TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

MALOPE KUFUNIKA TAMASHA MWANZA!!

NA MWANDISHI WETU
 BAADA ya kuweka historia  katika Tamasha la Pasaka la mwaka 2012, malkia wa muziki wa injili wa Afrika Kusini, Rebecca Malope anatarajia kuuinua umati wa mashabiki wa muziki huo, jijini la Mwanza Aprili 4 mwaka huu.
Nguli huyo wa Injili anayekubalika Afrika na bara la Ulaya anatarajia mwaka huu kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka katika mkoa huo ambapo kamati ya maaandalizi imeshakamilisha taratibu zote za kumleta mwimbaji huyo.
Kurejea mara ya pili  katika tamasha hilo inaonesha jinsi anavyokubalika, Malope ambaye alianza muziki wa injili akiwa na umri wa miaka 18, kipaji chake cha uimbaji kimekubalika Tanzania na yeye kuipenda nchi hii na kuja kuwapa raha ya neno la Mungu kupitia nyimbo zake.
Imezoeleka kuwa waimbaji kutoka nchi hiyo, wamekuwa waakiishia katika jiji la Dar es Salaam, ambapo kamati ya maandalizi inayoongozwa na mwenyekiti wake, Alex Msama iliona umuhimu wa waimbaji kutoka nje kufika katika mikoa mingine ambako wameanza na mkoa wa Mwanza ambao Malope anatarajia kufanya mambo makubwa.
Ni nafasi ya pekee kwa wakazi wa jiji la Mwanza ya kupata fursa ya kusikiliza neno la mungu kupitia nyimbo za mwimbaji huyo nguli, hivyo wajitokeze kwa wingi kupata jumbe nzuri za neno la Mungu kupitia kwa Malope na waimbaji wengine kutoka sehemu mbalimbali.
Rebecca Malope ambaye ni kipenzi cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na rais wa sasa Jacob Zuma, amepitia tabu na changamoto nyingi katika maisha yake na amekuwa mwimbaji wa kimataifa na amefanikiwa kufanya maonyesho takribani nchi nyingi za Ulaya na Afrika kwa ujumla.Historia ya Rebecca Malope
Mwimbaji huyo mkongwe alizaliwa 1968 katika kijiji cha Lekazi karibu na mji wa Nelsprut, Mpumalanga nchini Afrika kusini. 
Historia ya mwimbaji huyu nguli wa muziki wa injili ambayo si nzuri kimaisha ambapo Malope hakuendelea katika elimu na ni mambo machache yanayofahamika kuhusiana na enzi za utoto wake. 
Akiwa na umri mdogo Malope alipata ugonjwa uliopelekea kutoweza kutembea na madaktari walidhani asingeweza kutembea tena katika maisha yake. 
Familia yake ilikuwa masikini kwa kiasi kikubwa na ndipo yeye na dada yake Cynthia waliamua kukimbilia katika jiji la Johannesburg kitongoji cha Evaton kwa ajili ya kutafuta kazi kwa ajili ya kujikimu na maisha. 
Mwaka 1986 Malope akiwa na miaka 21 alishiriki kwenye mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji yaliyojulikana kama ‘Shell Road to Fame’ lakini hakufanikiwa kufika mbali. 
Malope hakukata tamaa ndipo mwaka uliofuata alishiriki tena na kuibuka mshindi na wimbo wa ‘Shine on’ ushindi huo ulimsogeza mbali zaidi kimuziki na ndipo alipokutanishwa na muandaaji mashuhuri Sizwe Zako na akapata meneja wake wa kwanza akijulikana kwa jina la Peter Tladi. 
Albamu yake ya kwanza ilikuwa na nyimbo za kidunia, albamu hiyo ambayo haikufanya vizuri sokoni na ndipo alipoamua kujiingiza moja kwa moja kwenye muziki wa injili. 
Alipata ushirikiano mkubwa kutoka redio mbalimbali kwa nyimbo zake za injili kitu ambacho hakikuwa kawaida Afrika Kusini. 
Mwaka 1990 Rebecca alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike wa Afrika Kusini na mwaka 1993 ilikadiriwa watu zaidi ya milioni moja walimpigia kura kama mwanamuziki bora wa kike kwenye Coca Cola Full Blast Music Award Music Show na alishinda kwa mwaka huo na 1994 pia. Kwenye mauzo, Album zake zote kumi za kwanza ziliingia kwenye hadhi ya dhahabu. 
Katika kipindi chote nakala zaidi ya milioni 2 zilikuwa zimeshauzwa sokoni. Mwaka 1995 kwenye CD yake ya ‘Shwele Baba’ nakala zaidi ya milioni moja ziliuzwa ndani ya wiki tatu toka uzinduzi wake na hii iliweka rekodi ya aina yake katika historia ya soko la muziki Afrika Kusini. 
Mwaka 1996 haukuwa mwaka mzuri kwa Rebecca kwani alimpoteza baba yake mzazi, kaka yake na dada yake. Wote walifariki katika mazingira ya kutatanisha wakifuatana. 
Lakini hili halikumfanya Rebecca kukata tamaa na kuacha huduma bali alisonga mbele na kazi hiyo akijipa moyo na kuamini ni mpango kutoka kwa Mungu mwenyewe na hataacha kumtumikia. 
Rebecca anasema siri ya mafanikio yake ni kujituma, kuwa na malengo na kufanya kazi kwa bidii akimshirikisha Mungu hayo ndiyo yaliyomfanya kutawazwa Malkia wa muziki wa injili Afrika huku wengi wakimfananisha na marehemu Brenda Fassie. 
Kati ya mwaka 1995 na 2004 Rebecca amezunguka ulimwenguni akiwa na bendi ya Pure Magic akimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji. 
Mwaka 2003 Malope alitunukiwa udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Natal kwa mchango wake mkubwa kwa jamii na muziki nchini Afrika kusini na Desemba mwaka huo huo alishinda tuzo ya Kora kwa upande wa mwanamuziki bora wa Injili. 
Licha ya kuwa mwimbaji Mwaka 2004 Malope alianzisha kipindi chake katika luninga kikiitwa ‘Gospel time’ ambacho kinafanya vizuri hadi sasa. 
Februari 25 mwaka jana  Malope alirekodi nyimbo za ‘live’ katika jiji la Pretoria hiyo ikiwa ni albamu ya 32. 
Baadhi ya Tuzo ambazo Dkt. Rebecca Malope amewahi kutunikiwa ni 1994 mwimbaji bora, 1997 albamu bora sokoni iliyoitwa ‘Uzube Nam’, 1998 muimbaji bora wa nyimbo za injili Afrika na albamu bora katika mauzo iliyoitwa ‘Angingedwa’. 
Nyingine ni 1999 muimbaji bora wa kike na muimbaji bora wa injili Afrika kupitia albamu ya ‘Somlandela’, 2002 msanii bora wa nyimbo za injili akishinda na wimbo wa ‘Sabel Uyabizwa’, 2003 msanii bora Afrika kupitia wimbo wake wa ‘Iyahamba Lenqola’ na 2004 msanii bora wa mwaka kwa wimbo wa ‘Hlala Nami’.

No comments:

Post a Comment