WATANZANIA WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI SHINDANO LA KUONGEZA KIPATO
“Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili
kuleta zaidi upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za
kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na
dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa
kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.
Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za vijijini barani Afrika
hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za
familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao
yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha
wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master
Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko
chanya.
MGODI WA DHAHABU WA BULHANHLU WAINGIA MAKUBALIANO NA TAASISI YA BENJAMINI WILLIAM MKAPA YA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akibadilishana hati za
makubaliano na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa,Dkt Ellen
Mkondya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati hizo iliyofanyika
wilayani Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew pamoja na Afisa Mkuu wa
Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt Ellen Mkondya wakitia saini katika
hati za makubaliano ya kuboresha mradi wa huduma ya afya ,Zoezi la
utiaji saini ulishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita
Kawawa(kulia) ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa
(nyuma ya mkuu wa wilaya) pamoja na viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu
,Elias Kasitila na Mganga Mkuu wa wilaya ya Msalala Dkt Hamad Nyembea.
Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Graham Crew akizungumza mara baada ya
kutiliana saini makubaliano ya kuboresha huduma za Afya na Taasisi ya
Benjamini William Mkapa wakati wa hafla iliyofanyika katika mji wa
Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akitoa neno la shukrani kwa
uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa michango ambao wameendelea
kutoa kwa wilaya ya Kahama na Msalala.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Mhe. Ummy Mwalimu
(IMb) akisoma taarifa ya Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma, 11
Mei, 2016.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akifurahi na Wabunge wenzie nje ya
Bunge mjini Dodoma.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.




Mtaalam
Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akieleza jambo kwa
waandishi wa habari juu ya kushiriki shindano la kuongeza kipato
lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa makundi yanayoruhusiwa
kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo
ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa
kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael
Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya
kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha
mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo,
Mkuranga
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii
Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.














Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Juliana Pallangyo (pichani) akisoma hotuba ya ufunguzi wa
mkutano wa siku tatu jijini Dar es Salaam uliokutanisha wataalam
kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam
mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani
Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro
nchini Uganda.
Wataalam
mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Juliana Pallangyo ( anayeonekana mbele kwa mbali)
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Juliana Pallangyo (wa nne kutoka kushoto waliokaa mbele)
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya
ufunguzi.
Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent
Mungy akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu tathmini ya hali halisi
kuelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini ifikapo mwezi june
2016 ambapo kiwango cha simu Bandia Kimepungua kutokana na Elimu
inayotolewa na Mamalaka hiyo kwa wananchi. Kulia ni Afisa Habari wa
Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
Kaimu
Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) toka
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Injinia Gabriel Mruma akiwaeleza
waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia
simu zenye ubora unaokubalika ili kuepuka athari zinazotokana na
matumizi ya simu Bandia. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy .(Picha na Hassan
Silayo- MAELEZO ).
Katibu
mkuu: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi
Joseph Nyamhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza
kutozwa kwa vyombo vya usafiri vitavyopita katika Daraja la Nyerere
kuanzia jumamosi ya Mei 14.(Picha na Raymond Mushumbusi) MAELEZO
John
Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka
WARAMI akizungumza na waandishi wa habari Kwenye Hoteli ya Tamarin
Mwenge jijini Dar es salaam kuhusu Sakata la Sukari ambapo amempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa
jinsi anavyothubutu kuwatetea watanzania waliowanyonge katika masuala
mbalimbali na hasa katika suala zima la uhaba wa sukari.
Makdeo
Makeja mratibu msaidizi WARAMI akifafanua jambo wakati viongozi hao wa
taasisi ya WARAMI walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam , kulia ni John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa
Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka
kwenda London Uingereza Mai 10 , 2016, kumwakilisha Rais John Magufuli
kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi wa kujadili masuala ya kupambana na
rushwa duniani.(Picha n Ofisi ya Wziri Mkuu).



No comments:
Post a Comment