TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 18, 2012

ATC YAZINDUA NDEGE YAKE MPYA AINA YA 737-500 KWA SAFARI ZA KILIMANJARO -MWANZA- DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ATC Paul Chizii akikata keki kama ishara ya uzinduzi wa safari rasmi za ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 hapa nchini kutoka Dar es salaam - Arusha-Mwanza- Dar es salaam kila siku kwa shilingi 199,000 ikiwani bei ya promosheni iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wateja wake.
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja viwili tofauti katika uwanja wa ndege wa KIA ambapo wafanyakazi na watu mbalimbali waliilaki ndege hiyo kwa furahi huku kukiwa na vinywaji na vitafunwa na kufuatiwa na sherehe rasmi iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.
Katika picha kulia ni wafanyakazi ndege hiyo Erica kushoto na Doris wakipiga makofi wakati mkurugenzi huyo alipokuwa akikata keki kwa ajili ya uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ATC Paul Chizii akikata utepe wakati akizindua safari za ndege  ya Shirika hilo kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.
 Kutoka kulia ni wadau wa kampuni ya ndege ya ATC Rinah, Neema na Marina wakiwa katika sherehe hiyo jijini Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ATC Paul Chizii akifurahia jambo na mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo Dada Mawanamvua.
 Mkurugenzi wa Fllshangweblog Bw. John Buku,ku akipozi kwa picha na mwandishi wa habari Said wakati ndege hiyo ikielekea jijini Mwanza kutoka KIA.
 Mfanyakazi wa ndege hiyo Erica Mchata akiwajibika kazini.
Baadhi ya abiria waliosafiri na ndege
Abiria wakishuka kwenye ndege  baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Abiria wakishuka kwenye ndege  baada ya kuwasili jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment