TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

MAMLAKA YA HALI YA HEWA ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA MAMLAKA HIYO DUNIANI INAYOADHIMISHWA KILA MWAKA IFIKAPO MARCH 23

Mtaalamu wa Hali ya Hewa Bw. Hassan Khatib Ame akitoa ufafanuzi wa kitu kwa wanafunzi wa Skuli ya Kombeni walipotembelea Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa iliopo ndani ya Uwanja wa ndege wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyo adhimishwa leo.DSC_0697Afisa Usalama wa Anga Bw. Rashid Omar Mselem akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani kuhusiana na usalama wa Anga na Hali ya Hewa pindi inapokuwa mbaya, katika kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani.
………………………………..
Na Miza Kona   – Maelezo Zanzibar              
Wanafunzi wa vyuo na sekondari wameitaka jamii kuwa na mwamko wa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa pamoja na kutembelea vituo hivyo ili kuweza kujua na kupata taarifa za mwenendo wa hali ya hewa Nchini.
Kauli hiyo wameitoa leo huko katika ofisi za Mamlaka hiyo ziliopo Uwanja wa Ndege Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani, wamesema jamii imekuwa haina mwamko mzuri katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa nchini.
Wamesema kuwa kila siku jamii inatakiwa kujua na kufuatilia taarifa hizo ili kuweza kufahamu hali ya hewa ilivyo ili kuepukana na majanga na matatizo yanaweza kutokea ambapo mamlaka hiyo hutoa taarifa.
Aidha wanafunzi hao wamewataka wanafuzi wenzao kutembelea katika vituo vya Mamlaka hiyo kwenda kusoma kwa vitendo na kuona shughuli hizo zinavyotolewa.
Wanafunzi hao wametembelea sehemu mbali mbali na kuona jinsi shuguli za kituo hicho zinavyofanyika ikiwepo sehemu ya usalama wa Anga, kipima joto, kipima mvua, kipima upepo, pamoja  utabiri wa hali ya hewa.
Wakitoa maelezo kwa wanafunzi maafisa mbali mbali wa Mamlaka hiyo wamesema kuwa huduma nyingi zinazoendeshwa nchini huwa zinashirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa taarifa za hali ya hewa ili kuendesha kazi zake.
Wamefahamisha Mamlaka ya Hali ya Hewa hushirkiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege jinsi ya kuingia kutoka kwa ndege nchini na namna ya kuwasiliana katika uendeshaji shughuli wa zake.
Aidha wamefahamisha kuwa Mamlaka hutoa taarifa zake kwa kutumia vipimo mbali mbali viliopo nchini vikiwemo kipima ju, kipima upepo pamoja na kipima mvua na kutoa taarifa jamii jinsi ya hali ya hewa ilivo na itakavyokuwa nchini.    
Nae  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mohammed Khamis Ngwali , amesema vijana wanatakiwa kubadilika na kuchukua tahadhari za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kizazi kijacho kiweze kufaidi dunia yenye mazingira bora.
Hata hivyo  Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana katika kujihisha na  masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa na hatua za kuchukua katika kipindi cha hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Amesema hatua hii muhimu ikichukuliwa na vijana italeta ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho kwa kujenga jamii iliyo imara baadae pamoja na kuokoa dunia  kwenye majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini.
 Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 23 Machi, kauli mbiu ya mwaka huu ni ushirikishwaji wa vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment