashabiki wake ( hawapo pichani).

MKUTANO WA KUJADILI NAMNA YA KUKABILIANA NA MAAFA MBALIMBALI WAFANYIKA ZANZIBAR.

1
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipoingia katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
2
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akisalimiana na Command Surgeo Usafricom Philip C Knight Sheen alipoingia katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.

UWANJA WA MCHEZO WA GOFU WAZINDULI ZANZIBARI

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini akisalimiana na wageni waliohudhuria  katika ufunguzi wa Kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu jana uzinduzi alioufanya kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.
Picha na Ikulu
2
Mwenyekiti wa Kampuni ya Sea Cliff Resort and Spa Zamzibar Bw.Subhash Patel (kushoto) akibadilishana mawazo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungua kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu jana alipomuwakilisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPUNGUA

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Januari, 2015 leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
9/2/2015, Dar es salaam.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2015  umepungua hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ya mwezi Desemba, 2014 kutokana na kuendelea kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini.

Mjue Magdallena Alphonce Shija A K A Dorcas-Chipukizi wa Muziki wa Injili TANZANIA.

Magdallena  Alphonce Shija A K A Dorcas, akiwa kwenye Utunzi wa baadhi ya nyimbo zake.
Magdallena  Alphonce Shija A K A Dorcas, alizaliwa  tarehe 5/7/1990, katika familia ya Mzee Alphonce Shija, yenye watoto 11 na yeye akiwa ni mtoto wa tisa (9) kuzaliwa kwa upande wa baba yake lakini pia kwa upande mwingine wa mama yake ni mtoto wa nne (4) kuzaliwa kutokana na kwamba wazazi wake walitengana baada ya yeye kuzaliwa wakati huo Magdallena akiwa ni mtoto mdogo mwenye umri wa Miaka 2.

AFTER EXAM PATY UNIVERCITY BASH 2015

Chuo cha Diplomasia Kurasini kwa Kushirikiana na DUCE, wanakuletea School Bash University siku ya ijumaa tarehe 13 itakayofanyika kwenye chuo cha Diplomasia Kurasini, 
kwa mujibu wa waandaaji wa Hafla hiyo, ina lengo la kuwapa burudani wanafunzi kutokana na kwamba siku hiyo wanakuwa wamemaliza Mitihani na hivyo kuwa kujiandaa na likizo fupi.

Hakuna kiingilio kwa wanafunzi wote wakati wa kuingia Ukumbini ambako watafurahia kwa Kucheza Pamoja kati ya vyuo hivyo Viwili. Wote mnakaribishwa sana.


Kesi ya Al Jazeera Misri yarejelewa

Wakuu wa mahakama nchini Misri wamesema kuwa marudio ya kesi ya waandishi habari wawili wa Al Jazeera yataanza Alhamisi.
Mohamed Fahmy na Baher Mohamed walikutikana na hatia ya kusaidia chama cha Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku.
Kesi hiyo ilizusha malalamiko kimataifa.
Wafungwa wameshatumika siku 407 gerezani.
Mwenzao, Peter Greste, raia wa Australia ambaye alifungwa nao, alifukuzwa ndani ya nchi juma lilopita.

Ivory Coast mabingwa wa Afrika

  Fainali ya Michuano ya Afrika imemalizika juzi jana ambapo Ivory Coast wamefanikiwa kuibuka mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 baada ya kufuinga Ghana kwa penalti 9 - 8 katika mchezo wa fainali ulichezwa katika uwanja wa Estadio de Bata huko Equatorial Guinea. 

 Mlinda Mlango wa Ivory Coast Boubacar Barry ambaye alikuwa hapangwi mara kwa mara lakini ndiye aliyeibeba Ivory Coast baada ya kudaka penati na kufunga penalti ya mwisho.

15 waokolewa katika ajali ya ndege

Picha ya maktaba ya ajali ya ndege iliyotokea nchini Taiwan, mwaka 2014 ya shirika la TransAsia.
Picha ya maktaba ya ajali ya ndege iliyotokea nchini Taiwan, mwaka 2014 ya shirika la TransAsia.

Wafanyakazi wa uokozi nchini Taiwan, wametumia “crane” kuinua sehemu ya mabaki ya ndege ya abiria iliyoanguka Jumatano, nje ya mji wa Taipei.
Ajali hiyo mpaka sasa imeua watu karibu 25, na kuacha wengine 20 wakipotea katika mto wenye kina kidogo.
Ndege hiyo aina ya ATR-72 iligusa daraja kwa bawa lake moja na kudondokea katika mto Keelung mara baada ya kuruka aiku ya Jumatao.
Picha na video zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, zinaonyesha ndege hiyo katika nyuzi 90, na kwa kiwango kidogo ilikosa kugonga magorofa marefu ambayo ni makazi ya watu.
Boti za uokozi zilizunguka ndege hiyo iliyokuwa imeanguka juu chini na kuwatoa abiria 15 kwenye usalama akiwemo mtoto.
 Mkurugenzi wa shirika la TransAsia, Chen Xinde, baadaye alitoa rambi rambi zake na kuomba radhi kufuatia ajali hiyo katika mkutano na wanahabari.

Zaidi ya Watu 20 wapoteza maisha Misri

Misri imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi hiyo baada ya watu zaidi ya Watu 20 kufariki dunia.
Kati ya waliofariki ni wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Mtandao mmoja nchini humo uitwao AL-Misriyun umeripoti.Tukio hilo limetokea baada ya Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mashabiki walikokuwa wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.

Uchaguzi wa Nigeria waahirishwa.

Wafuasi wakimkaribisha mgombea urais  Muhammadu Buhari (ndani ya gari),  wa chama cha All Progressives Congress party, wakati alipotembelea  Gombe Ewakati wa mkutano wa uchaguzi February 3, 2015.
Wafuasi wakimkaribisha mgombea urais Muhammadu Buhari (ndani ya gari), wa chama cha All Progressives Congress party, wakati alipotembelea Gombe Ewakati wa mkutano wa uchaguzi
Shutuma zimeongezeka Jumapili huko Nigeria  baada ya uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa urais February 14 kutokana na wasiwasi wa usalama kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Boko harm.
 Chama cha upinzani All Progressive Congress (APC) kinachoongozwa na dikteta wa zamani wa jeshi Muhammadu Buhari, kilieleza kuahirishwa huko kama kikwazo kikubwa kwa demokrasia ya Nigeria  lakini kikawataka Wanigeria wote kuwa watulivu.
Jumamosi mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Attahiru Jegga alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa kiti cha rais na wabunge kutoka February 14 hadi Machi 28.