TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 18, 2012

KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni Marekani yaahidi kusaidia kumaliza tatizo la umeme JWTZ Bomoabomoa fukweni iende sambamba na udhibiti hati bandia UWEKEZAJI Tume ya kukusanya maoni ipewe ushirikiano KIKAO Manispaa ya Bukoba na mikakati ya kuendeleza wananchi kiuchumi MKUTANO MICHAICHAI TIC yasifu ushiriki wa UNIDO WAKUNGA Mara yapitisha bajeti 2012/2013 MKUTANONI 'Wakuu wa Wilaya simamieni mfumuko wa bei Dar' MAFUNZO Mradi wa kuzuia maji ya bahari wakwama KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni

  MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:



Posted: 17 May 2012 12:21 AM PDT

Na Salim Nyomolelo

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.

Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.

Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.


"Kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza; "Ndivyo ilivyotokea."

Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.

"Ni Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.

Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani  aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."

Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji  aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.

Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.

Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu  yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."

Kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.

Alisema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.

Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema Bw. Maige.

Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.

Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.

Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga.
Posted: 17 May 2012 12:15 AM PDT
NA MICHAEL SARUNGI

UBALOZI wa Marekani nchini umetaja mikakati mbalimbali ambayo Tanzania inatakiwa kutumia kukabiliana na tatizo sugu la umeme na kuahidi kusaidia eneo hilo.

Mikakati hiyo ilitajwa Dar es Salaam jana katika mkutano uliowakutanisha mawaziri wa Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wa ubalozi wa Marekani ulioongozwa na balozi wa nchi hiyo nchini, Bw.Alfonso Lenhardt.

Bw. Lenhardt katika mkutano huo alisema nchi yake ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha tatizo hilo linakuwa ni jambo la kihistoria.

Alisema Tanzania inahitaji mbinu na mipango kazi ya kufikia malengo ya melenia ya mwaka 2025 inayolenga kuwapatia Watanzania wengi nishati hiyo ya umeme.

"Ndugu wana habari Marekani ipo tayari kuwekeza katika nishati hii na tayari tumewakilisha kwa waziri wenu mipango na mbinu iliyoandaliwa na wataalamu kutoka nchini Marekani kwa lemgo la kusaidia kuliondoa tatizo hili kama si kulimaliza kabisa" alisema Bw. Lenhardt

Alisisitiza kuwa Tanzania ina vyanzo vingi vya umeme ambavyo vikitumika uzalishaji wa nishati hiyo utaongezeka.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, alisema huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuwekeza katika vyanzo vyake vya umeme ili kukabiliana na tatizo hilo.

Alisema mojawapo ya tatizo kubwa inalolikabili Shirika la TANESCO ni uchakavu wa miundombinu hii inayochangia upotevu wa nishati hiyo.
Posted: 17 May 2012 12:14 AM PDT

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali, Kapambala Mgawe, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam juzi, kuhusu hatua za uchunguzi zitakazochukuliwa na jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kufukuzwa na kufikishwa mahakamani kwa askari atakayebainika kujiunga na jeshi kwa kutumia vyeti vya kugushi bila kujali cheo alichonacho hivi sasa, hatua hiyo inafuatia taarifa ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),kubaini udanganyifu kugushi vyeti kwa baadhi ya wanajeshi na polisi.  (Picha na Charles Lucas)
Posted: 17 May 2012 12:08 AM PDT

JUZI Serikali kupitia Wizara  ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilitangaza  imetangaza kwamba nyumba zote zilizojengwa kandokando ya fukwe za bahari na mito zitabomolewa bila wamiliki kulipwa fidia kutokana na kukiuka Sheria za Ardhi na Mazingira za mwaka 1992, 1995 na 2004.

Taarifa hiyo ilitolewa kwa pamoja na mawaziri i katika Wizara hiyo, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, walipozungumza na waandishi wa habari kuelezea migogoro ya ardhi inayotokea nchini na mikakati ya wizara zao kutatua migogoro hiyo.

Prof. Tibaijuka, alisema zoezi la kuwahamisha wakazi waliojenga kandokando ya fukwe za bahari litahusisha mikoa yote iliyopakana na Bahari ya Hindi ambayo ni Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kwa kuzingatia sheria zilizowekwa ambazo zinakataza ujenzi wa nyumba kandokando ya fukwe za bahari ndani ya mita 60 pamoja na mita 30 kandokando ya mto.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, alisema kuwa zoezi la kuwahamisha wakazi waliovamia mito linatarajiwa kuanza hivi karibuni na wataanza na wakazi waliovamia mto Mbezi na Nduwe.

Alisema Setelaiti ya mwaka 2005 inaonyesha mto Ndumbwi ulikuwa unaonekana wazi, lakini sasa wakazi wameuvamia na kujenga kandokando ya mto huo, hata Mto Mbezi Beach pia

Alisema kuwa ukaguzi kwa wakazi waliojenga ndani ya mita 30 kutoka kandokando ya mito utafanyika hivi karibuni sambamba na zoezi la kuwabomolea nyumba zao.

Tunaunga mkono tamko hilo la mawaziri hao kwani ni lazima tufuate sheria zinazokataza kujenga kandokando ya fukwe za bahari, kwani hizo ni sehemu maalum kwa watu wote kuzitumia

Hii ni kutokana na kwamba kwa  kujenga kandokando ya fukwe za bahari na mito ni hatari kwa maisha kutokana na kuwa tumeshuhudia athari zilizotokea pindi tsunami ilipoikumba nchi yetu, pamoja na mafuriko

Hatua hiyo ya wizara ni njema kutokana na kwamba ina lengo la kuzuia majanga yanayoweza kulikabili taifa endapo yatatokea majanga kama ya tsunami na  kupasuka kingo za mito pindi yanapotokea mafuriko.


Hata hivyo pamoja na nia njema ya wizara tunachukua fursa hii kuiomba oparesheni hiyo iende sambamba na udhibiti wa utoaji hati  za kumiliki viwanja kiolela kwani  ndicho chanzo cha kuibuka ujenzi huo.

Tumeshuhudia majengo mengi yakiota kama uyoga katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani fukweni mwa bahari na mito,huku wahusika wakiyafumbia macho .

Tuna imani kama wizara itadhibiti uchakachuaji wa hati za viwanja kwa kiasi kikubwa itasaidia kukomesha tatizo hilo.
Posted: 17 May 2012 12:04 AM PDT

Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu, akionesha ripoti ya Uwekezaji Afrika ya Mwaka 2011, na taarifa ya ufuatiliaji wa hali ya uwekezaji, baada ya kuizindua Dar es Salaam jana, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa  (UNIDO), Bw. Emmanuel Kalenzi,  ripoti hiyo imetayarishwa kwa ushirikiano wa TIC na UNIDO. (Na Mpigapicha Wetu)
Posted: 17 May 2012 12:00 AM PDT

Na Darlin Said

TUME ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba mpya hivi karibuni imeanza kazi tangu ilipoapishwa na Raisi Jakaya Kikwete.

Wakati wanaapishwa raisi Jakaya Kikwete moja ya ahadi  iliyoitoa kuwa bega kwa bega ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na tija na kupatikana kwa maoni ya wananchi ambayo ndio chachu ya katiba itakayojenga Tanzania mpya.

Tume hiyo yenye wajumbe 30 kutoka Tanzania bara na Visiwani tayari imeshakabidhiwa jengo maalum na magari 30 zikiwemo nyumba kwa wale waishio nje ya Dar es salaam.

Kazi kubwa ya Tume hii ni kusimamia mchakato mzima wa mabadiliko ya Katiba ili watanzania waweze kupata katiba mpya ambayo itakidhi na kukata kiu yao.

Majukumu mengine ya tume hiyo ni pamoja na kukusanya maoni, kuyachambua na kuandika rasimu ya katiba ambayo itazaa katiba mpya.

Pia kuhakisha elimu inatolewa  ya kutosha kwa wananchi kuhusu katiba ili wawe na ufahamu na uhuru wa kutoa maoni bila ya kukwazwa kuzuiwa au kutishiwa.

Wakati huohuo Tume imepewa jukumu zito la kuakikisha kwamba wanafanya kazi kwa hali na mali ili kuwatendea haki watanzania na baadaye kufikia hatima ya kile kanachohitajika kwa maslahi ya nchi.

Wakati wanakabidhiwa ofisi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Bi.Celina Kombani alisema tume imepewa kazi nzito isiyohitaji ubaguzi wa aina yeyote ambao inahitaji uaminifu, nguvu, maarifa na uvumilivu.

Hivyo basi italazimika kufanya kazi katika mazingira magumu usiku na mchana kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla

Katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba alivitaka vikundi na wananchi waliopendekeza majina ya wajumbe wa tume  kuiacha huru ifanye kazi iliyopewa.

Hivyo waliopendekeza majina ya wajumbe hawa wasitarajie kuwa wajumbe watafanya watakayo wao kwani tume hiyo ni ya watanzania wote na si watu wachache

Nionavyo, kauli ya Jaji Warioba ya kutaka wawe huru ilikuwa na dhamira nzuri lakini  bado kauli hiyo inachangamoto  kubwa kwani  inaweza kutafasiriwa kuwa tume itapenda iachwe iandike Katiba ya watanzania bila kusukuma na mtu yeyote.

Uundaji wa katiba ni nguzo na ujezi wa muafaka wa kitaifa na hakuna makubalino yanayoweza kupatikana bila msukumo wa wananchi.

Ingawaje tume imetaka iwe huru lazima muwasikilize wananchi kwa kupokea maoni yao bila ya upendeleo wowote ili iweze kutenda haki na kahakikisha watanzania wanashiriki mchakato huo.

Kwa kufanya hivyo mtaweza kuleta katiba mpya ambayo itaijenga Tanzania mpya yenye usawa katika nyanza  zote za kisiasa, kimila na utamaduni, bara na visiwani pamoja na usawa dini.

Tunawaamini na kuwategemea kwani mchakato huu ni muhimu na nyeti kwa mustakabali wa taifa, bila katiba iliyo bora hatuwezi kuijenga Tanzania iliyo safi.

Aidha ili muweze kufahamu watanzania wanahitaji nini lazima mtoe elimu ya kutosha ili waelewe umuhimu  wa wao kushiriki.

Kwa kukafanya hivyo mtawasaidia wananchi kuwa na ufahamu na uhuru wa kutoa maoni bila ya kukwazwa kuzuiwa au kutishiwa.

Kwani Watanzania waliowengi hasa waishio vijijini  bado hawajui katiba nini  na wala  hawajui umuhimu wake kwao, hivyo elimu kwao ni muhimu kabla ya kuomba maoni yao.

Mwenyekiti wa Tume na wajumbe wako muelewe kwamba tume hiyo  ni nguzo ya mchakato wa katiba mpya waipendayo watanzania.

Ndani ya miezi 18  mliyopewa kukamilisha zoezi hilo ni imani ya watanzania muundo wa katiba inayokuja itakuwa imeboreshwa mazuri, imeondoa mapungufu ili kujipima tulikotoka na tuendako.

Naamini  wajumbe wote wa tume wana sifa na uwezo mkubwa kiasi kwamba kama watazingatia misingi mikuu ya uundaji wa Katiba Mpya na ya Kidemokrasia inaweza kufanya kazi hiyo nzuri.

Aidha nawapongeza  na kuwatakia kila la kheri  wajumbe wote waliochaguliwa kulitumikia taifa letu  kwa kusimamia na kuakikisha kuwa Watanzania wanapata katiba mpya ambayo itakidhi mahitaji yao.

Ni rai yangu kwa wananchi kujitokeza na kuwapa ushirikiano watakapohitaji ili kurahisiha mchakato wa kupata katiba mpya kwa maendeleo ya nchi yetu.
Posted: 16 May 2012 11:58 PM PDT
Mwenyekiti wa TPAWU Taifa,Bw. Jaicy Kayera (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Kabangwe Ndebile katika moja ya kikao.
Posted: 16 May 2012 11:50 PM PDT

Na Anneth Kagenda

TATIZO la ajira kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa limeendelea kuwa sugu nchini huku idadi ya watanzania ikifikia milioni 42 hali inayoweza kuwa mbaya zaidi baada ya mika mitano.

Pia, umaskini umeshika kasi Tanzania licha ya kuwa na rasilimali nyingi, ikiwamo ardhi yenye rutuba, bahari, mito na maziwa, madini na wanyamapori.

Ongezeko la watu nchini haliendani na maendeleo ya kiuchumi na kusababisha umaskini hasa kwa vijana kuwa kubwa kuliko jitihada za kulimaliza tatizo hilo.

Kila mwaka vijana 8000 wanaomaliza katika vyuo vya ualimu nchini hupokelewa ajili ya kupewa ajira za ualimu pamoja na kwamba bado hazitoshi.

Utoaji wa ajira hizo ni lengo la serikali ambayo imekuwa ikitaka kumaliza tatizo hilo kwa vijana pamoja na kwamba jitihada hizo bado hazijakidhi mahitaji kwa walengwa.

Kutokana na kuwapo kwa tatizo la ajira nchini na kwa baadhi ya nchi nyingine duniani,  ajira zinazotolewa na serikali huwa hazikidhi mahitaji ya walengwa.

Pia tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa likiongezeka kila mwaka hususan mjini kutokana na vijana wengi kukimbia vijijini kufuata huduma muhimu za jamii.

Wengi wao hukimbilia mijini kwa kudhani kwamba wanaweza kupata ajira kirahisi jambo ambalo sio kweli na badala yake huishia katika makundi ya uhalifu na vijiweni wakipiga debe.

Katika kukabiliana na changamoto hii, serikali haiko peke yake badala yake ina wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambao hawapendi kuona vijana wakizurura na kushinda vijiweni.

Taasisi na wadau hao wamekuwa wakijitahidi kutafuta miradi, kwenye viwanda na maeneo mengine ili vijana wajishughulishe wakati wote pamoja na kwamba jitihada hizo bado zinaendelea kutokana na kwamba mahitaji bado ni makubwa.

Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Antony Amani, anasema, baada ya kuona tatizo hilo limekithiri aliamua kutafuta mbinu kupambana nalo.

Anasema, baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo mwaka 2011 alikumbana na changamoto nyingi na kubwa ambazo alitakiwa kuhakikisha zinapungua kama siyo kuisha kabisa.

"Changamoto ya kwanza niliyokumbana nayo uso kwa uso na ikanishangaza ni ile ya upungufu wa watu wenye hati za kumiliki ardhi ambapo tangu dunia inaumbwa nilikuta idadi ikiwa ni watu 4,881 wenye hati za kumiliki ardhi," anasema Dkt. Amani.

Anasema kuwa, kwa uzoefu wa siku nyingi alionao hakutegemea Manispaa kama hiyo kubwa iwe na hati kidogo kiasi hicho hivyo kujiapiza kwamba suala hilo lazima alivalie njuga.

"Na cha kushangaza zaidi kumbe kuna watu waliowahi kulizwa na wajanja wa mjini ambapo mwaka 2003 waliambiwa kwamba watu 8000 watapewa viwanja kumbe ulikuwa uongo," anasema.

Anaeleza kuwa, mgogoro huo uliodumu kwa miaka 8 huku mapato ya ndani yakiwa ni milioni 9 kwa mwaka.

Anasema kuwa, aliamua kuungana na  watendaji kuingia kwenye mkakati wa kuanza kutafuta fedha kwa lengo la kuanza rasmi kupima viwanja na ambapo jumla ya sh. bilioni 2.9 zilipatikana kutoka Unity Trast Of Tanzania (UTT).

"Fedha hizi zilipatikana na tukaanza kulipa fidia na kupata viwanja, kutengeneza barabara katika maeneo ambayo viwanja vinapimwa ili paweze kufikika kwa haraka," anasema Meya huyo.

Anasema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupima viwanja 5000 ndani ya miaka miwili na kuwakabidhi wananchi hati zao ili wapate mikopo kupitia hati hizo.

Anasema, zoezi hilo linaendelea vizuri na watu wanaendelea kununua viwanja huku barabara zikiendelea kutengenezwa katika maeneo yote ya Manispaa yake kuzunguka mji wa Bukoba.

Anasema kuwa, changamoto nyingini ni ile ya mapato kidogo ambapo alisema kuwa baada ya kuliona hilo alitambua wazi kwamba tatizo linatokana na wawekezaji kuwa wachache hivyo ameanza maongezi  na mashirika mbalimbali pamoja na taasisi.

"Nilizungumza na shirika la Nyumba NHC, PPT na PSPF na kuyashawishi yajenge nyumba ili kuwakopeshe wananchi wote ambao watalipa kwa awamu kadhaa na ndani ya miaka miwili  mambo yatakuwa mazuri," anasema  Dkt. Amani.

Anasema, katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa ajira, amelenga kukuza uchumi kwa wanabukoba ambapo amelenga kuwasaidia wananchi zaidi ya 2000 kupata ajira.

Anasema, atahakikisha anakuza pato la mwananchi wake ambapo amelenga mwananchi apate pato kutoka sh. 400,000 za sasa hadi kufika 650,000 pamoja na kutengeneza vitega uchumi ambavyo vitamsaidia kufikia hapo na kukuza uchumi kwa kasi ikiwa ni pamoja na wananchi kupata ajira.

"Kwa kufanya hivyo hautakuta vijana wangu na wananchi kwa ujumla wanalanda landa bila kazi yoyote na hilo ndilo ninalosema katika ukuzaji wa uchumi na ajira kwa wanabukoba lakini ajira hizi lazima ziwepo kutokana na kwamba zoezi hilo linaweza kwenda ili kupambana na tatizo la ajira ambalo ni changamoto kubwa, kinacholengwa kufanyika hivi sasa ni kuhamishwa kwa stendi ya Bukoba Mjini na kuipeleka eneo la Kyakailabwa.

Anasema, baada ya kupelekwa kwa stendi hiyo vijana watapata ajira kubwa kutokana na mabasi yatakapokuwa yakifika kutoka katika mikoa mbalimbali watatakiwa kuwabeba kwa kutumia usafiri wa aina mbalimbali wasafiri wanaorudi na kwenda kwenye safari zao.

Anaongeza kuwa katika stendi ya Kyakailabwa biashara nyingi zitakuwa zikifanyika na vijana wengi wataweza kujiajiri kupita kitegauchumi hicho kuliko kuendelea kukaa bila kazi kama hali ilivyo sasa.

Anasema kuwa vile vile katika soko la Kyakailabwa wanategemea kujenga shoplaite kubwa, mzuri na ya kisasa ambayo itatumiwa na wananchi pamoja na Jeshi.

"Jengo litakalojengwa ilipo stendi litakuwa ni kubwa, zuri na litakuwa na vitengo tofauti tofauti vya kufanyia shughuli za uzalishaji lakini pia litatoa hata ajira kwa vijana kwani lazima wasomi na vijana wengine wajishughulishe humo," anasema.

Kwa upande wa elimu anasema kuwa Manispaa imeanzisha Chuo cha Ualimu hivyo vijana wengi wataweza kujiunga katika chuo hicho na siyo kuangaika huko na kule.

"Pia tuna Tawi la Tumaini ambalo tunategemea lianze Septemba, 2012 lakini pia kwa upande wa shule za manispaa hatuna tatizo lolote kwani tumepata ufaulu wa asilimia 83 huku tukiwa na vyumba vya madarasa kwa asilimia 100 hivyo hatuna upungufu wowote" anasema.

"Mimi nimetembea nchi nyingi na nimeona majengo makubwa na mazuri hivyo tunampango wa kujenga soko ambalo ni la kisasa na la kimataifa ambalo kwa hapa Tanzania halipo," anasema Dkt.Amani.

Anatoa wito kwa wazawa wa Mkoa huo kutoukimbia mji huo na kuwataka wafike kwa ajili ya kuwekeza, kujua maendeleo ya mkoa wao.

"Lakini pia si tu wazawa bali tunawakaribisha hata watu wengine kwa ajili ya kuja kuangalia maendeleo yetu hata wale wa nchi jirani kwani kutoka bukoba hadi huko ni kilometa 290 wakati ni karibu sana kutoa bukoba hadi Kigali hivyo waje," .
Posted: 16 May 2012 11:49 PM PDT
Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Dkt.Antony Amani, akichangia mada kwenye moja ya mikutano ya maendeleo.
Posted: 16 May 2012 11:38 PM PDT



Mfanyabiashara ya miche ya michaichai akimshawishi mteja aliyeko ndani ya gari kununua miche hiyo, kama alivyokutwa makutano ya Barabara za Nyerere na Lugoda, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
Posted: 16 May 2012 11:34 PM PDT

Na Nyakasagani Masenza

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesifia ushirikiano mkubwa kinaoupata kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) katika kuhamasisha uwekezaji nchini.

Pongezi hizo zilitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Raymond Mbilinyi, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya taasisi hizo mbili za uwekezaji Afrika 2011 na taarifa ya ufuatiliaji wa hali ya uwekezaji iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

"Uhusiano kati ya TIC na UNIDO ni wa muda mrefu tangu mwaka 2000, tunatarajia kuwa tutaendelea hivyo ili kuhamasisha uwekezaji endelevu hapa nchini," alisema Bw. Mbilinyi.

Alisema kwa msaada wa UNIDO, umewezesha kituo hicho kuhakiki miradi iliyosajiliwa na TIC na kuthibitisha kwamba karibu asilimia 80 ya miradi hiyo inafanya kazi.

Aliongeza kuwa kupitia UNIDO, kituo hicho kiliweza kuendesha mafunzo ya kuendeleza biashara nchi nzima na kusaidia kuendeleza miradi 400 ambapo miradi 80 ilichaguliwa na kuendelezwa zaidi na kuifanya iweze kukopesheka, kutafutiwa masoko na kuunganishwa na wadau wengine ndani na nje ya nchi.

"UNIDO imeendelea kuisaidia TIC katika kujenga uwezo wa wafanyakazi wake hadi sasa," alisema.

Kwa upande wake, mwakilishi wa UNIDO  nchini, Bw. Emmanuel Kalenzi, alitoa shukrani zake kwa kwa TIC kwa kuongoza taasisi nyingine kwa niaba ya serikali katika utafiti huo wa masuala ya uwekezaji.

Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu, alisema ingawa Tanzania imeweza kuvutia mitaji ya uwekezaji toka ndani na nje ya nchi, bado haijaweza kufahamika hasa ni miradi mingapi inafanya kazi vizuri na ni thamani kiasi gani imeingiza kwenye uchumi.
Posted: 16 May 2012 11:33 PM PDT

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akimsikiliza Mkururugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Utafiti na Tiba Afrika (AMREF), Bi. Wanjiru Ruhanga, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya miaka mitatu ya Kuchangia Mafunzo ya Wakunga Nchini, Dar es Salaama juzi, utakaoratibiwa na shirika hilo ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. (Picha na Charl;es Lucas)
Posted: 16 May 2012 11:29 PM PDT

Na Thomas Dominick
Musoma

MAKADIRIO ya Rasimu ya bajeti ya Mkoa wa Mara kwa kipindi cha mwaka wa fedha
2012/2013,kwani mkoa umeomba kuidhinishiwa zaidi  ya shilingi bilioni 163 sawa na ongezeko la asilimia 22.5 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2011/2012.

Akisoma makadirio ya bajeti hiyo Katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa
Mkoa (RCC) Ofisa Mipango wa Mkoa huo, Bw. Nesphory Bwana alisema kuwa
sehemu kubwa ya ongezeko la bajeti hiyo ni mishahara iliyoongezeka kwa
asilimia 44.7. ongezeko hilo la mishahara limetokana na muundo mpya wa
sekretarieti ya mkoa na halmashauri ambapo jumla ya watumishi 152
wataajiriwa na sekretarieti ya mkoa na watumishi 2,607 wataajiriwa na
katika halmashauri za wilaya.

Alisema sh.bilioni 103.456 ni kwa ajili ya mishahara, bilioni 18.238 kwa ajili ya
matumizi mengineyo, bilioni 31.324 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na
bilioni 10.443 ni makusanyo ya vyanzo vya ndani

“Pamoja na maombi hayo hapo juu, Mkoa wa Mara unaomba kiasi cha
bilioni 22.573 kama maombi maalumu kwa ajili ya kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo kwa Sekretarieti ya mkoa na halmashauri
zake,”alisema Bw. Bwana.

Alisema kuwa bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vya wananchi toka
katika ngazi za msingi yaani vijiji, mitaa na kata ushauri toka katika
wizara mama ya OWM- TAMISEMI na wizara za kisekta, wizara ya Fedha,
Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Mabaraza ya Madiwani na kamati za kudumu
halmashauri.

Pia alisema kuwa imezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau
mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara, wenye viwanda, sekta ya kilimo,
utalii na wengine wengi.

Awali akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa huo Bw. John Tuppa aliwaomba
wajumbe na kujadili kwa kina na kutoa maamuzi sahihi yatakayosaidia
mkoa huo na kupewa baraka na wajumbe hao.

“Ukomo wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13 tuliopewa Serikali ni sh.
bilioni 163 ambao ni ongezeko la bilioni 32 ya bajeti ya mwaka jana,
ambapo ongezeko hilo lipo kwenye mishahara, matumizi ya kawaida
imepungua kwa asilimia 40 ambapo katika utendaji kutakuwa na kazi
kweli,”alisema Bw.Tuppa.

Alisema kuwa makusanyo ya ndani ndiyo yatakayookoa mkoa kwani  alidai kuwa hii inatokana na fedha za uendeshaji na maendeleo kuwa ndogo.
Posted: 16 May 2012 11:28 PM PDT
Katibu Mkuu wa Chama kipya cha siasa nchiniAlliance For Democratic Change (ADC) Bw. Lucas Kadawi Limbu, akipokea kadi kutoka kwa kundi la wasanii wa Magu One Theatre na kuwakabidhi kadi mpya za ADC mjini Magu hivi karibuni baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mkoani Mwanza. Picha na David Magesa
Posted: 16 May 2012 11:20 PM PDT

Na Heri Shaaban
Dar es Salaam

WAKUU wa Wilaya za Dar es Salaam wameagizwa kusimamie mfumuko wa bei ya vyakula katika masoko ya wilaya zao.

Agizo hilo limotolewa na Mkuu wa mkoa huo Bw.Meck Sadik mara baada kuwapisha wakuu wa wilaya zake.

Bw.Sadik alisema  kuwa kutokana na mfumuko wa bei katika bidhaa,anawagiza kutoa kipaumbe  kushughulikia suala hilo kwa kufanya  ziara katika masoko na kuangalia  bei ya vyakula.

Alisema kuwa katika masoko ya mkoa huo bei ya unga sembe kilo moja inauzwa shilingi 1200 hadi 1400 jambo ambalo wananchi wengi wanashindwa kumudu ukali wa gharama za maisha  na kulazimika kula mlo mmoja kwa siku.

"Serikali  imeshasambaza mahindi mengi kutoka katika  Ghala la Serikali  kwa kuwapa wafanyabiashara wakubwa kama Bakhresa  hivyo kwa sasa unga wa sembe utauzwa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo,"alisema Bw. Sadik.

Aliwataka wakuu wa wilaya hizo wawe na utaratibu ya kutembelea  masoko na kuangalia bei za bidha zinazopanda mara kwa mara.

Alisema  wafanyabiashara wote watakaouza unga sembe kwa bei kubwa badala ya bei ya serikali watachukuliwa hatua huku leseni zao zikikamatwa.
Posted: 16 May 2012 11:18 PM PDT
Mwanafunzi akitambaa juu ya kamba wakati wa mashindano ya skauti, mafunzo haya huwasaidia vijana kuwa wazalendo na nchi yao na wapenda amani.( Picha na mtandao)
Posted: 16 May 2012 11:10 PM PDT

Na Mwajuma Juma,
Zanzibar

MRADI wa kuzuia maji ya baharini ili yasiingie katika makaazi ya
wananchi umeshindwa kutekelezeka baada ya fedha zilizoombwa
kukamilisha mradi huo kutowafikia walengwa.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi  jimbo la Kikwajuni Bw. Mahmoud Mohammed
Mussa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia
ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa wakati alipofanya ziara kwenye
maeneo ya Binguni na Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Bw. Mussa alisema kuwa kabla ya kuanzishwa mradi huo wananchi
waliiomba jumla ya shilingi milioni 780 Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lengo la kutekeleza mradi huo.
Hata hivyo alisema kuwa ofisi hiyo ilituma shilingi milioni 531 lakini
hazijuulikani wapi zilipofikia na kuwa zinatarajiwa kuundiwa mradi
mwingine jambo ambalo wananchi hawakubaliani nalo.
“Kimsingi mradi umeshindwa kutekelezeka na tunachohoji wapi fedha hizo
zimekwenda,” alisema Mwakilishi huyo.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo uvumi huo kinachotakiwa kujuulikana
fedha hizo zimetumwa wapi ili wananchi hao waweze kuendeleza azma yao.
Tunajua fedha zimetumwa lakini wapi hatujui na kama zipo ni kwanini
utafutwe mradi mwingine wakati walioomba ni wananchi wa jimbo la
Kikwajuni hii kwa kweli sio sawa,” alisema.

Hata hivyo akizungumza mbele ya kamati hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Mazingira Bi. Sihaba Haji Vuai alisema kwamba kiasi hicho cha fedha
kinasubiriwa ili kutengeneza maeneo ya malindi ambayo kuna njia
imekatika.

No comments:

Post a Comment