TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

WANANCHI KATAVI WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA

Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhusu hali ya upatikanaji wa maji kwenye halmashauri hiyo wakati wakiwa kwenye moja ya kisima kinachotumika kusukuma maji kupeleka kwenye tanki la maji kasha kusambazwa katika maeneo mengine kijijini hapo
???????????????????????????????Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi,  Kanali Ngemela Lubinga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhiwa lita 90,000 za maji na litaweza kuhudumia wakazi wapatao 2000 katika kijiji hicho cha Isinde siku ya kilele cha wiki ya maji .viongozi wa mkoa huo.
Na Kibada Kibada Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewahimiza wananchi  wa Mkoa huo kutunza  mazingira  na kutoharibu vyanzo vya maji kwani kutofanya hivyo kunaleta madhara makubwa katika maisha ya kila siku.
 Akiongea na wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha maji Mkoa yaliyofanyika kwenye kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda,  Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu amesema wananchi wanatakiwa kutunza mazingira na  kuhifadhi vyanzo vya maji ili  viweze kuwa endelevu.
 Katika hotuba yake  hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya huyo,  imeeleza changamoto hizo  za uharibifu wa mazingirazi zinazoukabili  Mkoa wa Katavi kuwa ni uhamiaji holela wa wananchi kutoka mikoa ya Kigoma, Mwanza,Tabora,Simiyu na Shinyanga ambapo humami a na  kuchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu  kwenye vyanzo vya maji na mazingira
Aidha amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili kutunza na kuendeleza miradi ya maji waliyojengewa na serikali ili iweze kuwanufaisha wananchi wa Mkoa huo kwa kuwaondolea matatizo ya upungufu wa maji uliokuwa ukiwakabili.
Katika hatua nyingine amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili fedha inayopatikana isaidie kuendeleza ukarabati unaoweza kijitokeza iwapo kutakuwa na uharibifu wowote kwenye mradi wa maji kwa kuwa miradi ya maji ni mali yao.
Awali Kaimu  Mhandisi wa Maji  Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi  katika taarifa yake ya ujenzi wa tanki  la maji alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 200 zimetumika katika  ujenzi wa  tanki la maji lenye uwezo wa  kuchukua ujazo wa  lita  90,000 (90m).
 Msengi ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuwaondolea kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili  wananchi wa Kijiji cha Isinde  kwa muda mrefu.
Naye Mhandisi wa Maji Mkoa wa Katavi,  Elieda Mwakasungura katika Taarifa yake ya Mkoa wa kuhusu maji alieleza kuwa wananchi wanaopata maji  safi na salama katika mkoan huo ni asilimia 48 hali ambayo inaonesha bado lipo tatizo la upatikaji wa maji safi na salama katika mkoa huo.
Miradi mingine inaendelea kutekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda katika kijiji cha Ikola,Ngomalusambo na Karema,miradi mingine inatekelezwa katika Halmashauri ya Nsimbo.

No comments:

Post a Comment