TANAPA KUBADILI MFUMO WA UTENDAJI KAZI KUTOKA KIRAIA KUWA JESHI USU
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan
Kijazi akizungumza wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo
wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa .

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal
Shelutete (kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea
katika hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa
Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .

Mhifadhi Sekela Mwangota akisoma risala ya Wahitimu wa Mafunzo ya
Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa
kuhitimisha mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa
shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya
Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
CHURA KUJAKIVINGINE.
Meneja
wa msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura), Hemed Kavu akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba radhi wa
tanzania kwa video ya wimbo wa Msanii Snura na wimbo wake wa Chura.
Snura
amesema kuwa yupo tayari kufanya upya video ya Wimbo wake wa chura
ambayo itafuata maadili ya kitanzania kwani tayari ameshachukua vibali
vya kufanya upya video ya wimbo huo.Msanii Wa Bongo Movie
Snura Mushi (Snura) amewaomba radhi watanzania kwaujumla pamoja na
vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria
na kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube.
Msanii
Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) awaomba radhi watanzania kwa kufanya
video isiyo na maadili ya kitanzania ya wimbo wake wa Chura ameomba
radhi watanzania mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.VYOMBO VYA HABARI ASILIA (wa makaratasini) HOI BIN TAABAN WAKATI VYA digitali (wa mitandaoni) VYAPETA
Vyombo
vya habari vya asilia, hususan magazeti, vinakufa. Hivi sasa vvyombo
hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu na mdororo wa mapato
kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.
Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 ("State of the News Media 2015,”) imeonesha
kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na
TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu.
Utafiti
huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni
wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo
gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala
zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni
.
Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano
ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini
hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni changa sana kuweza kutishia
amani ya magazeti.
Upande
wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza
kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao,
maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya
magazeti.
Upande
wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi
anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini
wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya
tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio
magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) juu ya tuzo ya kimataifa ya viwango iliyotolewa
na International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM)
kwa bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey
Mbanyi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) vitabu vya mtaala mpya wa mafunzo ulioanza na Bodi ya
wataalamu ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB)Desemba mwaka 2015 kulia ni
mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey Mbanyi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) tuzo ya viwango vya kimataifa kutoka International
Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM) iliyotolewa kwa
bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey
Mbanyi.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa
akijibu maswali ya papo kwa papo yanayoulizwa na Wabunge leo mjini
Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwasili viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Wabunge wakiwasili viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.(Picha na Eleuteri Mangi-MALEZO, Dodoma).




Kulia ni Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) na Kushoto ni meneja wa msanii huyo, Hemed Kavu.




Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James
Mataragio (mbele) akielezea mikakati ya shirika hilo katika matumizi ya
gesi asilia inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na
nyingine kuuzwa katika soko la nje katika kikao kilichokutanisha Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo kilichofanyika jijini Dar es
Salaam. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili matumizi ya gesi
iliyogunduliwa nchini katika matumizi ya ndani na nyingine kuuzwa nje
ya nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya
nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (pichani) akisisitiza jambo
katika kikao hicho.
Wataalam
kutoka Idara ya Nishati kutoka kushoto, Mussa Abbas na Athur Lyatuu
wakinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katika kikao hicho.
Wataalam
kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini
wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika
kikao hicho.
Mkuu
wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi
ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa
sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali sura 182 ili kuzuia athari
zinazoweza kujitokeza kwa wasafirishaji na watumiaji wa kemikali hapa
nchini. Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank
Mvungi na kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw.
Sylvester Omari.
Mkuu
wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi
ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa
shughuli za usafirishaji wa kemikali na madereva 123 hapa nchini. Kulia
ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Sylvester Omari.








Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Zawadi Msalla (katikati) akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapopichani) wakati akitoa tamko la
Serikali kuhusu kusitishwa kwa wimbo wa Msanii Snura Mushi ujulikanao
kwa jina la Chura kwa kukiuka maadili kushoto ni Mwanasheria wa wizara
hiyo Bw. Patrick Kipangula na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Utamaduni Bibi. Lily Beleko.
Mwanasheria
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Patrick Kipangula
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapopichani) wakati wizara
hiyo ikitoa tamko la kusitishwa kwa wimbo ujulikanao kwa jina la Chura
ulioimbwa na msanii Snura Mushi kwa kukiuka maadili, kulia ni Kaimu Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi. Zawadi Msalla.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Kaimu Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
naMichezo Bi. Zawadi Msalla (hayupopichani) wakatia kitoa tamko la
Serikali kuhusu kusitishwa kwa wimbo wa Msanii Snura Mushi ujulikanao
kwa jina la Chura kwa kukiuka maadili.
No comments:
Post a Comment