Mkurugenzi
wa Kinga Jeshini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni
Kanali Charles Emilio Mwanziva akiongea na mwandishi wa habari kutoka
Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Luis Velarde wakati wa
ziara ya waandishi hao katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT
iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa
malaria.
Mtaalamu
wa maabara katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo
mkoani Tanga akiendelea na kazi ya kufanya vipimo vya malaria kwa
kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) ambayo majibu yake
hutolewa baada ya dakika 15.
Waandishi
wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa
tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
kituo cha Korogwe.
Mtaalamu
wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja akifafanua jambo kwa baadhi ya
waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini
Marekani walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania
inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Waandishi
wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani
wakimsikiliza Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja (hayupo pichani)
walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na
ugonjwa wa malaria.
Familia
ya Salumu Rashidi wa kijiji cha Masatu kilichopo wilaya ya Korogwe
mkoani Tanga wakiwa na mtoto wao Mohammedi Salimu ambaye ni miongoni mwa
watoto waliopo kwenye mradi wa kudhibiti malaria wilayani huo. Kushoto
ni mama yake Mohammedi Monica Mugunda.
Vijana
wa Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) wakitumbuiza wakati wa zaira ya
waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini
Marekani walipotembelea zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo
mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa
malaria.(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Tanga)UPDATES: MSIBA WA MTOTO WA ANKAL ISSA MICHUZI
Ukitokea
Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement Wazo, mbele mkono wako
wa kulia utaona Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona
uzio wenye rangi ya njano umeandikwa Twiga Cement, unakatisha hapo
upande huo huo wa kulia. ukikatisha tu utaona kuna mtaa mwingine
unaingia upande wa kulia, uache na usogee mbele, utaona mtaa mwingine
unaingia kulia, ingia nao huo na utakuwa umefika msibani.













NAIBU
Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameliambia
Bunge Mjini Dodoma, leo tarehe 12 Mei, 2016, kwamba serikali inaandaa
sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2016, itakayosimamia na
kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo




















No comments:
Post a Comment