TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 24, 2014

ASHABIKI SIMBA WATULIZWA JAZIBA, LOGA KUSUKA KIKOSI KAZI KUWAVAA AZAM , KAGERA SUGAR, ASHANTI, YANGA MECHI ZILIZOSALIA!!

Na Baraka Mpenja 

IMG_2166
KIPIGO cha bao 1-0 walichopokea Simba sc kutoka kwa Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga  jana  uwanja wa Taifa  katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kimezidi kuwavuruga  na kuwafanya wawe wanyonge  ngwe hii ya lala salama.
Wagosi wa Kaya wakiwa katika morali ya ushindi , waliandika bao la ushindi dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa mlinzi wake wa pembeni, Hamadi Juma kufuatia mabeki wa Simba kujikoroga.
Matokeo hayo yamepokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaona kama ligi kuu inawaonea msimu huu.
Hata hivyo Uongozi wa Simba sc kupitia kwa Afisa habari wake, Asha Muhaji umewataka mashabiki na wanachama wao kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao.
“Matokeo ya jana hatukuyatarajia hata kidogo. Tumeshitushwa mno na kipigo hicho. Lakini hayo ndio mambo ya uwanjani. Mpira umechezwa vizuri na tumepoteza. Hatuna budi kuukubali ukweli japo unauma”. Alisema Asha.
Mwamuzi vipi?: Kocha wa Simba sc, Dravko Logarusic (wa kwanza kulia) akiwa hailewi cha kufanya na kuonesha kuwa muda bado wakati mwamuzi anapuliza kipenga cha mwishoIMG_2041Shughuli ilikuwa pevu mno jana uwanja wa Taifa
Afisa habari huyo aliongeza kuwa kutokana na matokeo wanayozidi kuyapata, yanawapa watu cha kusema, lakini soka huwa lina tabia ya kupanda na kushuka.
“Siku za nyuma mashabiki wetu walikuwa wanatoka na furaha uwanjani. Kwa sasa mambo yamebadilika. Huo ndio Mpira, ukiupenda lazima uwe  na moyo wa kukubaliana na kile kinachotokeo”. Alisema Asha.
Asha alisisitiza kuwa bado wamebakiwa na mechi nne, hivyo mashabiki waendelee kuiunga mkono klabu yao ili iweze kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment