TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

WANAFUNZI WASHAURIWA KUJENGA MAHUSIANO YA URAFIKI NA WENZAO!!

Mtembeza wageni wa Kanisa la Mkunazini akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kutoka Dar es salam walipokuwa wakitembelea Kanisa hilo.DSC_0572Wanafunzi wakipata maelezo kwa Mtembeza wageni juu sehemu walipokuwa wakihifadhiwa watumwa Kanisani hapo.DSC_0602Hapa wanafunzi wakijichagulia katika moja ya maduka ya vinyago na nguo za Kiswahili yaliopo Ngome kongwe Mjini Unguja.DSC_0612Wanafunzi wakionyeshana Spices.DSC_0630Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid akiwaonyesha mmoja wa mmea wa Spice na kuwafahamisha matumizi yake, mmea huo unaotambuliwa kwa jina la mchaichai katika chamba hilo.
…………………………………………………………………………………………….
Na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.
VYUO mbalimbali nchini, vimeshauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki kati yao ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa msafara wa wanafunzi 70 kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Dar es Salaam, Dawson Kyungai, wakati wakiwa katika ziara kuwatembelea viongozi wenzao wa Chuo cha Elimu Zanzibar (Zanzibar Education College).
Kyungai ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa ujasiri wao wa kutafuta njia za kujenga mahusiano na vyuo mbalimbali nchini.
Naye Mkuu wa Zanzibar Education College Ussi Said Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika Kanisa la Mkunazini walikotembelea, alisema suala la urafiki wa vyuo linawasaidia walimu na wanafunzi kubadilishana mawazo na kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Wanafunzi hao 70 wako katika ziara ya siku tatu kuwatembelea wenzao wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kuzuru sehemu mbalimbali za kihistoria za Zanzibar.
Kwa upande wao, wanafunzi na walimu wa Zanzibar Education College, wanatarajia kufanya ziara kama hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment