TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, May 15, 2016

UPDATES: MSIBA WA MTOTO WA ANKAL

TAMASHA LA PILI LA MAVAZI YA STARA KUZINDULIWA

WATEJA WA MARA KWA MARA WA TSN SUPERMARKET/HYPERMARKET WAPEWA “LOYALTY VOUCHERS’






FIRST NATIONAL BANK WAFUNGUA TAWI MWANZA.






WALIOFICHA SUKARI WAASWA KUIFICHUA MARA MOJA.









ADC Yawafuta Uanachama Wanachama wake Wanne Akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho

Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uanachama wanachama wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Said Miraaj,Katibu Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi Bwana Jumanne Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar.

Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid amesema katiba ya chama inasisitiza ushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama katika mikakati yake ya kuchukua dola.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Bwana Sisty Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki uchaguzi kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya kuanzishwa chama Chochote cha siasa na kusisitiza ipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki katika chaguzi.

Aidha katika mkutano mkuu huo, wajumbe wamemchagua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.

Rais Magufuli asali ibada ya Jumapili Arusha Mjini atoa neno









RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA KUPAA KWA BWANA KATIKA PAROKIA YA TOLEO LA BWANA JIMBO LA ARUSHA

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA MAMA MJINI DODOMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasiriamali wadogowadogo kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajasiriamali wadogowadogo wakifuatilia maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi cheti mmoja kati waliofanya vizuri kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tunzo alizokabidhiwa na UWT Taifa kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke kwenye maadhimisho ya siku ya Mama yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,alipokua akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wanawake kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe za kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais Mwanamke wa kwanza yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

Vikundi mbalimbali vya Ngoma Vikitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Wanawake na Wananchi wa Dodoma baada ya kuwahutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.(Picha na OMR)

MTANGAZAJI WA CNN RICHARD QUEST AFURAHISHWA NA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA KATIKA MAONESHO YA INDABA


Kwa mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .Katika siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini.. Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. Baadhi ya wagenimbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya Utalii ya Indaba yanayofanyika katika jiji la Durban nchini Afrika Kusini. Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian na Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. wakiwa na mmoja wa wageni aliyetembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini. Baadhi ya wageni wakipata taarifa mbalimbali kutoka katika banda la Tanzania. Wageni mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania.

No comments:

Post a Comment