TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

MICHEPUKO YA MAGARI, BAJAJI NA BODA BODA KATIKA BARABARA MPYA NA ZA ZAMANI ZIMEKUWA CHANZO CHA AJALI JIJINI DAR.

Katika jiji la Dar es Salaam, Ujenzi wa Barabara Unaendelea ambao kwa asilimia 80 unaelekea kukamilika tena kwa kiwango kizuri kwa mkandarasi kwa kuwa upande wa Serikali sina hakika kama baada ya Muda Gani watavunja na kujenga Ingine, Tanzania ususani serikali inayoongozwa na watu wetu wenyewe imeendeleakuwa na tabia ya kufanya mabadiliko ya rasilimali bila kufuata utaratibu wa matwaka ya watu wanaoishi ndani yake.

Katika Kipindi hiki cha Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete na Safu ya Mawaziri wake wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa suala la usumbufu wa Barabara kwa kujenga Barabara nyingi nchini Tanzania kwa kiwango kizuri cha ubora wa Barabara Duniani, kitu ambacho kilikuwa tatizo kwenye miaka ya nyumba ususani hata wakati wa utawalawa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,  Utawala wa Mwinyi na Mkapa.

Pamoja na kwamba Barabara hizi zimejengwa ajili yetu wenyewe, lakini barabara hizi hizi zimekuwa tatizo kwetu maana hata ajali zingine pia zinatokea kwa kuwa tunashindwa kuzitumia ipasavyo barabara hizi,  zaidi ikiwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kama vile Pikipiki, Baiskeli na Magari.
Wajenzi wa Barabara hizi bila shaka Magufuli na watu wake(Wakandarasi) wanatambua jinsi taratibu za wapitaji wa vyombo vya usafiri wanavyopaswa kupita wakati zitakapokuwa tayari zimeamuliwa kutumika,
kwa sasa watumiaji wengi wa barabara ususani hizi mpya wanashindwa kuelewa jinsi itakavyokuwa zinatumika kwa kuwa kuna baddhi ya ya maeneo ambayo imeyalazimu magari kupita moja tu kwa maana hakuna eneo la kupishana gari na gari yaani iwe kwenda nyumba wala kupita gari ingine ili uwe mbele, kwa maana hiyo aliye wa mbele hatazidi kuwa mbele na wa nyuma kwa nyuma.
sasa swali  liliko ndani ya vichwa vya watu wengi ni jinsi gani itakavyokuwa wakati itakapokuwa inaharibika gari ya mbele wakiwa safari moja, kwa maana hakutakuwa na njia mbadala ya gari ingine kupita kupisha hilo,  kingine ni jinsi barabara hizo zinavyotakiwa kutumiwa na madereva walioiva katika kazi ya Udereva, maana badala ya njia kutengenezwa zimenyooka, barabara hizi za KIKWETE zimepinda pinda si kwa uharibifu bali kwa maboresho ya kiufundi zaidi ususani  ni fahari kwa Dereva Bora amabaye ni hodari kwa kazi ya kuongoza gari wakati wote wa Safari yake Barabarani.
kinacho nishangaza mimi ni kwa jnsi gani Magufuli ameshindwa kuitumia fulsa hii kuhakikisha anaweka Madaraja ususani maeneo ya Maungio zinapotumika Taa, na badala yake ingewekwa Madaraja kamailivyo kwa nchi zingine Duniani, kwa kuwa gharama iliyotumika na muda uliotumika, na Uongozi uliotumika kufanya haya hauta kuja tena kutokea nna kufanya haya katika kizazi hiki hakika.

Kazi kubwa sasa imebaki ni kwa wazazi wa watoto wa mijini zaidi wale wa maeneo hayo zilipojengwa hizo barabara kuwajengea misingi imara watoto ya kutokatiza hovyo barabarani kwa kuwa ivi sasa ongezeko la kugongwa litakuwa kubwa ukilinganisha na barabara za zamani ambazo kati ya barabara na barabara kuliachwa mwanya wa mtu kupumzika na kusubiri kuvuka upande wa pili.
Nikupongeze tu Magufuli na Wafuasi wako wote kwa Ujasiri wako, ambao umefanikisha kwa kiwango hicho kufikia hatua zilizopo za kukamilisha ujenzi wa barabara zetu za Tanzania ususani hizi za ndani ya majiji na Zinazoingia Mijini, maana umepambana bila woga, na Umefanya kwa ajili ya Watu na si kwa ajili yako bali kwa ajili ya Taifa na Kizazi kijacho.
Pia Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Mrisho, kwa kuweka mkazo usimamiaji wa Maendeleo ususani Barabara
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu, mchimati@gmail.com 
   Hii ajali imetokea maeneo ya Manzese  Hawa wanachepuka hata hawajielewi  Mbele kidogo hapa mchepuko tutafika? 

No comments:

Post a Comment