Katibu
wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Nd. Epi Fania Ngonyani
akibadilishana mawazo na Balozi Seif akijiandaa na ujumbe wake kuondoka
Bandarini Malindi kurejea Mjini Dar es salaam baada ya kumaliza ziara
yao ya ujirani mwema. Nyuma ya Ndugu Ngonyaji ni Mwenyekiti wa CCM wa
Tawi hilo Ndugu Haroub Othman Mberwa.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Ujumbe
Viongozi wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kinondoni
Mjini Dar es salaam katika Banadari ya Malindi baada ya kumaliza ziara
yao ya ujirani mwema Visiwani Zanzibar wakiwa wenyeji wa Tawi la CCM
Vikokotoni Mjini Zanzibar.Shirika la ndege la Etihad latoa taarifa kuhusiana na msukosuko wa Ndege yake Indonesia.
Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na
kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote
za matibabu.
Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao
wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na
Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi
wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo
walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma
waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni
ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu
ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa
usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”
Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao.
MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA UMEME WA GESI TOKA JAPAN
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya
Japan, Bw. Norio Shoji baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe
wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo
ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia
kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) .





Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia)
akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la
Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati
fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika
mtaji wa benki ya NMB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati)
akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji
wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika
mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB,
Waziri Barnabas na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la
Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia)
akizungumza jambo na Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri
Barnabas (kushoto), katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani
zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya
NMB.


Mkurugenzi
wa Masoko ya Fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Alexander
Ng’winamila (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
leo Jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji kwenye dhamana za Serikali.
Kulia ni Meneja Msaidizi Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BOT Bi. Victoria
Msina na Kushoto ni Meneja Msaidizi Masoko ya Ndani wa BOT Bw. Genes
Kimaro.
Meneja
Msaidizi Masoko ya Ndani wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Genes
Kimaro (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
Jijini Dar es Salaam kuhusu aina na faida za uwekezaji kwenye dhamana za
Serikali.PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

Mwenyekiti
wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa
Tanzania nchini Japan, Balozi Mathias Chikawe, Balozi huyo alipofika
kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es
Salaam,jana, Mei 9, 2016.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Balozi Mpya wa Tanzania
nchini Japani, Balozi Mathis Chikawe, baada ya mazungumzo yao, Balozi
huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.
Balozi
wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba akisaini kitabu cha
wageni, alipofika kumuaga Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya
Kikwete, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es
Salaam, jana.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania
nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba, Balozi huyo alipofika kumsalimia
katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana,
Mei 9, 2016.(Picha na Bashir Nkoromo).


Kamanda
wa Jeshi la Polisi ACP Paul Kasabago akipokea mfano wa hundi yenye
thamani ya TZS. 6,200,000/= iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni LAPF
kuwezesha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania
(medical wing) mjini Tabora. Wanaokabidhi kutoka LAPF ni Mkurugenzi wa
Huduma kwa wanachama Bw. Valerian Mablangeti, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu Bw. Desdery Sigonda pamoja na Meneja Kanda ya Dar es
Salaam Bi. Amina Kassim.
Mkurugenzi
wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. Valerian Mablangeti
akitoa mada kuhusu Mfuko ikijumuisha maandalizi kabla ya kustaafu,
Maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi wakisiliza kwa makini katika
kongamano la jeshi hili lililofanyika mjini Tabora hivi karibuni.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakifuatilia kwa makini mada toka Mfuko
wa Pensheni LAPF kwenye kongamano la Jeshi hili lililofanyika mjini
Tabora ambapo maafisa hao walivutiwa na kujiunga na mfuko wa uchangiaji
wa hiari ikiwa ni maandalizi kabla ya kustaafu.
Mmoja
ya Maafisa waandamizi walioshiriki kongamamo la jeshi la Polisi mkoani
Tabora hivi karibuni akiuliza namna ya kujiunga kwa hiari na Mfuko wa
Pensheni wa LAPF mara baada Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama
kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitoleawazo na Mfuko wa
Pensheni wa LAPF.



























No comments:
Post a Comment