TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 17, 2014

SERIKALI YATENGUA UTEUZI WA WAKURUGENZI

unnamed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kuwasimamisha kazi baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali hapa nchini na wengine kutenguliwa kwa uteuzi wao kutokana na kushindwa kusimamia vyema uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mapema hivi karibuni kote nchini.kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Jumanne Sagini,Kulia ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Kagyabukama Kilima.
……………………………………………………………………………………………
Na: Frank Mvungi- Maelezo

Serikali yatengua uteuzi wa wakurugenzi sita (6) wa Halmashauri mbalimbali hapa nchini walioshindwa Kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi huo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Hawa Ghasia wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam uliolenga kutoa taarifa ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kwa wale wote walisababisha kasoro mbalimbali katika uchaguzi huo.
Akitaja majina ya Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa Mh. Ghasia amesema kuwa ni Bw. Benjamin A. Majoya ambaye Alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuranga,Bw.Abdalla Ngodu Mkurugenzi Mtendaji Kaliua,Bw.Masalu Mayaya Mkurugenzi Mtendaji Kasulu,Bibi Goody Pamba Mkurugenzi Mtendaji Serengeti,Bw.Julius A. Madiga Mkurugenzi Mtendaji Sengerema na Bw. Simon C.R. Mayeye Mkurugenzi Mtendaji Bunda.
Akizungumzia wakurugenzi waliosimamishwa kazi Mh. Ghasia amesema ni watano (5) ili kupisha uchunguzi Zaidi wa Kiwango cha ushiriki wao katika kasoro zilizojitokeza kwenye Halmashauri zao ambao ni Bw.Felix T. Mabula wa Hanang, Bw. Fortunatus Fwema wa Mbulu,Bibi Isabella D. Chilumba wa Ulanga,Bibi Pendo Malabeja wa kwimba na Bw. Wiliam Z. Shimwela wa Manispaa ya Sumbawanga.
Kwa upande wa Wakurugenzi waliopewa Onyo Kali na ambao watakuwa chini ya uangalizi kubaini kama wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi Mh. Ghasia amesema kuwa ni watatu (3) ambao ni Bw. Mohamed A. Maje wa Rombo,Bw. Hamis Yuna wa Busega,Bw. Jovin A. Jungu wa Muheza.
Pia Mh. Ghasia aliwataja wakurugenzi watatu (3) waliopewa onyo na kutakiwa kuongeza umakini wanapotekeleza majukumu yao ambao ni Bw. Isaya Mngulumi Manisapaa ya Ilala,Bw. Melchizedeck Humbe Humbe wa Hai na Bw. Wallace J. Karia wa Mvomero.
Akitoa Wito kwa watumishi wa Umma na Viongozi wa Sekta ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Ghasia amesema kila mmoja anao wajibu wa kutekeleza kwa weledi na uadilifu ili kuepuka kasoro zinazoweza kuepukwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ilitimiza wajibu wake wa kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa ukamilifu kwa kutoa miongozo na mafunzo kwa watendaji wa Halmashauri ambapo Mikoa na Halmashauri ziliwezeshwa kwa fedha ili kugharimia maandalizi muhimu ikiwa ni pamoja na kuandaa vifaa na karatasi za kupiga kura.

No comments:

Post a Comment