TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 17, 2014

MNENGUAJI AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA

madindaaisha
Aisha Madinda wakati wa Uhai wake

Aliyekuwa Mnenguaji na Muimbaji wa Bandi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda amefariki dunia hivi punde Jijini Dar es salaam. Habari imethibitishwa na mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta Asha Baraka. Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.
“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Amesema Asha Baraka
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina Kwa hisani ya http://www.jamiiforums.com

No comments:

Post a Comment