TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

MBEYA CITY: HAKUNA DHAMBI KUBWA KAMA KUKATA TAMAA, KWA UZURI GANI, MAFANIKIO GANI UNAJIHANGAISHA NA VIDUKU?

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
HAKUNA dhambi kubwa kama kukata tamaa katika maisha. Inafahamika kuwa kuna changamoto nyingi zinazoweza kumkabili mtu na mwisho wa siku akajiona hawezi kufanikiwa tena.Kumbe njia sahihi ni kukubali changamoto iliyopo mbele yako na kutafuta njia ya kukabiliana nayo.Mafanikio si jambo la siku moja, zipo njia za kupita ili kufanikisha malengo yako.
Msimu huu wa 2013/2014  wa ligi kuu soka Tanzania bara kumekuwepo na ushindani mkubwa kuwania ubingwa.Nafasi za juu kuna timu moja mpya kabisa ambayo ni Mbeya City. Msimu wa mwaka juzi, Simba sc klabu walikuwa wanachuana vikali na Azam fc kuwania ubingwa, huku Yanga akiwa nyuma yao akijikongoja.
Mwisho wa msimu, Simba waliibuka vidume baada ya kutwaa ndoo na kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambako walijitahidi kucheza kwa nguvu zote, lakini walitolewa.
Msimu wa mwaka jana, Simba naye akaa pembeni na kuwapisha Azam fc wakichuano  vikali kuwania ubingwa. Mwisho wa siku, Yanga wakaibuka wanaume na kuiwakilisha Tanzania mwaka huu ligi ya mabingwa barani Afrika.Yanga hawajaweza kusonga mbele baada ya kukutana na kigongo cha Al Ahly ya Misri katika safari yao.
Japokuwa walitolewa kwa mikwaju ya penati 4-3 machi 9 mwaka huu nchini Misri, Yanga walipambana sana na kuonesha kukomaa zaidi.Kwa mara nyingine msimu huu  kigogo wa soka la Tanzania, Simba sc hazungumzwi katika mbio za ubingwa.
Watu wanawazungumzia Mbeya City, Yanga na Azam fc waliopo nafasi za juu.Ukiangalia katika misimu mitatu iliyopita, utagundua Yanga na Simba wamekuwa wakibadilika badilika, mara wana makali ya kutosha mara wanalowa.
Azam fc wanaonekana misimu yote ni washindani na ndio maana wamejaribu kutwaa ubingwa kwa misimu yote tangu wapande ligi kuu 2008/2009.Wamekuwa wakiishia nafasi ya pili mara kwa mara. Hii inatoa picha kuwa Azam fc wanaanzia pale wanapoishia.
Katika maisha ya kawaida, kama mwaka huu umepata alama B, basi mwaka ujao unatakiwa kuanzia B kuelekea alama A.Kama utapata alama C na mwaka jana ulipata B, basi ujue hauna mipango mizuri ya kuendeleza mafanikio yako.

No comments:

Post a Comment