TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 15, 2016

JASPER MAKALA WA MCDI KILWA ATWAA TUZO NYINGINE HUKO USA


Mkurugenzi wa MCDI,Jasper Makala(Kulia) Akipokea Tuzo ya ya Mwaka 2016 Utunzaji na Uhifadhi wa Misitu toka kwa Dr Gary Knel.Afisa Mtendaji Mkuu Geographic Society jana huko USA.


Jasper Makala Akikabidhi Tuzo ya Whitley Award Kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi.

Na Abdulaziz Video,Lindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhifadhi mpingo na maendeleo(MCDI) Mr Makala Jasper(Kulia)Usiku wa jana huko Washington DC-USA Ameibuka Kidedea baada ya kushinda Tuzo ya mwaka 2016 iitwayo National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation.Tuzo hiyo ina thamani ya Dolla 25,000.

Jasper Makala Mkurugenzi wa MCDI Yenye makao makuu yake Kilwa Masoko Mkoani Lindi ameiwakilisha vyema Africa na Tanzania Ambapo kwa Kushinda Tuzo hiyo. Ushindi huo ni Baada ya Kuwashinda Wasiriki wengine 30 Toka bara la Africa na Wenye Uwezo mkubwa na kufanya mchuano kuwa mkali sana.


Iikumbukwe hii ni tuzo ya pili ndani ya miezi miwili ambapo Makala Jasper aliwania tuzo za Whitley huko nchini Uingereza ambapo pia alishinda tuzo hiyo ambayo ilikuwa na thamani ya Paundi £35, 000.Zaidi ya Milioni 100 za Kitanzania.Ushindi huo unatokana na Mawasilisho ya Utunzaji Shirikishi na Uhifadhi wa Misitu
MPALULEBLOGS:

No comments:

Post a Comment