TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, June 14, 2016

DAWASCO YAAHIDI KUPUNGUZA KIWANGO CHA UPOTEVU WA MAJI KWA ASILIMIA 45


Mafundi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dawasco wakiendelea na operesheni ya kudhibiti mabomba ya maji ya nayovu, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dawasco,Cyprian Luhemeja akimkabidhi ndoo ya maji Bi Asha Muhamed malabaada ya kumrejeshea maji nyumbani kwake Sinza leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).


SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) limesema linatarajia kupunguza kiwango cha upotevu wa maji hadi kufikia asilimia 45 mwishoni mwa mwezi huu. Akizungumza wakati wa operesheni ya kudhibiti mabomba ya maji ya yanayovujisha pamoja na Kuwaunganishia maji wateja waliokatiwa kutokana na madeni katika mtaa wa Sinza jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dawasco, Mhandisi, Cyprian Luhemeja, amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 62 hadi kufikia asilimia 47 kutokana na opresheni ambazo wamezifanya. Amesema kuwa, kwa siku mitambo ya inazalisha maji yenye thamani ya Sh.Bilion 11 ukipoteza maji kwa asilimia 45 ni sawa na kupoteza Sh.Bilioni 5. Amesem, upotevu wa maji unapunguza juhudi za Serikali za kupunguza tatizo la maji vijijini kutokana na hasara kubwa inayopatikana kwa upotevu wa maji. Amesema kuwa wanatumia kubwa gharama ya kutibu maji kwa dawa lakini maji hayafiki kwa wateja kwani yanaishia njiani kutokana na miundombinu mingi kuwa ya zamani. Luhemeja amesema suala la kutengeneza miundombinu yote inayopoteza maji njiani na wameanzia eneo la Sinza E katika mitaa 26 kutengeneza mabomba hayo. Aidha amesema katika hatua nyingine alitoa ofa ya kumlipia kiasi cha Sh.200,000 Asha Muhammed mkazi wa Sinza E aliyekatiwa maji kwa kudaiwa ankara kwa muda mrefu na kushindwa kulipa kutokana na ugumu wa maisha. Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Sinza E, Kassim Kabulluh, alisema eneo lake lilikuwa na kero kubwa ya maji kuvuja na kusababisha uharibifu wa barabara

No comments:

Post a Comment