TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 18, 2012

SERIKALI YAANZA MCHAKATO WA KUANDAA MFUMO WA WASAIDIZI WA SHERIA (PARALEGALS)


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki pamoja na wadau wa   Wasaidizi wa sheria
Naibu Waziri wa katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki kushoto akisalimiana na Bi. Flora Masoy
Na Mohammed Mhina na Martha Komba
 
SERIKALI imeanza mchakato wa uazishwaji wa mfumo wa Wasaidizi wa Sheria (Paralegals) ili waweze kutambulika kwa lengo la kuwawezesha kutoa huduma za kisheria kwa wananchi hasa wa maeneo ya vijijini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki, wakati alipokutana na Wanaharakati wa Kisheria wa Asasi zisizo za Kiserikali ofisini kwake jijini Dar-Es-Salaam.
Mhe. Kairuki amesema kuwa mchakato huo utakapokamilika utawezesha  Wasaidizi wa Sheria kutambuliwa na sheria husika na hivyo kupanua wigo kwa wananchi wa mijini na vijijini kuwa na msaada wa kisheria wanapopatwa na matatizo.
“Natambua umuhimu wa uundwaji wa Sheria hii ya Paralegals ndio maana tumeanza mchakato huu kwa kuufanyia marekebisho na kueleza dhana nzima ya Palalegals,” Alisema.
Amewataka Wanaharakati hao kuendelea kuwasisitiza Wasaidizi wa sheria  kuhakikisha kuwa wanatoa Huduma zao kwa uwazi zaidi ili wananchi waweze kufaidika hiyo. 
Amesema Serikali itahakikisha kuwa inaweka mazingira bora yatakayowawezesha   Wasaidizi wa Sheria kufanya kazi zao vizuri lakini kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Haki za Binadamu.
Wanaharakati hao wamesema kuwa mpaka sasa Wasaidizi wa Sheria (Paralegals) bado hawajatambulika kisheria na kwamba sheria haitoi nafasi kwa Mawakili wa Serikali au wa kujitegemea kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo na Mabaraza ya Kikata maeneo ambayo ndiyo yenye matatizo makubwa ya kisheria kwa wananchi wa kawaida.
Akizungumza kwenye mkutano huo Wakili wa Kujitegemea Bw. Alphonse Katemi amesema wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu mfumo wa kisheria hauruhusu kwa Mawakili kutoa huduma za kisheria katika Mahakama za mwanzo na Mabaraza ya Kata.
“Kwa hiyo ni suala ambalo kwa kweli wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu ni mfumo wa kisheria mawakili kwenye mabaraza haya ya ardhi    hawaruhusiwi,” Alisema Katemi na kuongeza kuwa huko ndiko kwenye maeneo ambayo yanawatesa sana na kuwaumiza wananchi wa nchi hii.

No comments:

Post a Comment