TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 18, 2012

TUZO YA MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Jumapili Mei 20, 2012 saa nne asubuhi kitatangaza mdhamini wa Tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011.

Mdhamini huyo atatangazwa kwenye mkutano ambao ataufanya Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto pamoja na mdhamini wa tuzo hizo, ambapo mkutano huo utafanyika kwenye mgahawa mpya uitwao City Sports  &  Lounge uliopo jirani na mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe, Posta Dar es Salaam.
TASWA inachukua fursa hii kuwaalika waandishi wote wa habari za michezo kuhudhuria kwenye mkutano huo ili tuweze kuanza pamoja katika mbio hizi za kuelekea kwenye Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2011.
Tayari Kamati ya Tuzo ishateuliwa na imetangazwa, hivyo baada ya mkutano huo taratibu nyingine zitatangazwa kwa kadri zitakavyokuwa zimekamilishwa na Kamati Maalum ya Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania.
Kwa miaka mitano iliyopita walioshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni  Samson Ramadhani (2006),  Martin Sulle  (2007),  Mary Naali (2008), ambao wote ni wanariadha, wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan.

No comments:

Post a Comment