TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 16, 2016

KAMATI YA MAWASILIANO MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO.


Katika semina hiyo, watumiaji wa hudumza za mawasiliano ikiwemo simu pamoja na vyombo vya habari ambao waliwakilisha makundi mbalimbali kama vile wanahabari, wajasiriamali na walemavu, walipewa elimu juu ya uwepo wa Kamati hiyo pamoja na uwepo wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC).

Pia walielimishwa juu ya mwongozo wa kuwasilisha malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC) ambapo iliambatana na viongozi wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza kujitambulisha kwa baraza hilo.

Watumiaji wa huduma za mawasiliano walielezwa kwamba ni wajibu wao kuwasilisha malalamiko yao ikiwa wanapokea huduma zilizo chini ya kiwango ama ikiwa wana malalamiko ya aina yoyote kuhusu huduma za mawasiliano.

Walihimizwa kuwasilisha malalamiko yao kwa kuanza na mtoa huduma, yasiposhughulikiwa wanawayawasilisha katika Kamati ya Huduma za Mawasiliano mkoa, yasipotatuliwa yatawasilishwa katika Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka TCRA na hata ngazi nyingine zaidi hadi pale utatuzi utakapofanyika.

Semina hiyo ilionekana kuwafungua ufahamu watumiaji wa huduma za mawasiliano jijini Mwanza kwani baadhi yao walieleza kuwa awali walikuwa hawatambui haki na wajibu wao katika kutumia huduma za mawasiliano.
Baadhi ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza, wakiwa katika semina ya kuwaelimisha juu ya Matumizi ya Huduma za Mawasiliano.Picha Zaidi

No comments:

Post a Comment