TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 17, 2014

Kiingilio Tamasha la Krismasi 5000

index
Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi iliyo katika kampuni ya Msama Promotions, imetangaza kiingilio cha shilingi 5000 kwa wakubwa katika tamasha hilo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, linalotarajia kuanza Desemba 25-28. Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Abihud Mang’era watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo. Mang’era alisema tamasha hilo Desemba 25 litafanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine, Desemba 26 litafanyika mkoani Iringa kwenye uwanja wa Samora na Desemba 28 Wilayani Songea kwenye uwanja wa Majimaji. Aidha Mang’era alisema viingilio hivyo vitakidhi haja ya wakazi wa mikoa hiyo wenye kiu ya kupata neno la Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini watakaojitokeza kwenye tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment