TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 18, 2014

Serikali yatakiwa kuwachukulia hatua waliohusika na wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Chama cha demokrasia na  maendeleo-Chadema- kimeitaka serikali kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani viongozi waliohusika katika wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta -Escrow- licha ya wengine kuandika barua kujiuzulu wadhifa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari, naibu katibu mkuu wa Chadema, Mhe.John Mnyika amemtaka rais Jakaya Kikwete kuyafanyia kazi maadhimio ya bunge ya kuwaondoa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria viongozi hao, hata kama watajiuzulu nyazifa zao.
 
Akielezea uchaguzi wa serikali za mitaa, naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar Bwana Salum Mwalimu amemtaka waziri wa tamisemi Mhe. Hawa Ghasia kutangaza matokea chaguzi za serikali za mitaa kwa nchi nzima badala ya kuwahachia viongozi wa vyama vya siasa kuendelea kuwadanganya wananchi kuwa vyama vyao vimepata ushindi wa kishindo.
 
Kwa upande wake baadhi ya wananchi wameitaka serikali kufuatilia ajira za wageni katika baadhi ya benki nchni kutokana na ongezeko la wizi ambao yanaambatana na baadhi ya watendaji kujiuzulu nyadhifa zao baada ya muda.

No comments:

Post a Comment