TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 5, 2015

MWANAHARAKATI WA SIKU NYINGI WA WANYAMAPORI NCHINI TANZANIA AMPONGEZA RAIS KENYATTA

IMG_1715
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye harakati zake za matatembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na wanaharakati wenzake wa huko Philipine
IMG_1734
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye matatembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na Susan Jaylo

Rais Kikwete amtembelea Rubani wa ndegevita Hospitali ya Jeshi Lugalo

muh1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakimjulia hali Meja Peter Lyamuya aliyelazwa katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam akiuguza jeraha la mguu alilopata baada ya ndege ya kivita aliyokuwa akiiendesha kuanguka na kulipuka wiki iliyopita.Askari huyo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo iiyosababishwa na ndege mnyama kuingia kwenye injini na kusababisha hitilafu iliyopelekea kushika moto, kuanguka na kulipuka.Ndege hiyo ilikuwa katika mazoezi ya kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.(picha na Freddy Maro) muh3

UFAFANUZI JUU YA HALI YA AFYA YA NAIBU SPIKA

indexKumekuwa na taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii kuhusu hali ya Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa, taarifa hizo zinazosambazwa katika baadhi ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu.
Ukweli ni kwamba Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ni Mzima wa afya na hivi sasa yuko jimboni kwake Kongwa, Mkoani Dodoma akifanya maandalizi ya Mwisho ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii na hasa Jimboni Kongwa, Dodoma.
Ofisi ya Bunge inapenda kuwatoa hofu Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa si za kweli bali ni uvumi unaonezwa na watu wachache wenye nia ovu ya kujenga hofu miongozni mwa Wananchi kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha tunapenda kutoa rai kwa watu wote kuacha kusambaza taarifa hizo potofu na badala yake kama kuna taarifa zozote kuhusu Ofisi ya Bunge au Viongozi wake wafanye jitihada za kuthibitisha taarifa hizo kwenye Mamlaka husika kabla za kuzisambaza.
Ofisi ya Bunge inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na umma kwa ujumla, hivyo si vyema kwa watu kusambaza taarifa potofu kuhusu Bunge na viongozi wake ambazo zinaweza kuleta usumbufu miongoni mwa Viongozi na baadhi ya wananchi. Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge DAR ES SALAAM 4 MACHI 2015

MAONESHO YA UTALII YA ITB YAANZA RASMI UJERUMANI

men1Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh. Philip Marmo katika picha ya pamoja na mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi za jumuia ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani sambamba na maafisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha pamoja kujadili imaandalizi ya ‘siku ya jumuia ya Afrika Mashariki’ katika maonesho ya ITB itakayo fanyika tarehe 6/2/2015.
men2Waionsehaji kutoka Tanzania wakiwa katika mazungumzo ya Kibiashara na wenzao kutoka nchi mbalimbali katika sikuu ya kwanza ya maonesho ya ITB jijini Berlin Ujerumani.

Komba alikuwa Makamu Mwenyekiti SHIWATA

index
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unaungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha Makamu Mwenyekiti wao, John Komba aliyefariki Jumamosi na kuzikwa jana nyumbani kwao kijiji cha Litui, Mbinga mkoa wa Ruvuma. Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib katika salamu zake za rambirambi alisema mtandao huo umempoteza kiongozi mwadilifu aliyetumia kipaji chake cha usanii kuwaunganisha makundi ya wanamichezo,waigizaji, wasanii wa luninga, bongo movie,wacheza sarakasi na waandishi wa habari kuunda mtandao huo.
Alisema Kepteni Komba siku zote za maisha yake aliamini sanaa ni mkombozi wa wanyonge katika jamii ambako alitumia fani yake ya ualimu kufundisha wasanii wa fani mbalimbali alipokuwa na kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT), aliunda Kwaya, maigizo, sarakasi, taarab na muziki wa dansi.
Marehemu Komba akiwa na kikundi chake cha TOT aliibua vipaji vya wasanii mbalimbali waliotamba zamani na wengine bado wanaendelea kutamba katika kama Nasma Hamisi Kidogo, Laila Khatib, Sheba Juma, Selemani Pembe, Banza Stone, Mohamed Mrisho, Badi Makule, Ali Star, Khadija Kopa, Othman Sudi, Abdul Misambano, Mwanamtama Hamisi na Haji Boha.
Taalib alisema SHIWATA imempoteza kiongozi aliyekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha mtandao huo kwa hali na mali na kuwashawishi wasanii wake wa TOT kujiunga na mtandao huo ili kushirikiana katika kujenga kijiji cha wasanii cha Mwanzega, Mkuranga.
Marehemu Komba ambaye alikuwa mwanachama mwenye kadi namba moja wa SHIWATA kati ya wanachama 8,000 wa mtandao huo alikuwa akilipia michango yake na kuwa mfano kwa wengine.
Taalib alisema SHIWATA imewapoteza wanachama maarufu katika kipindi cha karibuni na hivyo kuongeza pengo katika utendaji wake kama Ibrahim Muchacho, Fundi Said (Mzee Kipara), Seteven Kanumba, Hamisi Amigolas na Amina Ngaluma.
Alisema katika uongozi wa marehemu Komba amesaidia kujengwa kwa nyumba 104 za wasanii katika kijiji cha Mwanzega ambapo wasanii wanaendelea na ujenzi.

HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA YAZIDUA UPIMAJI, USIKIVU WA WATOTO WACHANGA.

mna1
Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
mna2
Daktari Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika uzinduzi wa kuwapima  usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
mna3
Wafanyakazi wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
mna6
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
mna5
Baadhi ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja.
…………………………………………………………………….
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.  
Waziri wa Afya wa Zanzibar  Rashid Seif Suleiman amesema sikio,  mdomo  na macho ni sehemu muhimu sana katika maisha ya  binaadamu hivyo unapokuwa na   wataalamu wa  kushughulikia viungo hivyo ni neema kubwa inayopaswa kuenziwa.
Haya ameyasema jana katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati wa uzinduzi  wa kuwapima usikivu watoto wachanga mara  baadaya kuzaliwa ili kujua matatizo yao.
Amesema uchunguzi  wa watoto wachanga kujua usikivu wao  mapema ni mpango mzuri  ambao utalisaidia Taifa kuwa na   watoto wenye usikivu  mzuri na njia rahisi  ya kuwapatia matibabu kwa watakaogundulika na matatizo hayo.
“Kujua tatizo la kiafya mapema na kuanza kulishughulikia kunapunguza gharama za matibabu hivyo nawanasihi wazazi kuwapeleka watoto wenu mara baada ya kujifungua, ”alisisitiza Waziri wa Afya.
Amesema  maradhi ya usikivu  yamekuwa yakiwasumbua watoto wengi Zanzibar na iwapo kila mzazi atatimiza wajibu wake wa kumpeleka  mtoto wake  kupata vipimo yataweza kupungua.
Waziri wa Afya aliwataka wazazi  kuwa na utamaduni wa kuzalia Hospitali  ili kupata huduma hiyo kwa urahisi na watakaozalia majumbani  kuwapeleka watoto wao kuchunguzwa usikivu mara baada ya kuzaa.
Aidha Waziri huyo aliwataka madaktari  waliopatiwa mafunzo ya kutoa huduma hiyo kuwa waadilifu katika kutekeleza kazi zao kwani huduma za watoto wachanga  na wazazi zinahitaji uvumilivu.
Waziri alisema tatizo la uskivu huazia  mtoto  anapochelewa kulia mara baada ya kuzaliwa ama wanapopata homa ya manjano, kutopatiwa chanjo, mzazi kuchelewa kuzaa baada ya uchungu wa muda  mrefu na kuzaliwa mtoto bila ya ya kufika muda wa kuzaliwa.
Nao madaktari walio patiwa mafuzo hayo walisema kuwa wana uwezo mzuri wa kuwapima usikivu watoto  na kubaini matatizo yao  na kuishauri Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia watoto watakaozaliwa vijijini.
Mradi huo wa kupima watoto usikivu ulipokea msada wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kutoka Jumuiya ya Madaktari wanotoa huduma za matibabu vijijini ( ZOP) ambavyo vina thamani vya Dola elfu 50 za kimarekani.

SHIRIKA LA EfG LAWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUTOKA LUSHOTO MKOANI TANGA NA TEMEKE KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA MASOKO YA MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM

 Ofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline Mdendemi  akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni katika soko la Mchikichini Dar es Salaam jana kutoka Wilaya ya Lushoto ambao wamekuja Manispaa ya Ilala kwa mafunzo ya siku tatu  kuhusu mambo mbalimbali pamoja na masuala ya vicoba.
 
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (katika), akizungumza na wanawake wajasiriamali.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake Soko la  Mchikichini, Juliana Richard akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
 Mjasiriamali kutoka Lushoto Tanga, Magreth Mkomwa (katikati), akiuliza swali katika mafunzo hayo.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Mwenyekiti wa Soko la Lukozi lililopo wilayani Lushoto, Zakati Tendwa akichangia jambo.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wajasiriamali hao wakitembelea soko la Mchikichini kuona kazi za wenzao zinauzwa katika soko hilo.
 Hapa wakiangalia nguo aina ya batiki zinazotengenezwa na wenzao wa soko hilo.
Hapa wakifurahia gauni la batiki katika soko hilo.
 
Dotto Mwaibale
 
WANAWAKE wafanyabiashara katika masoko wametakiwa kujenga tabia ya kutunza kumbukumbu zao na kufanya vikao vya mara kwa mara jambo litakalosaidia kuwapunguzia changamoto za kazi zao.
 
Mwito huo ulitolewa na Ofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline Mdendemi wakati akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni Dar es Salaam jana kutoka Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga na Manispaa ya Temeke ambao wapo  Manispaa ya Ilala kwa ziara ya siku tatu ya mafunzo mbalimbali pamoja na masuala ya vicoba  yaliyofikia tamati jana. 
 
“Jengeni tabia ya kutunza kumbukumbu zetu pamoja na kufanya vikao vya mara kwa mara itawasaidia kujua changamoto mlizonazo na kuzitatua ” alisema Mdendemi.
 
Mdendemi alisema shirika hilo la EfG limefanikiwa kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa programu ya “Sauti ya Mwanamke Sokoni” kwa Manispaa ya Ilala ambapo wanawake wajasiriamali   wameweza kupaza sauti ya kupinga vitendo vya kinyanyasaji dhidi yao.
 
 
Alisema shirika hilo lilifanya mradi wa miaka mitatu katika manispaa hiyo ambayo sasa imekuwa ya mfano na ndio maana wafanyabiashara wanawake kutoka Lushoto mkoani Tanga wamefika kujifunza ili nao elimu hiyo waipeleke kwa wenzao.
 
Alisema lengo la mafunzo ni kuwapa fursa washiriki hao kuweza kujifunza kutoka kwa wanawake wajasiriamali sokoni katika manispaa ya Ilala masuala mbalimbali ikiwemo mbinu za kufanya ushawishi na utetezi ili kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi katika masoko.
 
Alitaja malengo mengine kuwa ni namna ya kuongeza wanachama wa umoja na vicoba, uendeshaji vikao vya umoja sokoni na namna mfumo wa kuweka na kukopa (Vicoba) unavyoweza kuwasaidia wanawake wajasiriamali kukuza vipato vyao na kuboresha biashara na maisha yao kwa ujumla.
 
Mdendemi alitaja wajasiriamali walionufaika na mafunzo hayo kuwa ni wanawake wanne kutoka wilaya ya Lushoto, Lukozi Lushoto watatu, Chamazi watatu na Temeke Sterio watatu.
Mwenyekiti wa soko la Lukozi kutoka Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Zakati Tendwa alisema mafunzo hayo yamewafumbua macho kwani walikkuwa hawajui chochote kuhusu masuala ya vicoba na kwa niaba ya wenzake amelishukuru shirika la EfG kwa kuwapigania wanawake wajasiriamali masokoni. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Fwd: KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA UWEPO WA SACCOS MAKAZINI

om1Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akimsikiliza Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga (wa pili kulia) akimuelezea mikakati ya ushirika huo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio, akifuatiwa na Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith Medson. om2Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu chake cha uanachama toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu toka kulia). Wengine ni Katibu wa wa ushirika huo  Bw. Benedicto Damiano (wa pili kulia),  Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto)  na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.  om3Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio wakishuhudiwa na  Katibu wa wa ushirika huo  Bw. Benedicto Damiano,  Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto)  Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.  om4Katibu Mkuu  Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo ya matumizi ya kitabu cha uanachama toka kwa  Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia, wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Kati ni Makamu Mwenyekiti wa ushirika huo Bw. Deodatus Gudio.
PICHA NA  IKULU
========================
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amefurahishwa na  uwepo wa vyama vya Ushirika vya Akiba na mikopo (SACCOS) katika taasisi na idara za serikali, akisema kuwa hilo ni jambo la maana kwa kuwa  inatoa fursa kwa watumishi kuwa na kipato cha ziada kitachosaidia kuwaletea ahueni  kwani mishahara pekee  haikidhi matakwa yao yote.
Amesema SACCOS ni
​kama ​
benki ya mtu mnyonge, na kusisitiza kwamba mifuko ya aina hiyo inaposimamiwa vizuri faida yake kwa wanachama ni kubwa sana kwani humpa mtumishi ahueni na kumfanya afanye kazi kwa moyo na  bila wasiwasi ama usongo wa mawazo.
Balozi Sefue ameyasema hayo Jumanne Machi 3, 2015 jioni alipokuwa akiongea na uongozi wa Ikulu SACCOS,
​uli​
omtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es salaam kumkabidhi rasmi kitabu chake cha uanachama kufuatia kujiunga kwake na ushirika huo.
 “Mishahara yetu ndani ya utumishi wa umma haitoshi kukidhi mahitaji yetu yote, kwa hiyo mipango yote hii ya SACCOS, Mfuko wa Rambirambi na Mfuko wa Ushirika
​iliyopo hapa Ikulu ​
inafanya maisha ya mtumishi yawe na ahueni sana na kumfanya afanye kazi kwa moyo.
“Hayo ni mambo ambayo nayaamini sana na nayaunga mkono;  na naamini hata Mhe Rais mwenyewe anayaunga mkono na ndio maana amekuwa mwepesi kujiunga na ushirika ”, amesema Balozi Sefue baada ya kukabidhiwa kitabu namba 2 na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio. Kitabu namba moja amekabidhiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Awali, mshauri Mkuu na Mlezi wa Ushirika huo wa Ikulu, Bw. Joseph Sanga, alimfahamisha Katibu Mkuu Kiongozi kwamba  mifuko ya SACCOS, Ushirika wa Nyumba na  Rambirambi ya  watumishi wa Ikulu iko imara na inaendelea kunufaisha wanachama wake kwa ufanisi.
Bw. Sanga amesema malengo makuu ya mifuko hiyo ni kuleta ustawi kwa watumishi na kwamba wote wanaelewa kuwa mikopo ya SACCOS yao sio kwa ajili ya kununulia chakula ama mavazi bali ni ya kuwekeza kwenye miradi itayowaongezea kipato.
“TUnataka kwenda mbali zaidi kwa kushirikiana na mfuko wetu ya Ushirika wa Nyumba ambo tayari umepeleka maombi ya ardhi kwa wanachama wake ambapo viwanja vikipatikana tuna mategemeo ya kuwapa mikopo kuvununua. Mpango huu una faida kwani ni wa amana kubwa na riba ndogo”, alisema Bw. Sanga alipokuwa anafafanua kuhusu mipango ya Ikulu SACCOS.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ahimiza watumishi wake kuendelea kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao

hab2Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha kawaida ambacho ufanyika kila baada ya miezi mitatuKikao hicho kimefanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Magreth Mtaki. hab3Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel akafafanua jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Magreth Mtaki.
hab4Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bibi. Magreth Mtaki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakifuatilia mada kuhusu bajeti ya Wizara iliyowasilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo Mwanzala Kayoka (hayupo pichani).
hab5Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Mwanzala Kayoka akiwasilisha mada kuhussu uelekeo wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 na 2015/16 wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
hab6Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Liwa akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na hab7Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Bib. Beatrice Sumari akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hab1Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
hab8Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGIA ELIMU

den1
Mkurugenzi wa tigo nyanda za juu kusini, Jackson Kiswaga akikabidhi moja ya bati alizotoa kwa shule mbalimbali za jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa
…………………………………………………………………………..
NA DENIS MLOWE, IRINGA
 
WANANCHI wa jimbo la Kalenga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za harusi na mambo mengine yasiyokuwa na tija katika maendeleo ya jimbo hilo.
 
Hayo yamezungumzwa na mdau wa maendeleo, Jackson Kiswaga wakati akikabidhi mabati 50 na mifuko ya saruji 30 kwa shule ya sekondari ya Nyabula inayomilikiwa na kanisa katoriki parokia ya Nyabula katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa maabara ya Shule hiyo iliyoko katika wilaya ya Iringa vijijini.
 
Kiswaga alisema kuwa urithi pekee kwa watoto ni elimu hivyo ni jukumu la wazazi kuchangia sekta ya elimu kuliko kusubiri serikali ambayo ina mzigo mkubwa kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo katika kukuza uwezo wa wanafunzi katika mambo ya masomo.
 
“Mzazi unaweza kumwachia kijana wako mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo urithi pekee watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu kama ambavyo tunafanya katika sherehe na kumbuka maisha ya sasa bila elimu utasababisha mwanao awe katika maisha magumu hapo mbeleni hivyo tusisubiri serikali tuwe na utamaduni wa kuchangia katika sekta hii ya elimu ndugu zangu,” alisema Kiswaga.
 
Alisema kuwa juhudi za wananchi na mashirika pamoja na serikali zinahitajika ili kuwajengea wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia na ili waweze kufaulu vizuri katika masomo yao hivyo kuchangia maabara itasaidia sana kukuza uwezo wa mwanafunzi katika masomo ya sayansi pindi yakikamilika.
 
Kiswaga aliongeza kuwa sekta ya elimu ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi ambapo inabidi juhudi zaidi ziongezeke kuweza kuifanya elimu kuwa silaha bora itakayowasiadia  vijana kuondokana na umaskini.
 
Naye Padri wa Parokia ya Nyabula Philipo Kindole alimshukuru Kiswaga kwa msaada wa mabati na saruji na kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo kwa maendeleo ya elimu katika mkoa wa

OLOLOSOKWAN WAFURAHIA UJIO WA KIJIJI CHA DIGITALI ENEO LAO

DSC_0003Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.
Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.
Alisema kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.
DSC_0044Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
Aidha alisema kwamba kuna changamoto katika zahanati yao yenye wauguzi wawili huku hospitali ya wilaya ikiwa kiasi cha kilomita 50 hali inayowafanya watu wengi kutegemea mitishamba katika matibabu mbalimbali pamoja na wanawake kusaidiwa uzazi na wakunga wa jadi.
Alisema kuwepo kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kuweza kujisomea kwa kutumia mfumo wa mtandao wa intaneti na hivyo kuwa katika nafasi ya kuelimika vyema kutambua wajibu wao na fursa zilizopo zinazowazunguka kwa kuwa hifadhini.
Aidha kuwepo kwa kiliniki ya mtandao kutaongeza ufanisi wa zahanati iliyopo pamoja na kuipa mkono katika tiba na kuondoa watu kutegemea tiba za asili.
Akizungumzia fursa za kiuchumi alisema ni matarajio yao kwamba kuwepo kwa kijiji hicho na utamaduni wake, kutawezesha kutumia vyema fursa za kitalii ili kukua kiuchumi kwa kujua mipango inayostahili katika kuendeleza utamaduni kwa jicho la kibiashara zaidi.
DSC_0036Mratibu wa shirika la IrikRAMAT Foundation, Salangat Mako akitoa mrejesho wa suluhu za changamoto mbalimbali za kikundi cha uchumi na utamaduni wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya wiki moja.
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Ololosokwan Obeid Laizer ambaye yupo katika kijiji hicho kwa miaka 15 amesema ana matumaini makubwa na mradi huo kwa kuwa mchanyato wake unaonekana kujali zaidi sosholojia za watu na afya zao hasa kwa kuwa na kliniki inayotembea na tiba kwa intaneti itakayomuwezesha kuwasiliana na madaktari wenzake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya afya.
Alisema kwamba kijiji hicho kina magonjwa mengi japokuwa makubwa ni nyumonia, ukosefu wa damu, magonjwa ya zinaa, majereha ya wanyama kutokana na kuchunga mbugani na ugonjwa wa kuhara damu.
Alisema uwapo wa maabara utawasaidia kupata uhakika wa tiba kuliko sasa ambako wanafanya kwa kukisia zaidi.
DSC_0018Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya afya kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman akiwasilisha mrejesho wa kikundi kazi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Naye Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro Beneth Bwikizo amesema kwamba mradi huo utaleta mabadiliko makubwa kwa wanakijiji hapo kutokana na shughuli nyingi za hapo kuhusanishwa na mradi huo.
Alisema mradi huo ambao unaangalia zaidi kukabili utamaduni unaokwamisha maendeleo kwa kutoa elimu na kuiunganisha na dunia nyingine kwa mawasiliano unaonekana utafanya maisha ya wakazi wa hapo kuboreka.
Alisema mradi huo wa kwanza nchini Tanzania na watatu bara la Afrika umempa hamasa kubwa baada ya kuona unaangalia changamoto zilizopo Ololosokwan ambazo ni za miundombinu katika elimu, afya na uchumi na kuzifanyia kazi.
DSC_0051Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro, Beneth Bwikizo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ujumbe wa kijijini cha Ololosokwan uliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC_0054Afisa Miradi msaidizi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko (kushoto) na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay wakinakili yanayojiri wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha kidigital (Unesco – Samsung digital village) katika kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0057Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la IrikRAMAT linalomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maoni yake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi kijiji cha Kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Warsha hiyo ya wiki iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini.
DSC_0066Pichani jii na chini ni wadau mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi waliohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC_0034
DSC_0008Kutoka kushoto ni Mathias Herman wa UNESCO, Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki pamoja na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Madeje.
DSC_0064Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akionesha kwa mifano baadhi ya bidhaa za nje zikivyokuwa na ubora kwenye vifungashio wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha digitali (Unesco-Samsung digital village) kwa wakazi wa kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0118Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisikiliza baadhi ya maboresho ya changamoto zilizojadiliwa na kikundi kazi cha sekta ya elimu na wadau mbalimbali wa elimu.
DSC_0070Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa maboresho ya kazi za vikundi vilivyokuwa vikijadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.
DSC_0070Picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya wiki moja iliyomaziki mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.