TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, May 19, 2012

NHIF YAWAPIGA MSASA WAHARIRI WA WASANIFU WA MAGAZETI KUHUSU MFUKO BIMA WA AFYA

 Naibu Mkurugenzi wa Mkuu waMfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee akifungua mafunzo ya Wahariri Wasanifu wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini, kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Dar es Salaam asubuhi hii. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tathmini na Uhai wa Mfuko na Takwimu, Michael Mhando (kushoto) na Mwenyekiti wa Umoja wa Wahariri Wasanifu, Laudeni Mwambona.
 
Mafunzo hayo yataendeshwa kwa siku moja na yanafanyika katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki Kurasini jijini Dar es salaam Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wahariri Wasanifu, Laudeni Mwambona (kulia), akizungumza wakati wa mafunzo hayo, katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Mkuu waMfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee na Kushoto ni Mkurugenzi wa Tathmini na Uhai wa Mfuko na Takwimu, Michael Mhando
 Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani (kulia) akiwa na Ofisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NHIF/CHF, Grace Michael.
 Mwana vipindi vya afya wa Chanel Ten, Lina Denis (kushoto) akitoa shukrani kwa NHIF, kuandaa mafunzo hayo muhimu kwa wahariri wasanifu. Kutoka kulia ni Beda Msimbe wa Habari Leo na Martha Ngwira wa TBC.
      Baadhi ya maofisa wa NHIF,CHF wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mafunzo hayo.
Sehemu ya Wahari Wasanifu wakiwa katika mafunzo hayo.Kutoka kulia ni Noor Shija wa gazeti la Uhuru, Jane Mathias wa Nipashe na Boniface Luhanga wa Nipashe.
Wahariri wasanifu wakiwa katika warsha hiyo kutoka kushoto ni  Lina Denis wa Chanel Ten, Martha Ngwira wa TBC na   Beda Msimbe wa Habari Leo.
 Hapa wakielekea kupiga picha.
Naibu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khimis Mdee (katikati mbele) na viongozi wengine wa mfuko huo, wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri Wasanifu.

No comments:

Post a Comment