TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

SOKA LINA MAAJABU YAKE, INAWEZEKANA MAN UNITED KUWANYUKA BAYAYER NA KUTINGA NUSU FAINALI UEFA!!

Wakati uso wasaa ya dunia unaenda kasi sana, huku nao wana sayansi wakiumiza kichwa kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea, nayo Brazili ikiwa na maombolezo ya nahodha wake  aliyewaisaidia kutwaa kombe la dunia pale Sweeden  1950 , wakati huo huo sherehe ya mzee Arsene wenger kutimiza mechi 1000 zikishereheshwa kwa kipgo kibaya cha goli 6-0 kutoka kwa Chalsea, bado uso wa saa wa dunia ukasema kwa nini Manchester United wakiwa mabingwa wa EPL wasistahili kukutana na bingwa mwingine wa Bundesliga ,Bayern Munchen.  The Bavarians.
 Luis Figo,  nguli wa zamanI wa Barcelona , Real Madrid na Ureno huenda ameingia kwenye orodha ya watu ambao pengine wanachukiwa na mashabiki wa Man u, hiii ni kutokana na Droo ya robo fainali ambayo Figo alikuwa balozi wake .
Bayern-Munich-Champions-League-Winners-2013-HD-WallpaperKweli Man United ataweza kuwatafuna wanaume hawa?
Katika droo hiyo,  klabu ya Manchester United imepangwa kucheza na bingwa mtetezi  wa kombe hilo Buyern Munich, huku wenzao Chelsea wakipangwa dhidi ya Paris saint Germain ya nchini ufarasa.
Lakini tukio lililoshika hisia za watu wengi, na kuchafua mapumziko ya mwisho ya wiki kwa mashabiki ni hili la  Mancheste united.
 Mashabiki  wengi kama sio wote, wakurugenzi, hata jopo la ufundi la Man United, na hata wachambuzi na waandishi mbali mbali wa habari za michezo wasingetamani  Mashetani wekundu  kwa hali waliyo nayo  kukutana na  Bayern ya Pep Guardiola. 
article-2585919-1C6E2CCB00000578-572_634x461
Wamevurugwa: Wayne Rooney na  Manchester United watautafuna mfupa wa Bayern Munich?
Si  kwamba timu hizi ndio zinakutana kwa mara ya kwanza, la hasha..! kwa mujibu wa vyanzo vya habari,   timu hizi zimekutana takribani mara 9.
 Manchester United imefanikiwa kushinda mara 2, kutoka sare mara  4 na kufungwa mara 3,  huku tukio linalokumbukwa na watu wengi na linalowapa matumaini si mashabiki hata wachezaji wa sasa wa Man United na viongozi wao, ni hili la mwaka 1999 katika fainali hizo ambapo Manchester ikiwa chini ya koch Sir Alex Ferguson ilishinda na kutwaa taji hilo.

No comments:

Post a Comment