TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, May 15, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWARAIS MTEULE WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI

  RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI UGANDA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWARAIS MTEULE WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI


MAADHIMISHO YA MIAKA SITA YA CHAMA CHA WATANZANIA WALIOSOMEA CHINA (CAAT)

Klabu Ya Waandishi Wa Habari Mkoa wa Shinyanga Yaanza Kuwatumbua Majipu "Waandishi wa Habari Hewa"


SERIKALI MKOANI MBEYA YAFUTA HATI YA KIWANJA CHA MAKAZI KILICHOTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Picha Maktaba) 
Na EmanuelMadafa,Mbeya(Jamiimojablogu)
SERIKALI Mkoani Mbeya imeagiza kufutwa kwa hati ya kiwanja kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha maji kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.
Agizo hilo, limetolwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kutembelea na kukagua chanzo kikuu cha maji cha Nzovwe, chenye uwezo wa kuzalisha mita 12 za ujazo kwa siku na kusambaza maji kwa asilimia 41 kwa wakazi wa jiji la Mbeya wapatao zaidi ya 200,000.
Kiwanja hicho ambacho kipo karibu na eneo la chanzo cha maji cha Nzovwe, kilitolewa na maafisa ardhi, idara ya mipango miji kwa ajili ya matumizi ya makazi na kumilikiwa na mtu binafsi aliyetajwa kwa jina moja la Mwakasala.
Makala amesema, chanzo hicho cha maji ndio tegemezi kwa kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa Jiji la Mbeya, hivyo kama kitaachwa na kuharibiwa, wananchi zaidi ya 200,000 wapo hatarini kuikosa huduma hiyo ambayo ni haki yao ya msingi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali iliwaondoa wananchi wote waliokuwa wanaishi au kuendesha shughuli zao za kiuchumi ndani ya mita 60 na kuwalipa fidia zao hivyo hatua ya wananchi hao kuendelea kuishia mahali hapo ni kukaidi agizo la serikali.
Amebainisha kuwa kiwango kikubwa cha upotevu wa maji kwa asilimia 31 inatokana na baadhi ya vyanzo vya maji kuharibiwa kwa kufanyika kwa shughuli za kibinadamu, kulisha mifugo au kujenga nyumba za makazi pamoja na mabadiliko ya kihaidrolojia.
Hata hivyo, Mkuu huyo aliutaka uongozi wa mamlaka ya maji kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, kuhakikisha wanalisiamamia zoezi hilo la kumondoa mvamizi huyo ndani ya siku tatu.
“Wananchi wengine wameondoka tena kwa hiari yao wenyewe, sasa kwa nini huyu atuchezee mchezo mchafu?.. kwa hili sikubaliani nalo, huku akiwataka wananchi ambao ni vijana kulilinda eneo hilo na kuwaonya wale ambao watakubali kutumiwa na mtu au watu kufanya fujo,”alisema.

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUTUMIA MIFUMO YA KIUTENDAJI



Mkurugenzi Msaidizi ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Veila Shoo alisema hayo wakati akitoa takwimu za matumizi ya mifumo hiyo katika kikao kazi kilichohusisha wawakilishi kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Bi. Veila alieleza kuwa ufuatiliaji wa mifumo umefanyika katika Idara Zinazojitegemea 16 ambapo imebainika baadhi ya mifumo inatukima ipasavyo wakati mingine bado.
Awali, akifungua kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba alisema kuwa zoezi la kufanya ufuatiliaji wa mifumo ni endelevu na watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutumia mifumo hiyo.
Alisema lengo la tathmini hiyo ni kupata takwimu za utekelezaji wa mifumo na viwango vya utendaji kazi, kutambua mifumo yenye changamoto za utekelezaji, kutoa hamasa ili kuboresha utoaji huduma na kutoa mrejesho kwa taasisi jinsi ya kuimarisha mifumo.
Mifumo iliyofanyiwa tathmini ni pamoja na:- Mpango mkakati Mkataba wa Huduma kwa Mteja; Mfumo wa wazi wa Tathmini ya Utendaji kazi; Uboreshaji wa michakato ya Utoaji huduma; Tathmini ya Utoaji huduma wa Taasisi; Tathmini ya ndani ya Taasisi; Ushirikiano wa Taasisi ya Umma na Asasi za Kiraia(AZAKI); Waraka Namba 1 wa mwaka 2012 kuhusu Ununuzi wa Samani za Ofisi; na Usimamizi wa Fomu za Serikali. 

JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA









VIKUNDI 39 VYA WANAWAKE WILAYANI MOROGORO VYAPATIWA MIKOPO YA SHILINGI MILIONI 23.8









SERENGETI BOYS KUONDOKA LEO







WAKURUGENZI WA BODI YA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA,TAFORI NA TTB WATEULIWA.











WATEJA WA “RAHISI inayowezeshwa na AccessMobile”KUTOKA AccessBank KUNUFAIKA KWA ZAWADI MBALIMBALI






No comments:

Post a Comment